Nimemuunga mkono sababu ndio uhalisia tembelea vyuoni uone uchafu, angalia wataalamu wetu wengi bado wanababaika bado, nani mtaalamu aliyetoka nje kafanya jambo la maana litakalokumbukwa vizazi na vizazi lenye faida kila uchao kwa ustawi wa taifa letu,ndio maana nikatoa mfano wa madaraja mengi hapa bongo, Mimi na Bsc yangu ndogo ya banking tu baada ya kazi kwa maika 3 at least nikafungua kimicrofinance na debt solutions co. baada ya ajira kwa miaka 3, nasasa ni kiwanda kidogo kinafuata November kigamboni, istoshe hapo bado tuna application ya mtu kasoma Sussex university anataka aje pata uzoefu wa ishu za finances, alivyokuwa ulaya alikuwa ni mtu wa tungi na totoz tu, namjua vizuri sababu tulisoma ifm akasitisha mwaka wa pili akapelekwa UK na mshua wake ili apate elimu iliyo bora lakini so far bure kabisa!! sasa unajiuliza huyu badala alete nondo za ubunifu toka ulaya anakuja tafuta uzoefu wakati sisi tunataka madini yake namna ya kuboresha huduma yeye anataka aje pata uzoefu kama kutupa ushauri..loooh!!
Sisi bado tunahitaji mapinduzi makubwa kielimu,kiuchumi na kiustaarabu japo tunaelekea ila dunia inakimbia sisi tunatambaa...!
ndio maana ngono mbele, angalia kwenye maofisi rushwa ya ngono ilivyotamalaki, mwaka fulani wakati nimeajiriwa tulikuwa dodoma kwenye GM pale morena hotel hahahhaha CEO akamwambia hr huyo fulani (mfanyakazi mpya mke wa mtu - ila ilikuwa pisi kali) usimchukulie chumba bali ampe namba ya chumba chake ili apige mzigo huku mtoto wa watu hajui lolote na vile alikuwa newcomer, ilihali Mzee ana mke na watoto kibao, sisi ngono mbele watu weusi.
Hapo sijakupa kisa cha MD wa benki moja ya k'njaro aliyepita na kasoma nje huyo Mzee, mpaka benki almanusura ifirisike, tembea uone mkuu.