WHO: Zaidi ya watu milioni 40 wa miaka 13 – 15 wameanza kutumia tumbaku

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Mei 31 kila mwaka ni siku ya Tumbaku duniani, ni siku inayotumika kueleza madhara ya tumbaku duniani. Kwa mwaka huu Shirika la Afya Duniani imewekeza zaidi ya dola bilioni 9 katika miradi ya kupunguza matumizi ya tumbaku ambayo yanaua watu milioni 8 kila mwaka.

Ili kuwafikia vijana, Shirika la afya Duniani limezindua shindano lenye jina #TobaccoExposed au #TumbakuImeumbuliwa katika mtandao wa TikTok na kuwakaribisha wadau wa mitandao ya kijamii kama Pinterest, Youtube na Tiktok kuusambaza ujumbe.

WHO imeshauri watu maarufu na wenye ushawishi wakatae udhamini unaotoka katika makampuni ya tumbaku.Pia Televisheni na huduma za kurusha maudhui mitandaoni ziache kuonesha tumbaku na sigara za kielektroniki.

Mitandao ya kijamii ipige marufuku kutangazwa kwa tumbaku na bidhaa nyingine zinazohusina na bidhaa za tumbaku, serikali na sekta za kifedha ziachane na viwanda vya tumbaku pia zipige marufuku aina zote za matangazo, promosheni na udhamini wa tumbaku.
 
Back
Top Bottom