Nakubaliana na wewe katika mengi uliyoandika ukifuatilia post zangu tweeter na facebook utagundua yote unayoongelea ndio huwa nayapigania mara kwa mara na kuyaongelea na hiyo ndio imani yangu na msimamo wangu, wa kuleta mapinduzi ya mfumo mzima katika nchi yote na kudailisha mwelekeo wa taifa letu. chochote kinawezekana kwa wenye dhamira. Ufunguo wa nchi yetu uko mikononi mwetu, tuufungue mlango au tuuache ukiwa umefungwa katika jamii ya kibinafsi na yenye ufisadi. Kama taifa tunauwezo wa kusonga mbele na kufanikiwa, Kitu cha msingi ni umoja wetu na utayari wetu kujitolea kwa taifa letu.
Shayu,
Nimefurahi kugundua kuwa hata Fbook na Tweeter unatumia ID hii, nitajaribu kupata nafasi na kusoma machapisho yako huko!
Nafikiri Pia nimeweza kuupata IMANI NA MSIMAMO WAKO! Sasa tusaidane, Ni kweli kuwa Hali ya uadilifu, Uzalendo wa jamii na Taifa vimeshuka. Nilikuuliza ... Kuwa .. Tufanyeje ili kuvirejesha au Kuvijenga ili lengo la mapinduzi yafikiwe?
Mimi nasubiri aina fulani ya Maumivu yaikumbe jamii yetu ... Nikitegemea kuwa hiyo ndio njia pekee ya kuiamsha... Yes, some kind of a wake up call ?
Wewe unafikiri kuna njia nyingine ya kutegemea Kulileta Taifa kwenye umoja unaofikiri!!