Whatsaap facebook kuunganishwa

Whatsaap facebook kuunganishwa

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,464
MABADILIKO kwenye mtandao maarufu wa simu, WhatsApp, yataanza rasmi leo wakati kipindi cha siku 30 cha kukubali masharti mapya kitakapomalizika.

Mabadiliko hayo yanawataka watumiaji kusambaza taarifa zao kutoka Whatsapp hadi Facebook, mtandao ulioinunua Whatsapp kwa S. trilioni 22 mwaka 2014.

Hata hivyo, unapokubali masharti hayo haimaanishi kuwa Facebook itadukua taarifa za mtumiaji kutoka Whatsapp kwa vile kwa siku 30, ana hiari ya kuchagua kusambaza au kutosambaza taarifa zake kwa Facebook.

Watakaokataa kusambaza taarifa zao, wataendelea kutumia Facebook kama kawaida ila watakaokubali, kufikia leo hawataweza tena kuubatilisha uamuzi huo.

Facebook ilisema Ijumaa kuwa hii ni mara ya kwanza kwao kufanya mabadiliko makubwa kwa Whatsapp tangu ianze kuimiliki.

“Hili ni jambo la kawaida kwa kampuni zilizonunuliwa lakini tunajitahidi kuwapa watumiaji hiari ya kuchagua iwapo Facebook itatumia taarifa zao za Whatsapp kuwaletea matangazo na bidhaa zinazolingana na matakwa yao,” Facebook ilisema.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa mitandao hiyo miwili itazidi kushirikiana ili kuboresha huduma zao mbalimbali.

Baadhi ya watumiaji wanahofia kuwa kukubali kusambaza taarifa zao kutaifanya Facebook kudukua undani wao huku wengine wakikubali bila wasiwasi.

Hata hivyo, wataalamu wanaamini hakuna haja ya kuhofia kwani Whatsapp ina mbinu maalumu ya kukinga ujumbe kutosomwa na yeyote asiyekusudiwa yaani ‘encryption’.

Facebook ina zaidi ya watumiaji bilioni moja kote duniani.
 
encryption wakati wenyewe wale wakiamua tu decrypt, tena wanakwmabia kabisa hiyo encryption WHEN POSSIBLE, ina maana kuna nafasi ya mawasiliano kuingiliwa. Ingia setting kwenye account kisha security alafu soma vizuri utaona wanaanza kwa kusema when possible...

Angalia udukuaji ulipofikia
Tesla updates software after car hack - BBC News
 
MABADILIKO kwenye mtandao maarufu wa simu, WhatsApp, yataanza rasmi leo wakati kipindi cha siku 30 cha kukubali masharti mapya kitakapomalizika.

Hata hivyo, wataalamu wanaamini hakuna haja ya kuhofia kwani Whatsapp ina mbinu maalumu ya kukinga ujumbe kutosomwa na yeyote asiyekusudiwa yaani ‘encryption’.

Ikiwa encryption ni end to end au tuseme sender to recipient, ni muhimu sana tujiulize swali kuhusu hizi adverts/ matangazo yanayozungumziwa...
 
Sasa kwa watanzania hii ina madhara gani maana nadhani wanachoongelea sio picha za uchi au sexting messages wanazotumiana watu ila wanaangalia trend ya mtumiaji kwa ajili ya advertisements/marketing, hii ni common kwa nchi za huko
Cjui labda nieleweshwe.
 
Back
Top Bottom