Mimi nilishaacha kutumia WhatsApp kutokana na hizi features mpya wanazoongeza. WhatsApp ilikuwa ni mtandao mzuri kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki: walipoleta "Status" mtandao ukabadilika kwenye Status za watu unakuta videos, picha ambazo huhitaji kuziona maana lengo kuu la mtandao ilikuwa ni kutumiana jumbe, picha na video baina ya mtu na mtu.
Wakaja kuharibu zaidi kwa kuweka "Channels" ambazo ukiingia tu unakuta suggestions kibao ambazo huzihitaji maana tayari kila kitu kwenye Channels kipo kwenye Social Work zao: Instagram, Facebook.
Meta pia wameharibu mitandao ya Facebook na Instagram kwa kuweka "Reels" na "Suggestion Posts" unaingia mtandaoni badala uone posts za watu uliowa-follow unakutana na mavitu ya ajabuajabu tu.
Facebook ilikuwa mtandao wa kuungasha ndugu na marafiki. Instagram ilikuwa mtandao wa kuweka picha na matukio ila sasa hivi imekuwa kama uwanja wa picha za utupu na video TikTok.
Meta wajitafakari, hizi updates zinaharibu maana ya mitandao ilivyoanzishwa.