What's the story: Ulipataje kazi unayofanya au uliyowahi kufanya?

Kwenye Ishu ya ajira kila mtu na Bahati yake na Mungu wake..Ila MaHR wawe waaminifu mbele zao na mbele za Mungu..Unaimwita mtu kutoka mkoani tayari kumbe unamtu wako wa hiyo nafasi kwanini umsumbue aingie gharama zisizokuwa za lazima..si bora uachane naye kwenye interview au usitangaze hiyo nafasi.
HR unatangaza nafasi ya kazi tayari kuna watu wako wako kwenye ajira hii naikumbuka nilikuwa nikifanya kazi taasisi fulani ya fedha..nafasi zikatangazwa mwezi 5 kwenye gazeti huku watu walikwisha ingizwa kwenye ajira toka mwezi 3. vijana wakaomba nafasi za kazi hakuna hata mmoja aliyeitwa kwenye interview maana HR alikwisha jaza watu wake na hawakuwa na interview.
 
Hahaa niko passion na rural issues tu.Aise mimi sio mdau wa kusafisha rungu naamua kuacha maana wenyeji walinitisha appetite ikakata
Ahahahahah majamaa walikupa warning mapema.........na mademu Wa bush kwa kubabaikia wageni hasa walotoka town.....bila mkwara wake zao na mademu zao wangekuwa hatarini. BTW hvi huko rushwa,ruhita, ngenge,kishuro n.k, kuna Mizigo kweli???
 
Nilitumiwa message na recruitment agency kupitia linked in, nikafanya interview ya kwanza kwao, ya pili nikafanya kwa client wao na namshukuru niliipata ingawa baadae nilikuja kuacha kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu.
Siku ya interview ya pili mwishoni niliambiwa " of all the candidates we have interviewed, you have shown a great character and being very honest Thank you...! Hii statement ilinifanya nihisi nimekosa kazi ila mungu si athumani niliipata japo haikuwa riziki.
 
Siku ukimsaliti ndo utakuwa mwisho wa hiyo kazi. Pole, nakupa pole kwasababu maisha yako yote utakuwa mtumwa wa ndoa yako
 
Mkuu kwan kwa sasa hauwezi nisaidia angalau nipate pa kutulizia akili huko maana nimemalza chuo cna pa kushika samahan lakini
 
Very interested with this. Thank u mkuu
 
Reactions: vvm
Kazi ninayoifanya sasa ni kazi ya tatu.
Ni kazi ambayo niliipata kupitia rafiki mfanyakazi mwenzangu ambaye tulikuwa tunafanya naye kazi kwenye kazi yangu ya 2.Alinipigia simu akaniambia kuna sehemu wanataka mtu peleka cv basi baada nikaenda Mungu akajalia.
-Kazi yangu ya pili niliipata humu Jamiiforum nilijitambulisha mimi ni nani,sifa zangu na nini naweza fanya basi Mungu akajalia 1person akanipick soon.sitasahau nilipata kazi sehemu nzuri kupitia JF.That why I respect jf mpaka kesho,coz sikutarajia kwa %kubwa kwamba kupitia jf ningeweza kupata kazi.
-Kazi ya kwanza niliipata kupitia class met wangu wa chuo.alikuwa anafanya kazi sehemu akaulizwa kama kuna mtu anamfahamu anayeweza fanya kazi fulani basi akanipoint tu nikapeleka cv Mungu akajalia.

:Nilichojifunza
Yeyote unayekutana nae maishani,sehemu yeyote ile anaweza kuwa sababu ya wewe kupiga hatua na kufikia ndoto zako.Mungu atusaidie kuweze kuhusiana na watu vizuri.Hata kwenye hii mitandao ya kijamii ambayo hatujuani,trust me unaweza kula bingo la kiuhalali kabisa kama mimi nilivyopata kazi.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…