Skillionare
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 1,190
- 523
Nimeupenda huu mnakasha mm nlikariri tu sayansi wakuu !
The speed of light in a vacuum(c) is not a constant. Is the particle of light,the photon do not have mass? where is the vacuum?Is the speed of light in a vacuum (c) a constant or not?
Sasa mbona tunakubaliana. Umeshasema kuwa equation ile ni "good approximation!!". Maana yake ni kuwa katika matumizi halisi (practical applications) madhara ya migongano kutokuwa "perfectly elastic", madhara ya "intramolecular forces", madhara ya hivyo vitu vingine vyote ni madogo tu. Hapo ndo maana ya approximations.
Tunatengeneza hypothetical ideal gas ili tuweze kutumia milinganyo kukokotoa matokeo fulani fulani. Ndiyo maana inabidi ukokotoaji huo ufuatwe na majaribio halisi. Majaribio hayo huthibitisha kuwa madhara ya vitu vile tulivyovipuuzia kwenye milinganyo ni madogo mno kwenye tokeo la mwisho. Tukishajiridhisha hivyo kwa kufanya majaribio ya kutosha na kulinganisha na matokeo ya kimahesabu ndio maana inawezekana watu kujua hata kiwango cha kosa (Margin of error). Kutokana na kujua kiwango cha kosa, kwenye matumizi halisi (practical application), Callibration hufanyika ili kuondoa kosa hilo.
Ndugu yangu, ndo maana watu walikwenda kwenye mwezi na wakarudi salama. Ingekuwa "approximations" maana yake ni uongo matokeo yake ungeyaona. Ndo uzuri wa sayansi. Tena akija mtu mwingine akatumia milinganyo ile ile na kufanya "assumptions" zile zile, matokeo yake huwa ni yale yale. Hapa ndo tunasema sayansi ni "superior" kuliko maalifa mengine ambayo binadam ameshayapata.
Tatizo la maarifa mengine kama yale ya dini na ushirikina, au mazingaombwe; mtu mwingine hawezi kuiga ulichofanya wewe na akapata matokeo sawa. Kwenye dini mtu unaweza ukafanya yale yale aliyofanya mwenzio, yeye akafanikiwa, wewe ukashindwa; halafu mtu akasema aaaa si mapaenzi ya mungu!!!! Mungu huamua pale anapotaka!!!!! n.k. Inaonekana maarifa kuhusu mungu anataka nini na wakati gani hayatoshi na kilichobaki tunakuwa tunadanganyana tu!
Sayansi ni mwisho wa uongo. Approximations na assumptions kama zimekosewa, ni wazi kiwango cha kosa (error margin) kitakosewa. Kiwango cha kosa kikikosewa "callibration" ya kuondoa kosa hilo haitafanikiwa. Kosa lisipoondolewa, balaa litaonekana kwenye matokeo ya mwisho; yaani kama ni jengo litadondoka, kama ni ndege italipuka hewani au kuanguka, n.k. Uhandisi wote uliopo, tiba, n.k. vyote hutegemea approximations na assumptions. Ukiona hizo fani zinafanikiwa na kutoa matokeo halisi, ujue assumpitions na approximations ni halisi!!!
Dhana ya CONSTANT ni muhimu sana kwa watu wanaokariri,ukianza kutafakari tu,CONSTANT ni uzushi kweupe,wanasayansi wengi sana walitumia Constant ili kufikia hitimisho ya kile ambacho wameshindwa kukitambua kutokana na mapungufu ya kibinadam, Kama wahasibu vile,trial balance ikigoma unaweka balancing figure, kwa kuweka suspense akaunti,wakati wahasibu wanakuwa na kibarua cha kuondoa hiyo balancing figure,wanasayansi wanakomea hapoooooooooo hapo. Na wengine huendeleza utafiti kwaanzia na fix husika na kwenda mbele,huku wakitegemea peer review,kwa miaka mingi sana mwanafizikia Isaac Newton kwa kutumia sayansi hiyo hiyo aliupiga fix ulimwengu,na kwa kuwa wengi sayansi ni kukariri kwa kwenda mbele,baada ya kuoneshwa mapungufu ya kazi nyingi za Newton baadala ya kufunguka na kuona Fix zilivyonyingi kwenye sayansi ndio wanajikita kueneza imani kwa sayansi ndiyo mwake kila kitu kiko waaaah.
Tatizo lako ni kuwa unafikiria Constant Maana yake ni namba isiyobadirika. Kuna constants kama PI ambazo hazibadiriki. Lakini katika milinganyo kama hiyo, constant ni namba ambayo kuwepo kwake hakuathiriwi na "variables" za mlinganyo wenyewe. Kwenye mlinganyo huo ulioutoa maana yake ni kuwa nR haiathiriwi kwa vyovyote vile na P, V na T.
Sasa tuje kwenye "assumptions". Nadhani unajidanganya kwa kusema eti kwa sababu kuna "assumptions" ndo maana huamini sayansi!!! Mhhh, hapo naona ajenda yako ni nyingine. Ungesema kuwepo kwa "assumptions" kunafanya vitu vishindikane!! Hapo ungeleleweka! Sasa ukiangalia mfano wa ndege ulioutoa na eti zimefanyika "assumptions" nyingi!! Ni kweli zimefanyika, je ndege hairuki na ikatua?? Ni mamilioni mangapi ya watu wanasafiri kila mwaka kwa kutumia ndege?
"Assumptions" ni vitu ambavyo madhara yake kwenye matokeo ya mwisho ni madogo mno pamoja na kuwa vipo. Nadhani "assumptions" zinaonesha ushindi zaidi kwa sayansi kuliko kushindwa. "Assumptions" zinaonesha kuwa yule anayezifanya anazijua kuwa zipo; zinaweza kuleta madhara katika mazingira fulani; ila katika jambo hilo hazina madhara. Kwa mfano unapojumlisha namba moja kubwa sana na namba moja ndogo sana, katika matumizi ya kawaida tunasema ile namba ndogo sana ni sifuri na hivyo mchango wake kwenye jumla nzima hauna maana (tunaupuuzia - neglect).
Kuzungumzia 0-2 na kupata -2 mbona hili ni jambo linaloelezeka kirahisi sana. -2 ni deni. Hiyo mbili umeikopa kutoka sehemu fulani ndo ukaiweka pale (ndo maana inabidi uweke - kumaanisha kuwa hii mbili imekopwa kutoka mahali). Pengine wewe ulisoma hesabu tu kama kasuku hukufundishwa matumizi ya mahesabu ndo maana unachanganywa na mambo yanayoelezeka kirahisi mno. Ni kweli kuwa waalimu wengi huwa wanapofundisha hawayaweki mambo haya katika "context", kwa hiyo, "casual learner" unaona kama unafanyiwa mazingaombwe au viinimacho. Hapana, si viinimacho hivyo!!
we mwongo wewe katika fluid mechanics hakuna PV=nRT....labda ungesema kinetic theory of matter au Thermodynamics usitudanganye toka hapa!
ipo, hata mimi nimeisoma mwaka wa pili chuo!
The speed of light in a vacuum(c) is not a constant. Is the particle of light,the photon do not have mass? where is the vacuum?
we mwongo wewe katika fluid mechanics hakuna PV=nRT....labda ungesema kinetic theory of matter au Thermodynamics usitudanganye toka hapa!