Mkuu, allow me to confess what you have just advised here is an uphill task to me. But I gonna start putting it into action. Its true I am perfectionist (that's my weakness), I catch my breath when a person does what I consider wrong or less than what I expect of them. I need to get rid of this mindset and behavior.
I am always a fair person and open minded. Nakubali kukosolewa na pia nakubali kubadilika. I am determined to change and learn how to better understand her to make her tick better, but what I wish for is kama angekuepo mtu ama mwanamke ambaye angeweza kumfungua na mwenzangu nae akubali kubadilika na kujaribu kwa nguvu zote kunielewa. then tukutane somewhere katikati safari ianzie hapo kwa hatua mpya.
Akibaki kama alivyo na misimamo yake ikibaki kama ilivyo, nahisi itaniwia ngumu zaidi kuwa na mwanzo mpya kama nilivyosema hapa mwanzo wa hii post. Ni mtizamo tu naweza kushauriwa zaidi katika hili ninalolihisi.
Tatizo kubwa lipo kwako ndugu, kila saa kukosoa tu kila saa kulalamika, kila saa kulaumu na kuona mabaya tu ya mwenza wako unayotaka abadilike (awe perfect).... Hii kitu kwenye mahusiano au hata kwenye maisha ya kawaida tu ni SUMU mbaya sana.
Huna shida nyingine yeyote ile. Acha kuwa Mr perfect, mshukuru na mfurahie mkeo kwa vile alivyo sasa, vile ambavyo amekua mke mwema kwako, vile amewalea vyema wanao, vile ambavyo amakuwa mwaminifu kwako (seven years hakuna tuhuma za kucheat sio mchezo kwa kizai cha leo) na mengine meengi anayokufanyia mazuri itamsaidia kuboreka zaidi.. Maandiko yanasema ''Mithali 17:22 MOYO ULICHANGAMKA NI DAWA NZURI, BALI ROHO ILIOPONDEKA HUIKAUSHA MIFUPA '' (Asignment yako iko hapa kuuchangamsha moyo wake)
Kama kila wakati ni kukosoa kwa kujidai unautetea ukweli, kumlaumu kwa vitu vidogo kama unavyosema unakosea sana kaka kwa maana UNAIPONDA ROHO WAKE bila kujua. Na roho ikishapondeka ndio inakua imejaa uchungu, hasira, chuki, ghadhabu, visasi, woga/wasiwasi na kukata tamaa. Wanawake wapo sensitive sana na comments tunazowapa na kama kila saa ni kusikia habari mbaya tu utampoteza kabisa siku za usoni kwa depression n.k kaka yangu
Learn to appreciate her, compliment her, mfurahie kwa mapungufu aliyo nayo (si ilimpenda kiwa hivyo toka mwanzo), acha kabisa kumkosoa bali katika kila jambo zungumzeni kwa nini liko hivyo na mnawezaje kusaidiana kuuondoa au kucover huo upungufu. Ukilenga kumkosoa mwanamke unatakiwa utumie akili na busara sana kiasi kwamba utamfanya akuelewe na mnaishia kucheka baadae. Kumuambia tu acha kitu fulani kama mtoto sio sawa, bali mnazungumza na kubembelezana kwa upendo.
Kumbuka ukiwa na nafsi ya kukosoa kosoa sana ni NADRA sana itatokea uweze kuona mazuri ya mtu. Jitahidi kwenye hilo.
Tumeambia tutumie akili sana kuishi na wanawake, usimchukulie kama mtu yeyote tu yule au kama unavyowakomalia watu walio chini yako ofisini au kwenye kazi yako ukaona wanawake nao wako hivyo.
THE ONLY ONE WITH A PROBLEM AND YOU CAN TO CHANGE IS YOURSELF MR jaxonwaziri. No one else. We can only influence the changes, we can not change people. See how to improve your infuence, and leaders we only show the way and not telling the way.
Pole nimetumia lugha ngumu kidogo, ila kwa kuwa wewe ni mwanaume mwenzangu, unapaswa kuambiwa vyako ili upone.
Best to you.
Tized.
Tized ushauri wako ni mzuri ila sikubaliani nao kwa kiasi fulani.
Umesema kwamba tatizo liko kwa jaxonwaziri na umemshauri kuwa ajifunze to appreciate and compliment his wife.
Kwa nini sikubaliani na wewe katika kipengele hicho; ni kwa sababu hujui / hatujui ni katika jambo / mambo yapi jaxonwaziri amekuwa akimkosoa mkewe kwa ukweli na udhati kama alivosema.
narudi kwnye upande wa babu Asprin kwamba jaxonwaziri amlete mkewe hapa ili tusikilize upande wa pili ndio tuweze kushauri, kwani hapo tutaweza kujua who is wrong and who is right.
Since kumleta shemeji yetu hapa litakuwa ni kizungumkuti tunamuomba jaxonwaziri atueleze japo in brief ni kwa mabo yapi amekuwa aki offer his candid opinion to his wife; hapo tutaweza kujua who is wrong and who is right ili tumshauri ipasavyo.
jaxonwaziri what is it that your wife anataka umpake mafuta kwa mgongo wa chupa????????????
My fellow married men, your advice please.
Married women,give me insights into woman's view and point out where I am wrong.
Mkuu chardams you have a very valid point. Labda itasaidia akitoa maelezo ya ziada... ila ukimsoma vzr unaona ni mtu anaependa kuona vitu perfect kila wakati, trust me hata kama ni bosi mahali walioko chini yake lazima nao watakua na ishu flani naye hata kama hawamwambii au kumuonesha.
Napenda sana kuangalia vitu from behind the scene...... Nilivyosoma ishu yake nilipata picha flani na ushauri wangu umelenga kwenye attitude yake ya u-perfectionist ambayo pia ameikiri kuwa anayo. Na kwa uzoefu mdogo nilio nao (nimeuelezea kwenye comments zilizofuata) ni nadra sana kuwa perfectionist halafu uweze ku-appreciate machache au mengi aliyo nayo mwingine. you just spot what is wrong, or what needs to be done. Period. yale mazuri na mema unaona kama ni wajibu wake. Sasa ukute ni hivyo na mke wake anajitahidi kila siku kuboresha vile vichache anavyoviweza lakini jamaa akirudi haoni improvement yeyote japo ipo... yye ni kukomaa na kuongeza kero nyingine mkewe arekebishe nayo.
We are all human beings, we need to be appreciated by the little things we do, being appreciated fuels you to do even better. Kukosolewa kila saa kunakuondolea ujasiri, kunakupa woga/kunakupa kutojiamini, uchungu, hasira, kunakunyima furaha, unatamani uwe mbali na huyo mtu maana akiwa karibu tu unalo... n.k
Si unaona mkuu chardams ulivyoanza comment yako? ''Ushauri wano ni mzuri ila.....'' Unaonaje ungeanza kwa kuniponda kwanza?....... wahenga walisema Never criticise before you genuinly praise''
Mkuu kwanza poleni. I know very well what you are going through (believe me). Si kosa lako wala lake, ni kosa lenu...
Labda nikupe a little insight kuhusu sisi.
No, i'll start by telling you about my wife. Ni mwanamke wa pekee(to me), yani huwa sidhani kama nikipewa chance nyingine ya kutafuta mke nitabahatika kiasi hiki. Ana uwezo mkubwa sana wa kushirikiana katika kusolve tabu. Kila gumu tulilopitia tumelisolve pamoja na watu wa nje hawajawahi kuingilia maamuzi yetu.
Yani there is a time ninashindwa kabisa kurekebisha kitu na she does it. Ananiheshimu sana. kuna mengi naweza kuelezea ila tuseme tu namshukuru Mungu kwa mke huyu. However, I tell her sometimes how lucky I am, Ila mara nyingi namchukulia poa. Atajitahidi sana kunifanyia vitu(atapika kama tuna sherehe, ataninunulia vitu, atanipa special care n.k) ili nimpe baraka za sifa lakini either ntajisahau, ntafanya makusudi ama basi tu ntachukulia poa. Na mimi mtu huwa akikosea namuambia hapohapo na hutasikia tena nasema, nasahau. Kiukweli tangazo la waume bora likitolewa na mimi ntaenda (hata kwa kujifichaficha!). Meaning, I am just an average guy doing everything i can for my wife, but i have faults(kwanza nyingi).
Mahali tulipocollide na wife ni hapa. Nikimkosea hasemi anavumilia tu, siku nikimsema akikasirika ataanza kusema things za way back(though kila kitu huwa ni mimi na yeye, mtu wingine haingizwi). Kuna mara tukaanza frustration.
Mimi nikajiangalia kuwa recently akikosea namwambia! akifanya vizuri kuliko kawaida, napotezea hiyo ikapelekea akaanza kujiona a bad wife...Kwa sababu mkuu, hatuko perfect na tunajisikia vibaya tukikosea ila ni zile sifa za wenzetu wakati tunapofanya vizuri ndio hutukumbusha kwamba nasisi ni binadamu wazuri regardless of our weaknesses!
Na hata mtu akikwambia hajali ila bwana opinion ya your significant other ina nguvu sana kwenye your self value.
Na yeye akaja kujua kuwa sipendi aumie kimya kimya akawa ananiambia. Sasa mimi nikikosolewa nakuwa very fine with it. Ila sasa nikikosolewa sana, nakosa muelekeo kwamba, mbona hakuna jema ninalofanya? Sometimes I felt like a useless husband (nasema kweli). Tukaanza kuwa hatusemezani sana. Basi one day akaniambia, "If I was given another chance to look for a husband, I don't know what I will do if I couldn't find you". Huku analia! Dah, that is one of the days that niliinjoy ndoa jamani. NIlijiona booooonge la dume la mbegu. Yani nilitakiwa kwenda kazini jumamosi, kisha kwenda kuwasalimia ndugu fulani na kikao cha harusi, kisha jumapili ibadani kisha twende kwa mama. Hapo ratiba ya mpira hujaweka. I CANCELLED ALL THOSE THINGS.
Nillimpeleka honey wangu Zanzibar tukaenda kuchoma lots of money ambazo hata sikuwaza naweza kuwa mpuuzi kiasi cha kuzitumia, kuanzia saa 12 jioni ijumaa hadi jumatatu na kazini nilichelewa. It was the best time I have ever had!
Dah! ndoa tamu weweeee!!!!
Mi bado sijaoa na sitegemei kuoa ngoja nipite manake ushauri ntakaokupa utaongeza utata tuuu hapo home! Over
So wewe ni jinsia gani?au unategemea kuolewa.
Hutokaa upende kitu asilimia 100 brother. Try kuchukua muda uenjoy wife anavyomanage jiko na usafi. Hata kama ataanza kwa kutokukufurahisha, taratibu akijua anachofanya ni cha muhimu kwako huku ukimpa sifa kwa improvement. Itakapokuja akaanza kuona usafi na chakula chake ni kitu unaenjoy lazima aongeze manjonjo. Kiukweli mimi ni mchaguzi sana wa vyakula. Cha kushangaza (I still wonder) asilimia kubwa ya atakachopika wife nakula. Na hata simkosoi. Na kwenye kula napendwaje? Yani hata nije saa 9 usiku for absolutely no reasonable reason. Kama sijala na hakuna chakula ntaandaliwa, nikimaliza kula ndo niulizwe kulikoni kumjia saa9?1. I happen to be very particular in my tastes.
2. Suala la kuwahi kuamka na kuweka mambo ya nyumbani sawa, be it we are travelling, we are going to church etc. Ni mzito ajabu, na nikijaribu kumuamsha na kumuhimiza anakua very reluctant.
3. The matter comes anapokua mwenyewe, she may appear not as per my liking (ilhali najua uwezo wa ku-appear alikua nao na nguo kaziacha nyingi na nzuri ndani).
And so are all women! She is normal kabisa. Mungu aliyewaumba hivyo ndiye ajuaye faida za kuwa hivyo. Inawezekana kwa kujudge kwake by feelings ameshafanya maamuzi mengi mazuri ila hujaona tu. Sikatai kuna rational decisions ambapo wewe ndiye unatakiwa kuongoza ila kuna decisions za feelings ambazo only her can see.4. anapenda sana ku-rely kwenye 'feelings'
5. To us it was just normal or felt normal basing on our background but kwake yeye alovyoyachukulia it is like hatukuyapa baadhi ya mambo uzito uliostahiki.
Only God can make a human to be such. Hapa muombee na Mungu atamsaidia.6. I like a God fearing, constant God seeking woman.
Mkuu, Sasa hivi kuolewa ni Independent Variable, jinsia zote zinaolewa, hali imekua mbaya...
Mkuu PetCash shukrani kwa inputs zako.
Nadhani nijipange kuufanyia kazi ushauri wako na wa wadau wengine hapo juu.
Najua wife atapita hapa na kuona mjadala ulivyokua, apate ujumbe pia kua it has not been easy on me.
Weekend njema nyote