Where are our Dr. Chu and Co.? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Where are our Dr. Chu and Co.?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Dec 11, 2008.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 11, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Dr. Steven Chu, mwanasayansi aliyeshinda nishani ya Nobeli katika fani ya Fizikia ameteuliwa na Rais mtarajiwa wa Marekani Bw. Barack Obama kuwa waziri wa Nishati.

  Nanukuu majukumu yake na wasifu wake kama yalivyoandikwa kwenye gazeti la New York Times;

  Tukija kwenye wizara ya Fedha, aliyeteuliwa kuwa waziri wa fedha ni mchumi aliyebobea ambaye alikuwa ni Rais(Gavana) wa Benki Kuu ya Marekani-New York Bw. Tim Geithner, Ulinzi yupo aliyekuwa mkuu wa shirika la kijasusi CIA, Robert Gates, National Security yuko Generali mstaafu James Jones, Mambo ya nje yuko Hillary Clinton, bado tuje Kilimo, Elimu, Biashara, Usalama, Sheria kote huko wameteuliwa watu waliobobea katika fani hizi na hivyo kuashiria kuwa wataingia kufanya kazi kwa umahiri, wakitumia juhudi, maarifa na ujuzi walio nao katika hizi fani.

  Najiuliza je Tanzania ya 2010 tutapata kina Dr. Cho wetu?

  Nikiangalia wizara kama ya Nishati na madini, sidhani kama tumewahi kuwa na Waziri ambaye ni mtaalamu wa sekta ya Nishati au madini. Yona, Kikwete walikuwa wachumi, Msabaha ni mtu wa mambo ya Kimataifa, Karamagi ni biashara na sasa Ngeleja ni mwanasheria.

  Ni lini wizara nyeti kama hii ya Nishati na Madini ikapata mtu bingwa kama Dr. Cho? Bingwa ambaye ataweza kututatulia tatizo sugu la umeme na kusambaa kwa umeme nchi nzima, atakayelipigania taifa lake kulinda madini yetu, atakayesimama kidete kuhakikisha kuwa Tanzania inaelekea kwenye mwendo wa kutumia nishati safi kwa uzalishaji mali na matumizi ya nyumbani, atakayehakikisha kuwa mafuta yetu na hata ile gesi ya Songosongo na makaa ya mawe Kiwira yanalizindua taifa letu kiuchumi?

  Hata nikija kwenye suala la wizara ya fedha, mipango na uchumi, ni lini tutarusi kwenye zile enzi za kuwa na Waziri mwelewa mwenye utaalamu wa Uchumi, Fedha, Uhasibu na Mipango na si kuwekewa vilaza kama Mramba na Mkullo ambao si kwamba hawakuonekana hawajui kitu, bali wana kaharufu ka uzembe, kukosa uwajibikaji na kuvunda kama vile ufisadi?

  Tatizo liko wapi? ni ile sheria au kifungu cha katiba kinachosema Waziri lazima awe mbunge? Mbona Mwandosya ni mwanasayansi bingwa hatukumpeleka Nishati na Madini?

  Je Kilimo, Mifugo na Utalii tumewapeleka kina nani?

  Je kama tatizo si Katiba kwa maana ya kuwa makatibu wakuu wa wizara hizi watakuwa ni wataalamu au watu bingwa wa fani, je ni tunaweza kukiri kuwa ni sera za chama au ilani ya chama ndiyo mbaya maana inashurtisha mgombea wa uraisi na mizengwe ya ndani ya chama kuwa na Serikali ya kishkaji iliyo na sera za kishkaji?

  Au tatizo ni sisi wananchi kuwa hatujitumi katika fani zetu bila kutegemea kuona tuna Waziri bingwa au wanasiasa bingwa? Je kuna uwezekano wa Mkinga kulima chai kwa ziada bila kusubiri Waziri wa Kilimo awe ni Phd. wa mavi ya kuku na samadi?

  Na elimu kwani jukumu la kumwelimisha mtoto ni shurti tuwe na Prof. Mmari au hata gwiji mwenzetu humu Mwalimu Augustine Moshi kama waziri wa Elimu ndipo watoto wetu waelimike?

  Je ni lini tutaachana na mazoea ya kutoa Uwaziri eti kuleta mgawanyiko wa majimbo, jinsia, makabila na dini na si kutumia uzoefu wa mtu katika nyanja kama Dr. Anna Tibaijuka?

  Where are our freakin Dr. Cho and others?
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mchungaji hoja nzito hii!!

  Kwa sasa niguse tu hiki!!

  Wanasema kunakuelimka Ki_Akili na Kuelimika Ki_UTU...

  Leo Tanzania tunahitaji Kipi kati ya hivyo? Vyote au kimoja chaweza kutusukuma? Kama ni Madarasa ya Kiakikili mbona ... Vipanga wako tele?

  Nafikiri Dr Chu anavyote!! Kiakili na kiutu!

  Ngoja tuone...!
   
 3. M

  Mpanda Merikebu Senior Member

  #3
  Dec 11, 2008
  Joined: Dec 27, 2007
  Messages: 170
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mchungaji,
  Punguza spidi na munkari...umesahau hii ni bongo? Profesa bingwa wa upasuaji mifupa alikuwa ni waziri wa ulinzi hivi karibuni tu!

  Baada ya kijembe changu hicho cha kuikejeli serikali yetu na jinsi inavyofanya mambo yake, nafikiri tatizo tulilonalo si wasomi. Tatizo ni kuendekeza siasa hususan pale isipostahili. Mfano mzuri wa wenzetu wa unyamwezini ni pale rais anavyoweza kumteua mtu mwenye itikadi kama yake, itikadi iliyotofauti na ya kwake, na yule asiyefungamana na upande wowote. Wote hawa wana nia moja, kutumikia kwa utiifu wapiga kura na walipa kodi wa Marekani.

  Kwetu hali ni tofauti kidogo; kama wewe si wa itikadi yangu hupati kitu, au labda uhame chama (ahem, Mh. Lamwai upo?) Pia, watu wengi wanaogombea nafasi za siasa ili kujinufaisha wenyewe, kunufaisha marafiki wao (wafanyabiashara), wengine kwa ajili ya heshima, wengine mazoea baada ya kuwa wabunge kwa zaidi ya miaka 25, na wengine kwa ajili ya wananchi. Wakishapata uwaziri, ni kujipitisha kwa aliyewateua ili waendelee kuwa madarakani. Obama alisema hatarajii mikutano yake itakuwa mteremko yote; atabishana na watu ambao watampa uchambuzi wa kitaaluma na fani zao. Hivi kweli mwanasheria Chenge (tena nasikia ni msomi wa Harvard) anaweza kumd*#@ia Mkapa na kumwambia kuwa kutumia Ikulu kama ofisi ya biashara zako binafsi au kujiuzia shirika la umma ni kinyume na sheria? Ni heri mara mia kuwaacha wasomi (Profs. Mwandosya, Mmari, Shayo (RIP), etc) wabakie kwenye taaluma na kufundisha wengi. Nafikiri watapata faraja kuona watu wengi wanafaidika na elimu yao, badala ya kuwashauri akina haambiliki na akina hashauriki!

  Japo si upendi ukweli huu, Nyani Ngabu alisema (na ninaukubali usemi huu) "Waafrika ndivyo tulivyo".
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Dec 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Mpanda Merikebu,

  Inabidi tujiulize hata ndani ya vyama nini na lengo la sisi kujiunga na hivyo vyama!

  Hatuwezi kuendelea na siasa kichaa za kuwa na watu katika nafasi za kiutendaji na uongozi watu wasio na uwezo ama wa kiutaalamu au uwezo wa kuwa makini na fanisi.

  Leo ukinichukua mimi unipe wizara ya afya, sana sana nitanunua bendeji nyingi, lakini naweza nisijue kingine cha msingi na zaidi maana si fani yangu!

  Hivi mfano mama Anna Abdallah alipokuwa waziri wa afya au hata Zakhia Meghji walikuwa na wasifu gani kuongoza hiyo wizara?

  Hata pale Anna Abdallah alipokuwa waziri wa ujenzi na mawasiliano?

  Ni lini tutaachana na hii "kawadia bi mazoea" na kuanza kuwa na watu walio mahiri katika fani?

  Zaidi ni lini tutaachana na kanuni butu ndani ya katiba yetu inayolazimisha mawaziri wawe ni wabunge?
   
 5. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #5
  Dec 13, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Hata waziri wa nyumba mteule wa Obama ni mtaalamu wa mambo ya nyumba! Ni msanifu, sisi ndiyo kwanza tumemuweka Magufuli baada ya kina Siwale, Cheo, Lowassa...
   
Loading...