What we learnt from Arumeru by election | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What we learnt from Arumeru by election

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Bongolander, Apr 1, 2012.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wakuu naomba tuangalie issue hii kwa mapana, tusiangalie kwa mtizamo wa mvutano kati ya CCM na CDM, kwani tunaona kuwa nchi yetu imefika hatua ambayo naweza kusema tunaonekana kuchangamka kisiasa.

  Nakumbuka by election ya kwanza kabisa ilifanyika hapa Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 90 (may be 92), enzi hizo Horace Kolimba akiwa katibu Mkuu wa CCM. Kulikuwa na kina Komba na waiambaji wengi wakiwakejeli wapinzani na wapinzani wenyewe hawakuwa organised hata kidogo. CCM ilishinda kiulaini sana, kama nakumbuka vizuri kulikuwa na by election Mbozi, Igunga na jimbo lingine sikumbuki ni lipi. Uchaguzi wa wagombea ulikuwa very smooth, na ndani ya CCM kulikuwa shwari kiasi.

  CCM haikuhitaji kutumia nguvu sana kushinda, haikuwa na haja hata ya kufikiri kuchakachua, hakukuwa na haja ya rais mstaafu, waziri mkuu mstaafu, kamanda mkuu wa polisi, katibu mkuu wa chama, mkuu wa mkoa au hata maofisa wa juu wa usalama wa taifa na mkoa kwenda majimboni kuhakikisha kuwa CCM inashinda. CCM ilikuwa inashinda by default, na wengi kwa wakati huo tulikuwa tunaona kuwa wapinzani wote ni makapi ya CCM na waganga njaa. Imani hii iliongezeka pale mwenyekiti wa TPP Alec Che Mponda, alipotangaza kuwa chama chake kimeshinda by election kwa kupata nafasi ya pili, kwani alisema haitawezekana kamwe kuishinda CCM. Kuna siku pia aliitisha maandamano yasiyo na maana, na kutufanya tuwaone kuwa wapinzani ni waganga njaa. Watanzania wengi tukaona kuwa wapinzani ni kundi la wahuni tu.

  Matumizi ya vyombo vya dolam hayakuwa makubwa, idara ya usalama ngazi ya wilaya na polisi ngazi ya mkoa na wilaya waliweza kushughulikia maswala ya uchaguzi na uchaguzi ulikuwa unaisha kwa amani kabisa.

  Hakukuwa na lugha za matusi, hasa kutoka kwa CCM, wapinzani ndio walikuwa wanatoa matusi, hadi kuna wakati Horace Kolimba akawa anasema wanakashifu chama.

  Ni miaka 20 imepita sasa, hali inaonekana kuwa tofauti sana. Uchaguzi wa Arumeru umeonesha picha tofauti kabisa. Sina haja ya kutaja ni vigogo gani wamekwenda huko, wengi tu wa chama, serikali, polisi na idara ya usalama. Idadi kubwa ya wana usalama kuliko idadi ile ya waliokwenda Zanzibar, sina haja ya kutaja matusi yaliyoporomoshwa kule, sina haja ya kutaja rushwa waziwazi iliyoetembea kule. Walipo Arusha wanaweza kusema mengi zaidi yaliyotokea huko.
  Sasa hivi ni wazi kuwa ndani ya CCM kuna makundi mawili, CCM-Asili na CCM-Mtandao, tumeona jinsi walivyotumia mbinu za ajabu kupitisha mgombea. Kundi moja lilitoa rushwa na ikatangazwa wazi, na kundi lingine(lile linalopinga ufisadi) likakaa kimya. Even worse wapinzani nao wamekaa kimya as if ni halali. Tume yetu ya uchaguzi imeendelea kuwa ya kutia mashaka, tumesikia kuwa masanduku ya kura yamekamtwa yakiwa yamejaa kura zilizopigwa na iko kimya tu.

  Inaonekana sasa kuwa wapinzani, are not as hopeless as we saw them in 1992, CCM will not win by default as was in 90's, sasa inabidi itumie nguvu zote ilizonazo kushinda uchaguzi. Mtaji wa CCM kushinda uchaguzi kiurahisi kama ilivyokuwa igunga, mbozi na kwingineko ambao Profesa Baregu alisema ni unyonge wa kiuchumi na kielimu walionao wapiga kura katika maeneo husika,a huenda una ukomo. Na matumzi ya vyombo vya dola kwenye uchaguzi inaonekana ni makubwa na makini zaidi kuliko katika kupambana na uhalifu unaotuliza kila siku, hii si dalili nzuri kwa watu tuliozoea kupiga kura tukisimamiwa na mgambo wenye marungu. Tumetoka mbali lakini tunakwenda mbali zaidi.

  Hatua iliyofikia CCM sasa ya kutumia nguvu kubwa kushinda by election kwa lolote lile inatia shaka. Hali hii ikisambaa nchi nzima kuna uwezekano kukawa na hali ya ajabu nchini kwetu.
   
 2. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Bongolander, heshima mbele mkuu! Long time...
  Kwa hakika walio madarakani wana underestimate mambo yafuatayo, licha ya uliyoeleza:

  1. Kwamba kiu ya demokrasia inakua siku hadi siku
  2. Kwamba mabadiliko yoyote yale huwa hayazuiliki, sana sana yanaweza tu kucheleweshwa
  3. Uelewa wa wananchi juu ya hayo hapo juu umepanuka sana, na hata baadhi ya vyombo ulivyovitaja vinachoshwa na hali hii
  4. Mifano hai kaskazini mwa bara letu ipo, na inaonyesha namna ambavyo kiu na uvumilivu wa wenye nchi ikifika kikomo inavyoweza kushindwa kuzuilika.
  5. Pamoja na hayo nilioeleza, bado hakuna upinzani wa dhati unaoweza kusimamia mageuzi bila kudhoofu. Kuna changamoto nyingi zinazoonekana kurithiwa na baadhi yetu kwenye vyama vyetu. Pengine angalizo la Prof wangu Baregu ni halisi, unapoona nguvu ya fedha ikitawala pande zote...tawala na pinzani.
   
 3. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu you are right, mpaka sasa bado hatujaona upinzani ule tunaotaka wa kuweza kuing'oa CCM madarakani au kutoa challenge makini walau kufikia nusu ya wabunge bungeni au zaidi ya wabunge wa CCM. Unajua mpaka sasa bado CCM kupitia vyombo vya dola imekuwa ikijipenyeza kwenye vyama vya siasa vya upinzani na kuviyumbisha. Kwa hiyo CCM bado haina uwezo wa dhati wa kuongoza na kuendeleza nchi, lakini imepenyeza kwenye upinzani ili kupunguza upinzani wa kweli. Tunasonga mbele lakini. Kama kweli Chadema wameshinda, ni aibu kubwa sana kwa CCM, hasa ukizingatia nguvu na pesa waliyotumia.
   
 4. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Matokeo haya yanatoa fundisho kwamba haiwezekani kuwalazimisha watu wamchague nani. Zaidi, inaonyesha CCM hawakuthamini analysis ya pre-election au haikufanyika kabisa. Nakumbuka jinsi walivyobishana NEC juu ya udhaifu ulioonyeshwa kwenye suala la mgombea wao, na bado wakaamua kumrejesha yule yule.

  Au la, Mwenyekiti, kwa udhaifu wa kushindwa kukidhibiti chama na hasa powerful figures, kaamua kwa makusudi kuwaonyesha kwa vitendo kuwa wakitumia nguvu kuliko akili basi matokeo ndo yanakuwa hayo...kwamba yeye anaona he has nothing to loose?
   
Loading...