Kwa haraka haraka nani anasimama na Job ndugai humu dhidi ya Prof, Mussa Assad?
Kama hakuna hivi Ndugai hajioni kama yuko mwenyewe dhidi ya Assad na wananchi takribani milioni 40 ukitoa wa pale magogoni(kwa mujibu wa maneno yake Ndugai ni kwamba Raisi anapatiwa wakati mgumu na assad ina maana mkuu mchukia mafisadi anapatiwa wakati mgumu na mtu anaemtafutia mafisadi ),
Ndugai anatakiwa ajue kwamba Tunachukia Ufisadi,na kama kweli tunauchukia hatuwezi kupigana vita na yule anaetutafutia mafisadi,
Ndugai unatakiwa ushukuru kwa Report ya CAG iliyopo hapo mezani kwako na kuhoji pamoja na wabunge unawaongoza dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za wananchi waliokuchagua,
Tumia Bunge lako unaloliongoza kuhoji sasa matumizi ya zile Bilioni 16 zilizotumika kununulia sare za jeshi la polisi zimeenda wapi mbona sare hazionekani,
Tumia bunge unaloliongoza kuhoji zile bilioni 1:3 zilizotumika kwenye vikao 26 vya bodi pale ngoro ngoro kwa mwaka, kulikuwa na ulazima gani wa kufanya vikao vyote hivyo na kutumia pesa nyingi za walipa kodi ikiwa wewe jimboni kwako kuna wanafunzi wanakaa chini hawana madawati wala madarasa ya kutosha, kuna wananchi wako wanapata tabu hawana miundombinu ya maji wala access ya Umeme,
Tumia bunge unaloliongoza kuhoji zile bilioni zilizotumika kununulia mashine feki elfu 5,kati ya mashine elfu 8 zilizoitajika pale ofisini kwa Jaji Lubuva,
Tumia bunge unaloliongoza kuhoji zile bilioni 3 zilizopigwa na Pole pole pale Kwenye Chama chako kwa nini hazikupelekwa kwenye mifuko ya hifadhi za jamii zimeenda wapi hizo ni kodi za wananchi waliokuchagua,
Tumia bunge lako kuhoji kwa nini mbowe na chama chake watumie fedha ya ruzuku iliyotokana na kodi za wananchi kununulia gari la mamilioni kwa kutumia jina la mtu badala ya chama,
Tumia bunge lako kuhoji kwa nini uendeshwaji wa shirika letu la ndege wanalosema linatuletea faida lukuki ghafra tu limehamishwa na kwenda kufanya kazi chini ya ofisi ya Raisi ikulu(Ambayo haina ukaguzi) kulikuwa na ulazima gani au kuna kitu gani kinafichwa kwa walipa kodi wako ?
Tumia bunge lako kuhoji kwa nini bado kuna halmashauri zinapewa hati chafu tena zingine ni zaidi ya mara moja na hakuna kiongozi yeyote wa serikari anaewajibishwa ili kukomesha tabia hii,
Kuna Vingi vya kuhoji na wewe kama kiongozi wa bunge unatakiwa kusimamia bunge lako kuhoji chochote kinacholeta sitofahamu kwa wananchi,
Ndugai unatakiwa kutambua kwamba hapo ulipo unasimama dhidi ya wananchi na Serikari ni waajiri wako, chochote wanachofanya lazima kiwe na faida kwa wananchi Waliokuchagua kusimama badala yao na ndio maana ata bajeti na matumizi ni lazima ifike kwako wewe na bunge lako ndio wenye wajibu wa kujadili na kupitisha ni wapi pesa itumike kwa namna gani na kwa sheria/kanuni ipi?
serikari wao ni watekelezaji tu wa maamuzi yako wewe kama kiongozi wa bunge na wabunge wako kwa ujumla.
TAFAKARI.
Cc Zero IQ