MKALIKENYA
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 1,196
- 486
Chintu, usichanganye mambo. Msimamo na fikira ni vitu viwili tofauti kabisa. Kama chama tunapaswa kuwa na msimamo mmoja katika mambo ya msingi, lakini hatupaswi kufanana kifikra. Narudia tena, ni ujinga wa kutisha kutaka Watu wafanane kifikra kwa sababu ni kujaribu kywafanya wasiwe binadamu!
Mkuu nadhani utakubaliana na mimi kua hiyo sera ya ukweli na uwazi ilikua katika maneno tu
na si katika matendo. Sisi tunataka sera ya ukweli na uwazi katika matendo na si katika maneno.
Mwambie ZItto akuambie yeye Ana mahusiano gani na hayo makampuni ya kutafuta Mafuta na Gesi , MWambie akuambie yeye ni nani kwa MKono ADvocate na anahusika vipi na mikataba husika , akishakuambia njoo hapa umtetee! Nasubiri ajiingize kwenye 18 zaidi. Tafakari
Nasema tena nasisitiza kwako Kitila ambae ni rafiki mkubwa sana na ZItto KAbwe , mwambie akuambie yeye Kama mshauri maelekezo ( consultant) wa MKono anamasilahi gani kuhusiana na mikataba iliyosainiwa? Alishiriki kwa kuwa go gani? Je? Alikoenda na kukutana na baadhi ya mabalozi Jana aliongea nini na wanufaika aw mafuta na gesi alipokuwa na nao? Chunguzeni hili jambo ni kubwa kuliko
sasa mbona hamfikilishi akili zenu linapokuwa suala limeanzishwa na zitto??
Watu wanamchukia Zitto bila sababu yoyote ile
M4C ni jambo la msingi na ni dira ya kukijenga chama nadhani unatakiwa umshauri ZITTO aungane na wenzie kujenga chama sababu kama kufikiri tofauti ni kuacha kukitumika chama na kwenda kuzunguka na SPIKA na kufanya mikutano ya mara kwa mara na KIKWETE basi ni bora afikiri kitofauti kwa niaba ya familia yake si CHADEMA.
KWA HIYO TUNAJADILI JINA la ZITTO ZUBERI KABWE(MBUNGE) AMA ISSUE?KWA TAARIFA YENU UKITAMKA REVIEW KWA WACHIMBA MADINI WAKIJUA UNA NGUVU FULANI WANAKUTUMIA UJUMBE WA KHERI HAPO HAPO NA UKIZIDI KUKUNJA SHINGO WATALETA AJALI,MAJAMBAZI AMA SUMU YA RUSSIA,HILO NENO REVIEW LIMEWATAJIRISHA WENGI!
Tatizo la Zitto anauota Urais hata akiwa barabarani anatembea. Tamaa ya fisi.
Moja ya matatizo yetu kama nchi na wananchi ni kuchukia watu wanaofikiri tofauti. Tumezoea mazoea; ukiona mtu anaenda tofauti na mazoea tunaanza kumpa majina kibao: kanunuliwa, msaliti, anajipendekeza, hana ushirikiano, n.k.. Lazima tubadilike na kujua kwamba binadamu tu tofauti kimwili, kiakili na kila kitu. Ili tutoke hapa tulipo lazima turuhusu akili zifikirii sawasawa na tena tuhangaike kufikiri kitofautitofauti. Kama tunataka kila mtu afikiri kama sisi ni kuendeleza utamaduni wa kutumia akili za kuazima. Zitto ni miongoni mwa watu wachache hapa nchi aliyeamua kujipambanua na kuamua kufikiri kitofautitofauti. "Kosa" lake ni kwamba ameamua kuacha kufanya mambo kwa mazoea na ameamua kuhangaika kufikiri kitofautitofauti. Zitto analaaniwa kwa kudiriki kwake kuhangaika kufikiri na kuachana na mazoea. Atabambikizwa majina yote ya ovyo kama usaliti, kujipendekeza, n.k. Tunamtia moyo aendelee kuhangaika kufikiri, wapo watakaomuelewa.
kwaio wewe kama kiongozi wa chama unakub ali kwamba zito anachukiwa ndani ya cdm...bora wewe umeongea ukweli maana kosa lake atokei kaskazini.
Naona Zitto anatafuta mbinu ya Julias Marema maana amepoteza supporters wengi kwenye chama chake
Je hii mbinu yake ya kutaka kureview hii mikataba itamsadia?
Kwanza nimpongeze kakangu Dr. Mkumbo kwa jinsi alivojaribu kufafanua juu ya alivyo zito. Mi nafikiri tusiwe na conclusive statements juu ya Zitto kisa tu eti anafikiri tofauti na sisi, hatutaenda haki kwa Ndg yetu Zitto hata kidogo. Zitto ni mwanasiasa mchanga wengi wanaomfahamu toka yuko sekondari na Chuo pale mlimani ni mtu makini anayependa kusimamia anachokiamini, na mda mwingine huwa yuko tayari hata kusimama peke yake kutetea anachokiamini na hii ndio sifa kubwa ya viongozi wengi duniani ilimradi tu anachokisimamia na kukiamini kiwe na maslahi kwa waliowengi. Tumeona hivyo kwa Mwal. kipindi cha uongozi wake kuna kipindi aliotofautiana na wenzake ndani ya chama akawambia CCM sio mama yake kwa kuwa alijua anachosimamia, vivyo hivyo mapema miaka ya mwanzoni kuna hata waliotaka kumpindua kwa kufikiri tofauti na yeye. Na kwa CDM mimi nafikiri ili chama hiki imara kiwe imara we need a diverse of views and sometimes our ideas may differ as far as we think differently. Zitto asihukumiwe kwa lolote kwa sasa, personaly bado namuona Zitto kama kiongozi shujaa, makini, visionary, mzalendo, na wa mfano kwa vijana wengi na ambae atakisaidia sana chama huko mbele. Mfano mzuri ni katika kutetea rasilimali za nchi kutonufaisha wachache. Tutafute taarifa sahihi kumhukumu kiongozi huyu sio uvumi unaletwa na wasioitakia mema CDM tutakuja kujuta baadae.Rafiki yangu Mkumbo heshima mbeeeele kama tai kwanza kwako na kwa mwenzetu Zitto Zuberi Kabwe. Ila tu nikutahadharishe mkuu; huyu Zitto umuonaye wala si yule wa wakati ule wa harakati za kweli na wala usipoteze muda wako kwani hatuwezi kumpata tena.
Hakika tumempoteza mpiganaji kwa kujichagulia kujiunga na manyang'au wa uchumi wa nchi hii kwenda kuficha Uswisi.