What's Up Abroad

Buswelu

JF-Expert Member
Aug 16, 2007
1,998
354
Hellow Wana board

Kuna kitu huwa kina nikeleketa sana...hapa watu tunachangia sana mijadala kuhusu nchi yetu na mstakabali wa nchi yetu.

Nije kwenye swala...vijana wengi wa kitanzania wako nje ya nchi all over the word wakihangaika na maisha kupata malisho mabichi.
Lakini ni nini wanaifanyia nchi yao na wao wenyewe kwa ujumla hapa nazungumza kama kuwakeza...nchini kwao!,Kujenga nchini kwao..yaani hapa wewe kujenga kwenu kibanda cha kuishi hata ukija kutembea tanzania unajivunia kuwa kwao abroad una kitu kwenu.

Sina hakika ni wapi niliona wapi hoja hii lakini ilijibiwa kwa hasira na jazba za vijana wengi walio nje kuwa hawaweza wekeza tanzania walitoa sababu nyingi sana....ingawa hizi hazibadilishi ukweli kuwa one day ukija tanzania hata kama umekusanya dola 3000kuja ku spend its nothing kama huna cha maana ulichofanya hapa tanzania.

Tuchulie mfano kwa sasa imekuwa ni fasheni tanzania mta akimaliza degree yake akipata kazi tu inayolipa fresh lazima ajenga nyumba...na sio makazi.Anunue gari na sio usafili.

Hii yote ni dalili nzuri ya kupevuka kwa vijana sasa walioko Nje ya nchi mnakwenda then mnarudi tanzania back to square one yaani abroad inakuwa kama mlikwenda kujifunza kiingereza.Na pesa huna kiingereza unajua...ila unashi kwa wazazi mambo yanavyoendelea nchini hujui watu wanapataje kazi.Achilia mbali shida zetu.

Jamani umuhimu wa kuwa abroad ni nini?Achilia few ambao wamefanikiwa wakiwa uko uko na wameamua kutokuja tanzania kabisa kwa kuwa itakuwa ni aibu.

Tufikili kuhusu hili na tujiulize nini maana ya kuwa Abroad?

Regards
Buswelu.
 
Back
Top Bottom