Who stands with Job Ndugai?

Who stands with Job Ndugai?

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,985
Reaction score
25,195
Kwa haraka haraka nani anasimama na Job ndugai humu dhidi ya Prof, Mussa Assad?

Kama hakuna hivi Ndugai hajioni kama yuko mwenyewe dhidi ya Assad na wananchi takribani milioni 40 ukitoa wa pale magogoni(kwa mujibu wa maneno yake Ndugai ni kwamba Raisi anapatiwa wakati mgumu na assad ina maana mkuu mchukia mafisadi anapatiwa wakati mgumu na mtu anaemtafutia mafisadi ),

Ndugai anatakiwa ajue kwamba Tunachukia Ufisadi,na kama kweli tunauchukia hatuwezi kupigana vita na yule anaetutafutia mafisadi,

Ndugai unatakiwa ushukuru kwa Report ya CAG iliyopo hapo mezani kwako na kuhoji pamoja na wabunge unawaongoza dhidi ya matumizi mabaya ya fedha za wananchi waliokuchagua,

Tumia Bunge lako unaloliongoza kuhoji sasa matumizi ya zile Bilioni 16 zilizotumika kununulia sare za jeshi la polisi zimeenda wapi mbona sare hazionekani,

Tumia bunge unaloliongoza kuhoji zile bilioni 1:3 zilizotumika kwenye vikao 26 vya bodi pale ngoro ngoro kwa mwaka, kulikuwa na ulazima gani wa kufanya vikao vyote hivyo na kutumia pesa nyingi za walipa kodi ikiwa wewe jimboni kwako kuna wanafunzi wanakaa chini hawana madawati wala madarasa ya kutosha, kuna wananchi wako wanapata tabu hawana miundombinu ya maji wala access ya Umeme,

Tumia bunge unaloliongoza kuhoji zile bilioni zilizotumika kununulia mashine feki elfu 5,kati ya mashine elfu 8 zilizoitajika pale ofisini kwa Jaji Lubuva,

Tumia bunge unaloliongoza kuhoji zile bilioni 3 zilizopigwa na Pole pole pale Kwenye Chama chako kwa nini hazikupelekwa kwenye mifuko ya hifadhi za jamii zimeenda wapi hizo ni kodi za wananchi waliokuchagua,

Tumia bunge lako kuhoji kwa nini mbowe na chama chake watumie fedha ya ruzuku iliyotokana na kodi za wananchi kununulia gari la mamilioni kwa kutumia jina la mtu badala ya chama,

Tumia bunge lako kuhoji kwa nini uendeshwaji wa shirika letu la ndege wanalosema linatuletea faida lukuki ghafra tu limehamishwa na kwenda kufanya kazi chini ya ofisi ya Raisi ikulu(Ambayo haina ukaguzi) kulikuwa na ulazima gani au kuna kitu gani kinafichwa kwa walipa kodi wako ?

Tumia bunge lako kuhoji kwa nini bado kuna halmashauri zinapewa hati chafu tena zingine ni zaidi ya mara moja na hakuna kiongozi yeyote wa serikari anaewajibishwa ili kukomesha tabia hii,

Kuna Vingi vya kuhoji na wewe kama kiongozi wa bunge unatakiwa kusimamia bunge lako kuhoji chochote kinacholeta sitofahamu kwa wananchi,

Ndugai unatakiwa kutambua kwamba hapo ulipo unasimama dhidi ya wananchi na Serikari ni waajiri wako, chochote wanachofanya lazima kiwe na faida kwa wananchi Waliokuchagua kusimama badala yao na ndio maana ata bajeti na matumizi ni lazima ifike kwako wewe na bunge lako ndio wenye wajibu wa kujadili na kupitisha ni wapi pesa itumike kwa namna gani na kwa sheria/kanuni ipi?

serikari wao ni watekelezaji tu wa maamuzi yako wewe kama kiongozi wa bunge na wabunge wako kwa ujumla.

TAFAKARI.

Cc Zero IQ
 
CAG nae atambue.
1. Hayuko juu ya sheria.
2. kuwa CAG sio tiketi ya kuwadharau wengine.
3. Kuwa Prof. Siyo tiketi ya kuwadharau wengine.
4. Amewahi kumuiona CAG wa marekani anakuja kutangazia matokeo Tanzani? Lazima aheshimu taratibu za nchi. Ni hilo tu
Kwa kusema hayo sijasema kuhusu ripoti yke kwani ni safi kabisa lakini si tiketi ya kupractise niliyoyasema hapo juu.
 
C

kamdharau nani?
 
kamdharau nani?
Mtu yeyote! si nani wala nani! Wananchi tumemuajieri atuangalizie mahesabu yetu. Na hiyo kazi anaifanya vizuri sana. Mengine anayoyafanya yasiyostahili kama kwenda kuloloma huko nje ya nchi ayaache!
 
Mwana Mpumbavu ni mzigo kwa mama yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umefeli
C

CAG nae atambue.
1. Hayuko juu ya sheria.
2. kuwa CAG sio tiketi ya kuwadharau wengine.
3. Kuwa Prof. Siyo tiketi ya kuwadharau wengine.
4. Amewahi kumuiona CAG wa marekani anakuja kutangazia matokeo Tanzani? Lazima aheshimu taratibu za nchi. Ni hilo tu
Kwa kusema hayo sijasema kuhusu ripoti yke kwani ni safi kabisa lakini si tiketi ya kupractise niliyoyasema hapo juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kandugali kwanza ni kagonjwa pili ni kakorofi tatu ni kambilikimo nne ni kajeuri tano ni kanahasira kali inshu ndogo kanaweza kukugonga nyundo kichwani, sita ni kalevi kamadaraka, saba ni kazee kakujipendekeza na kujitongozesha kwa jiwe, nane ni kaimba taarabu za mipasho. sasa ni mtz gani mwenye akili timamu asiyenufaika na system anaweza kusimama na haka kagonjwa?
 
Mtu yeyote! si nani wala nani! Wananchi tumemuajieri atuangalizie mahesabu yetu. Na hiyo kazi anaifanya vizuri sana. Mengine anayoyafanya yasiyostahili kama kwenda kuloloma huko nje ya nchi ayaache!
Hee kaloloma maneno yepi hayo Mageni ambayo hajawahi kuyasema hata akiwa hapa Tz hebu yaweke hapa tuyatathmini
 
Amani ya Mola iwe juu yenu wote.

Ama kwa hakika sakata linaloendellea dhidi ya Speaker na CAG linakera na kuchukiza sana sisi wananchi tunaotamani kuiona Tanzania yenye usawa na future bora kwetu na vizazi vyetu vijavyo.

Kinachokera zaidi ni huyu mtu mmoja aitwaye Job Ndugai ambaye ameanzisha malumbano yaliyo na kiwango kikubwa cha upimbi kwa CAG huku akijinasibu kuwa wao hawako tayari kufanya kazi na CAG bali watafanya kazi na Ofisi ya wananchi(Yaani ofisi ya CAG)

Hivi huyu speaker anajidanganya kudhani kuwa sie wananchi tunapenda upumbavu wake huu anaouendeleza???

Nadhani kama kungekuwa na namna au utaratibu ambao ungeweza kufanyika wananchi tupige kura tumchague ambaye hatumtaki hakika Ndugai angepata kura zoote za wananchi wa JMT hata ya mkewe angeipata.

Hivyo wito wangu kwa huyu mheshimiwa ambaye inaonekana kuna FUSE kadhaa zimeachia mahali huko kichwani afunge domo anatukwaza Watanzania na kutusababisha tutende dhambi za kutukana kimyakimya kila dakika tunapoliona sura lake na matamko yake.

Na nyie ndugu zetu wa PRAISE TEAM jaribuni kuwa watanzania hasa ktk suala kama hili maana wote hata km mtashindwa kukiri hadharani but CAG ni Mtanzania anayetupenda watanzania kwa moyo wake wote na ndio maana anasimamia matumizi ya Jasho letu,Sasa huyu ndugu yenu mgogo inapaswa hata nyie mumkemee na kumkana kwa upumbavu huu anaouendeleza...

"Proudly, brought to u by Bachelor Sugu"
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom