What you see is real? Education is Power

What you see is real? Education is Power

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,970
Utangulizi

Kwanza kabisa ninawasalimia wote kwa pamoja.

Pili nimekosa kichwa cha habari kinachoendana na nilichoandika hapo juu kwa lugha ya kiswahili.

Bila kupoteza muda mrefu sana, ninaendelea na maelezo mbalimbali kwaajili ya kujuzana uhalisia wa mambo. Tunaishi katika mazingira na haya mazingira yanatufanya tuweze kufanya kazi na zaidi ya yote tuweze kuishi. Lakini sisi wanadamu tumeshindwa kuelewa sisi ni akina nani na haya mazingira ni nini hasa uhalisia wake. Kutokana na elimu tuliyoipata kutoka kwa waliotutangulia tumejikuta tumebaki pale pale tu na zaidi sana kutokutimiza lengo lilotuweka hapa duniani.

Mazingira yamezidi kuwa hatarishi siku baada ya siku na kufanya maisha yetu kuwa magumu sana sana. Sisi wenyewe ndio tumefanya mazingira kuwa magumu na kuonekena kana kwamba tupo hapa duniani kuishi kwa shida. Umimi na uoga ndio chanzo kikubwa sana cha kuharibu mazingira yetu.

Lengo langu hapa ni kwamba; Je kitu unachokiona ndio uhalisia? Je tofauti ya wewe ukiwa kwenye ndoto na ukiwa haupo kwenye ndoto ni nini? Ni maswali rahisi sana kuyajibu kwa mkato, lakini ukifikiria zaidi sana utakuja kugundua kuwa "What you see is illusion".

Sayansi inavyosema
Kwa wale waliosoma sayansi aghalabu darasa la saba; tutakubaliana kila unachoona ni taswira ya kitu halisi. Mwanga unapoingia kwenye macho unapigapicha vitu vinavyotuzunguka na kuvipitisha kwenye ubongo kwaajiri ya kutafsiriwa. Kwa hiyo kile unachokipata kwenye macho ni taswira ya kitu halisi. Sasa kama ni taswira je kitu halisi kikoje sasa? Je unapoona ule ni mti kweli ni mti? au ni taswira ya mti!!?

Kitu kingine tena utashangaa jinsi sayansi inavyozidi kufunua mambo. Mwili wa binadamu umetengenezwa na Multi-Systems (Mfano: Reproduction System, Digestion System etc). Utakuja kushangaa kuwa hizo system zimeundwa na Organs mbalimbali na hizo organ zimeundwa na Tissue na ukienda zaidi hizo Tissue zimeundwa na Cells na utakuta baada ya Cell utapata DNA na RNA. Kwa hiyo DNA tunaweza kusema kwenye Chemistry ni Compound ambayo ndani yake kuna molecules na kwenye molecule kuna Atoms

Hebu twende zaidi tuone je hiyo Atom imetengenezwa na nini? Utashangaa utakuta ni Protons na Electrons. Dah!! sasa hapa ni nin? Je hizo Protons na Electrons zimetokana na nini? Utakuja kugundua ni Particle ambazo zinaelezwa kwenye Quantum Physics. Na ukienda zaidi sana utakuta frequency na ukiendelea utakutana na Void.

HITIMISHO
Sasa hapa je huo mwili wa mtu umetokana na nini? Utakuja kugundua kumbe ni illusion tu. In Short what you see is not real.

Mtu ni consciousness(Soul/Spirit) zaidi ya hayo ni illusion. Akili huwa zinajaribu kutengeneza vitu ili kuweka twaswira ili kuendana na mazingira yaliyopo. Pale sisi watu tutakapogundua kwa pamoja kuwa we are not body; Tutafanya tuishi kwa furaha. Dini na imani mbali mbali ndio vinavyofanya sisi tusijielewe sisi ni nani. Zinaleta ubaguzi na umimi. Hatima ya dunia hii ipo mikonoi mwetu, tukigundua tu sisi ni nani.

EDUCATION IS POWER
 
Back
Top Bottom