GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu
itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa,
ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enhee...
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari
nitaswaga zizi zima la ng'ombe napeleka
kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia
Range Rover Sport na mama mkwe ntampa
Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesome...
BOY: Halafu mdogo wako wa kiume ntampa
Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo
sijaanza kula....
GIRL: Enhee...na sisi??
BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima
Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli
zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu,
itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon
Bahamas....halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ya electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheart..halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji
nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo!