Jamaa Mmoja Aliondoka Asubuhi Kwenda Kazini Ilipofika Mchana Akampigia Simu Mke Wake:
Jamaa: Halooo! Mke Wangu Vipi?
Mke: Safi.
Jamaa: Uko Wapi?
Mke: Si Niko Nyumbani.
Jamaa: Kama Kweli Uko Nyumbani Washa Blender Nisikie.
Mke: <akawasha> Si Umesikia?
Jamaa: Sawa! Nitakuja Baadae.
" Siku Ya Pili Hivyo hivyo Akapiga Simu"
Jamaa: Haloo! Za Saa Hizi?
Mke: Salama.
Jamaa: Uko Wapi?
Mke: Kama Ulivyotuacha Asubuhi Nyumbani.
Jamaa: Kama Ni Kweli Uko Nyumbani Washa Blender Niamini?
Mke: < Akawasha> Si Umesikia?
Jamaa: Yaaah Nitakuja Baada Ya Masaa 2.
" Akafanya Ivyo Kama Siku Sita Lakini Kuna Siku Akaja Bila Kumtaarifu Alipofika Nyumbani Akamkuta Dada Wa Kazi Yuko Peke Yake Akamuuliza:
Jamaa: Vipi Mama Yako Yuko Wapi?
Dada: Sijui Mana Katoka Na Blender Tangu Asubuhi