WHO: Hakuna ebola Tanzania

WHO: Hakuna ebola Tanzania

Watakuja live live sasa... Kifinyo kikali sana asee. BTW nimejibu kulingana na content yako.

But Swali ni, kwa nini umefikiria hivyo mkuu? Inawezekana kweli kukawa na njama za namna hiyo? Kwanini..na vidole vielekezwe wapi haswa?
ni mawazo tu mkuu, ila naishauri serikali kuwa makini maana hawa watu ni mabingwa wa kutengeneza maovu maslahi yao yanapoguswa
 
WHO wenyewe ndio wanatakiwa watoe taarifa rasmi ya kiofisi kuthibitisha kuwa Tz hakuna ugonjwa LA Ebola, ingependeza sana kuliko hizi taarifa za kudandia dandia ambazo hazina reliable sources.
WHO wanapaswa kutoa official confirmation statement kuhusu jambo hili.
 
Kwa hiyo yule mgonjwa alofia pale temeke hospital hadi ndugu zake kuzuiliwa wasishiriki kumzika serikal ikaenda kuzika haraka haraka bila hata ndugu wa marehemu kuonyeshwa maiti yao imezikwa wapi ilikuwa ni uwoga/hofu tuu serikali.
View attachment 1212742

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) na Kitengo cha Kupambana na Magonjwa kutoka Marekani (CDC), wamethibitisha kuwa Tanzania hakuna mlipuko wa ugonjwa wa ebola. Uthibitisho huo umekuja baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuruhusu kuchukua sampuli za wagonjwa waliodhaniwa kuwa na ebola na baada ya kupima wamethibitisha kuwa Tanzania hakuna ebola.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile (pichani) jana alifanya mazungumzo na Mkurugenzi wa CDC wa Marekani, Robert Redfield aliyewasili nchini juzi kwa ajili ya kuangalia namna ya Marekani itakavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko.

Kutokana na mazungumzo baina ya pande hizo mbili jana imeelezwa kuwa hadi sasa Tanzania haina mgonjwa wa ebola. Katika taarifa yake, Redfied alisema Marekani na Tanzania zitaendelea kushirikiana na kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kupambana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kupitia Global Health Security Alisema lengo kuu la Marekeani ni kuendelea kushirikiana na nchi marafiki kulinda usalama wa afya dunia.

Mbali na Tanzania Ofisa huyo atazuru nchi za Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako kumeripotiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. Ofisa huyo amekuja nchini na kufanya mazungumzo na Dk Ndungulile, ikiwa ni siku chache baada ya serikali kutoa tamko kuwa hakuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema tetesi za kuwa ugonjwa huo upo nchini si za kweli na kwamba wagonjwa wawili ambao walihisiwa kuwa na ugonjwa huo vipimo vimeonesha kuwa hawana kitu. Ummy alisema mpaka sasa hakuna mgonjwa aliyethsibitika kuwa na ugonjwa huo na kwamba serikali inaendelea kuchukua tadhari kudhibiti ugonjwa huo.

Kauli ya Waziri Ummy ilikuja baada ya kuenea tetesi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kuwa kuna mtu mmoja amefariki dunia kwa ugonjwa huo na wawili wamewekwa karantini. Pia tetesi hizo zilichagizwa zaidi na waraka wa WHO na ule wa Umoja wa Mataifa (UN) ambao ulisema kuna tetesi za kuwa Tanzania kuna ugonjwa usiojulikana na kwamba wanachunguza tetesi hizo.

Alisema wagonjwa wawili ambao walihisiwa kuwa na ugonjwa huo mmoja kutoka Songea na mwingine Dar es Salaam, wamechukuliwa sampuli mara mbili kwa nyakati tofauti na vipimo vimeonesha hawana mambukizi ya ebola.

Tangu Agosti mwaka 2018, DRC ilivyobainika kuwa na mlipuko wa ugonjwa huo mpaka Agosti 12, mwaka huu, jumla ya wagonjwa 3,099 wamefariki dunia. Kufuatia hali hiyo serikali imechukua tadhari kwa kununua vifaa vya mkononi vya kupima joto 2,700 na mavazi kinga na kusambaza katika mikoa ya Kagera, Mwanza, Kigoma, Rukwa Katavi na Dar es Salaam. Pia, wametoa mafunzo kwa watumishi 460 na kwa upande wa ngazi ya jamii wametoa mafunzo hayo kwenye kada mbalimbali ambapo 264 ikiwemo waendesha bodaboda wamenufaika na mafunzo hayo.
 
EBOLA huwa haijifichi wala haihitaji kutangazwa kisiasa. Ikitia team mtajua tu maana mtifuano wake sio wa mchezomchezo. Ebola sio kama Kipindupindu (Cholera) mnayoweza kufichaficha na kudai ni seasonal diarrhea au acute watery diarrhea (AWD)
Tatizo wengi wana google symptoms, etiology, diagnosis hadi treatment. Ukiona taarifa ni kutoka kwa Dr.Google.
Kwa serikali wao ni siasa kila kitu, maana wao wanapiga pesa za wahisani.
 
View attachment 1212742

SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) na Kitengo cha Kupambana na Magonjwa kutoka Marekani (CDC), wamethibitisha kuwa Tanzania hakuna mlipuko wa ugonjwa wa ebola. Uthibitisho huo umekuja baada ya Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kuruhusu kuchukua sampuli za wagonjwa waliodhaniwa kuwa na ebola na baada ya kupima wamethibitisha kuwa Tanzania hakuna ebola.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile (pichani) jana alifanya mazungumzo na Mkurugenzi wa CDC wa Marekani, Robert Redfield aliyewasili nchini juzi kwa ajili ya kuangalia namna ya Marekani itakavyoweza kushirikiana na Tanzania katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko.

Kutokana na mazungumzo baina ya pande hizo mbili jana imeelezwa kuwa hadi sasa Tanzania haina mgonjwa wa ebola. Katika taarifa yake, Redfied alisema Marekani na Tanzania zitaendelea kushirikiana na kuisaidia Tanzania katika juhudi zake za kupambana na kudhibiti magonjwa ya mlipuko kupitia Global Health Security Alisema lengo kuu la Marekeani ni kuendelea kushirikiana na nchi marafiki kulinda usalama wa afya dunia.

Mbali na Tanzania Ofisa huyo atazuru nchi za Rwanda, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambako kumeripotiwa kuwa na ugonjwa wa Ebola. Ofisa huyo amekuja nchini na kufanya mazungumzo na Dk Ndungulile, ikiwa ni siku chache baada ya serikali kutoa tamko kuwa hakuna mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema tetesi za kuwa ugonjwa huo upo nchini si za kweli na kwamba wagonjwa wawili ambao walihisiwa kuwa na ugonjwa huo vipimo vimeonesha kuwa hawana kitu. Ummy alisema mpaka sasa hakuna mgonjwa aliyethsibitika kuwa na ugonjwa huo na kwamba serikali inaendelea kuchukua tadhari kudhibiti ugonjwa huo.

Kauli ya Waziri Ummy ilikuja baada ya kuenea tetesi kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, kuwa kuna mtu mmoja amefariki dunia kwa ugonjwa huo na wawili wamewekwa karantini. Pia tetesi hizo zilichagizwa zaidi na waraka wa WHO na ule wa Umoja wa Mataifa (UN) ambao ulisema kuna tetesi za kuwa Tanzania kuna ugonjwa usiojulikana na kwamba wanachunguza tetesi hizo.

Alisema wagonjwa wawili ambao walihisiwa kuwa na ugonjwa huo mmoja kutoka Songea na mwingine Dar es Salaam, wamechukuliwa sampuli mara mbili kwa nyakati tofauti na vipimo vimeonesha hawana mambukizi ya ebola.

Tangu Agosti mwaka 2018, DRC ilivyobainika kuwa na mlipuko wa ugonjwa huo mpaka Agosti 12, mwaka huu, jumla ya wagonjwa 3,099 wamefariki dunia. Kufuatia hali hiyo serikali imechukua tadhari kwa kununua vifaa vya mkononi vya kupima joto 2,700 na mavazi kinga na kusambaza katika mikoa ya Kagera, Mwanza, Kigoma, Rukwa Katavi na Dar es Salaam. Pia, wametoa mafunzo kwa watumishi 460 na kwa upande wa ngazi ya jamii wametoa mafunzo hayo kwenye kada mbalimbali ambapo 264 ikiwemo waendesha bodaboda wamenufaika na mafunzo hayo.
So far hii ndio stand ya WHO
Nyie leteni unazi kwenye Masuala ya Afya,Mumeo akipata Ebola ndio akili itakukaa sawa
IMG-20190920-WA0032.jpg
 
Statement ya WHO iko wapi?Kauli zenu haziaminiki
 
Alhamdulillah.. Mungu atunusuru nchi yetu na Gonjwa hilo hatari. Pole kwa majirani zetu, Tuwaombee waushinde ugonjwa huo.
 
Back
Top Bottom