patience96
JF-Expert Member
- Aug 19, 2011
- 1,353
- 575
Kwa kweli there is no way useme kwamba Mungu alikuwepo tu since forever.., yaani alitokea tangu milele yote.., its impossible. ngoja nikwambie kwanini.
1.) assuming Mungu ali-exist since forever, na tunaipa forever a value T. Sasa niambie at time (T-1 second) alikuwepo..??!
2.) Na at time (T-1 second) palikuwa na nani.., je ndie aliyefanya uumbaji..?! na je yeye huyo aliekuwepo at time (T-1 Second) kaumbwa na nani na katokea wapi na kwa sababu gani na kwa faida gani na ya nani..??! na ili iweje..??!
3.) Na tukisema Mungu atakuwepo up to forever, na tukaipa hiyo forever a value F, je at time (F + 1 second atakuwa wapi)..??!
jifunze kwanza mungu ni nini ili ujue namna ya kuuliza maswali sahihi!
kwa nini hajaumba mungu ??
kwa nini mungu hayupo ???
Akikujibu hili swali nishtue....
Unachanganya ujuzi wa kibinadamu wenue mipaka na huo unaodaiwa kuwa ujuzi wa mungu awezaye yote usio na mwisho.
Binadamu anaposema "kesho mvua itanyesha" ana forecast, hana uhakika wa 100%.
Huyo mungu wenu mnayedai yupo, kwa mujibu wa habari za yeye kujua yote na kuweza yote, akisema "kesho.mvua itanyesha" sio.kwamba anaforecast, hilo ni hakika kwa 100% at that point, na.kwa kuwa yeye ana.uwezo wote, ukiwamo.uwezo.wa kubadili hilo, na kwa kuwa yeye ndiye mnasema kwamba.ndiye.muongozi wa vyote (jua, mawingu, upepo etc) na hakuna unywele unaotikisika bila yeye kujua na kutaka, mungu huyu akiaema amejua kesho mvua itanyesha ni sawa na akisema amepanga kesho mvua itanyesha.
Ukisema vingine umemshusha vyeo vyake vya ujuzi wa yote na uwezo wa yote.
mungu ni infinity .na ni roho..so kamaunatumia akili umepotea
Hapana
Unachanganya mambo....
Ukijua jambo fulani litatokea kesho kwa uhakika wa 100% halafu ukawa na uwezo wa kulizuia bado utakuwa hujalipanga litokee!
Except mungu wenu anatakiwa kuwa ndiye muumba wa vyote na hakuna kinachoweza kutokea bila ruhusa yake.
Kitu kikiweza kutokea bila ruhusa yake, maana yake mungu si muweza wa yote.
Na kama kila kitu kinatokea kwa ruhusa yake, huko ndio kupanga kwenyewe.
Kuruhusu ni kupanga kwa maana gani?
Kwa maana ya kwamba, huyu mungu wenu haruhusu kama mwalimu mkuu anavyoruhusu mwanafunzi mtoro achapwe fimbo sita (ambazo mwanafunzi mtoro mjanja anaweza kuziepuka kwa kutoroka bila kushikwa, au akashikwa na kumbembeleza mwalimu asimchape kwa sababu alitoroka kuwahi hospitali kumhudumia mama yake aliyekuwa anafariki kwa ugonjwa hatari).
Kuruhusu kwa huyu mungu wenu mnavyosema ni kwa aina isiyopingika wala kurekebishika.
Kama vile kuruhusu binadamu aweze kuishi katila muda unaoenda mbele tu na usiorudishika nyuma.
Kuruhusu huku ni kupanga. Mungu kuruhusu muda uwe unakwenda mbele tu kwa binadamu ni kumpangia binadamu aishi katika ulimwengu ambao muda hauwezi kurudishika nyuma.
Ukisema mungu karuhusu tu muda uwe unaenda mbele na haurudi nyuma kwa binadamu, na hajapanga hivyo, una imply jwamba kuna kingine kilichopanga hivyo ambacho kipo juu ya uwezo wa mungu.
Jambo ambalo litavunja hoja ya kwamba mungu ni mjuzi wa yote na muweza wa yote.
Kwa sababu anavyoelezwa anajipinga mwenyewe kwa namna isiyowezekanika kuwepo.kwa nini mungu hayupo ??
Hapa unajichanganyaKwa maana ya kwamba, huyu mungu wenu haruhusu kama mwalimu mkuu anavyoruhusu mwanafunzi mtoro achapwe fimbo sita (ambazo mwanafunzi mtoro mjanja anaweza kuziepuka kwa kutoroka bila kushikwa, au akashikwa na kumbembeleza mwalimu asimchape kwa sababu alitoroka kuwahi hospitali kumhudumia mama yake aliyekuwa anafariki kwa ugonjwa hatari).
Kuruhusu kwa huyu mungu wenu mnavyosema ni kwa aina isiyopingika wala kurekebishika.
Muda unakwendaje mbele?Kama vile kuruhusu binadamu aweze kuishi katila muda unaoenda mbele tu na usiorudishika nyuma.
Hii hoja yako imejengwa kwenye assumption,kama sio nioneshe muda ....!!Kuruhusu huku ni kupanga. Mungu kuruhusu muda uwe unakwenda mbele tu kwa binadamu ni kumpangia binadamu aishi katika ulimwengu ambao muda hauwezi kurudishika nyuma.
Ukisema mungu karuhusu tu muda uwe unaenda mbele na haurudi nyuma kwa binadamu, na hajapanga hivyo, una imply jwamba kuna kingine kilichopanga hivyo ambacho kipo juu ya uwezo wa mungu.
Jambo ambalo litavunja hoja ya kwamba mungu ni mjuzi wa yote na muweza wa yote.
Kwa sababu anavyoelezwa anajipinga mwenyewe kwa namna isiyowezekanika kuwepo.
Mkisha tafuna hivyo vya namanga mnajiona kama mungu.
Kwa sababu anavyoelezwa anajipinga mwenyewe kwa namna isiyowezekanika kuwepo.
Kwani Kiranga ww unasemaje kuhusu asili ya dunia na viumbe vyake? Bana mwanzo au havina? Km vina mwanzo, huo mwanzo ni lini na nini asili yake? Km hivina, ww hapo km Kiranga na dunia yote mmetoka wapi?
isiyowezekenia ni nini ?