Bila kumsahau Konfara Ngon'gweraWewe Hatukusema UZALEENDO UMETUSHINDA....... Tuliimba, Tumekosa uzalendo tumekosa uzalendo
Binafsi nilifurahi sana, Mechi ambayo sitaisahau ni Ile ya Simba Na Atletico sports Aviacao ya Angola
Ilikuwa na wachezaji kama Kanka Wemba, Abilio Amanali, Gito, Bravo, Lolo, libenge, Yanda
Aliahidi gari aina ya KIA kwa kila mchezaji,wachezaji walikua 30,sasa piga hesabu..baniani ikabidi afanye ubaya wake,akatembeza hela kwa wachezaji muhimu wa simba,simba akafungwa kizembe,mzee mwinyi akiwa mgeni rasmi ilimuuma sana,akawaomba wamwingize lunyamila,akaambiwa yule yanga
Kimti alikuwepo, nakumbuka zike Corolla walizopewa badala ya Kia, ya Damian Kimti ilibiwa.Damiani Kimti,
Simba ndio hiyo imetua kwa MO Yanga sijui itaenda kwa nani? Tatizo tunalo sisi wenyewe hatupendani hata kama tunawezaThat why siwaamini wahindi kabisa, thanks kwa James siang'a kwa kutufumbua macho jinsi wanavyouza mechi hao wahindi, hawahai kupewa timu kabisa.
Leo umetobolew na azam 3 khaaa ushakua handaki ssMkuu
Hakuna aliyeuza game, ila uwezo wako Simba uliishia hapo, n'a aibu tukaipata mbele y'a Rais wetu mpendwa Mzee Ruksa, kama ilivyokuwa jana mbele ya JPM, Kagera wakajitobolea Tundu Tobooo... Kuisha habari yao.
Ww mwaka huu unafanya nn zaid ya kutudhalilisha tu 4GMleta mada bora umeliibua hili...hatutaki upuuzi kwenye michuano ya CAF kwa vilabu bingwa msimu ujao. Simba macho yetu kwenu hata kama sisi ni watani zenu...hatutaki mtudhalilishe tena kama 1993.
Sawa ila siyo mbele y'a Mh. Rais. Hiyo ni record yenu Simba, hata mtoto mdogo akiulizwa timu gani Mh. Rais JPM alisema mbele y'a TV kuwa imetobolewa Tundu, utasikia SIMBAAAA.... Kama unabisha Jaribu kuwauliza watoto nyumbani kwako au mitaani kwako alafu tupe mrejesho.Leo umetobolew na azam 3 khaaa ushakua handaki ss
Mkuu alikua anaitwa sekou bambaAcha uongo Boli Zozo alifunga goli la pili. Goli la kwanza lilifungwa na Ceku Bambe
Sasa utashangiliaji mtu mshindwawaliwaomba yanga wawe na uzalendo wawashangilie na yanga walifanya hivyo lakini baada ya kutunguliwa goli 2 na bolizozo, Yanga wakaanza kuimba uzalendo umetushinda
Jumapili ya 19/5/2019 kwenye kipindi cha Sports AM kinacho rushwa na Azam TV kikiongozwa na Mahmud Zuber, Ali ulizwa mgeni mwalikwa aliyekua mchezaji wa Simba na aliyekuwepo kwenye timu iliyo ingia fainali ya 1993 Fikiri Magoso.Ilikuwa ni game ya fainali ya kombe la Caf mwaka 93 kati ya Simba Sport Club Vs Stella Abidjan ya Ivory Coast.. Tetesi zilizoenea mitaa ya jiji la Dar WS Salaam na viunga vyake ni kwamba Simba Sc waliuza hiyo game..Wadau wa Soka la Bongo ..What do u think ? Ni kweli Simba waliuza hiyo game ? Kama waliuza nani walihusika na mchezo huo mchafu ?
umewasahau usm el harrach tuliwapiga 3-0 Taifa, kwao tukapigwa 2-0 robo fainaliTulianza Kwa kuwatoa Ferroviario ya Msumbiji Kwa advantage ya Goli la ugenini hapa tulitoka bila nila kwao tukatoka Moja Moja
Tukaenda Robo Fainali tukamchapa nje ndani Timu ya Manzini ya kule Swatziland
Tukaingia nusu Fainali tukacheza Na Club bingwa ya Angola ya wakati huo inaitwa Atletiko Aviacao hapa Taifa Tukampiga Tatu Kwa Moja then kwao tukapigwa Moja bila wakawa wametoka
Tunaingiza Fainali Sasa hapo, Ikawa Simba vs Stella Andijaa
Mechi ya kwanza tukaanza kule Kwao Ivory Coast tukatoka nao suluhu ya Bila ya kufungana
Sasa Kombe Uwanjani ya Kombe la CAF Africa nzima ikafanyika Uwanja wa Taifa
Mgeni wa Heshma akawa Rais Ally Hassan Mwinyi akisindikizwa Na Waziri wake wa Michezo Prof Philemon Sarungi ( Mshabiki wa Simba damu)
Wakati huo Kocha wa Simba akiwa Abdallah King Kibaden Mputa Na Msaidizi wake akiwa Hassan Hafif
Tukapigwa Goli la kwanza Uwanja Ukawa kimyaaaaa Mara likaingia la pili Mchomo uliopigwa umbali wa mita 18 hapo ndipo Kelele za Mashabiki wa Yanga '...Uzalendo umetushinda...' Ndio zikaanza
Mpaka Mwisho bila ya kutegemea Mzee Mwinyi akashuka Jukwaaani Kwa huzuni usoni lakin akiwa Na furaha moyoni Kwa Kuwa Nae Ni Yanga Damu Kuliko Mzee Akili Mali
Baadhi ya Wachezaji ninaowakumbuka wa Simba Ni Mohamed Mwameja, Hussein Masha, George Magere Masatu, Alfred Kategile, Damian Kimti, Alfred Kategile, Alphonce modest, Makenzi Ramadhan, Dua Said, Edward Chumila n.k
Personally naamini Kwa Umri wangu niliosalia sitoishuhudia Simba bora ya kiwango ile
Mzee Mwinyi akakabidhi Kombe Kwa kina Bolizozo nao usiku ule ule wakaondoka Na Kombe kupumzika Nairobi
Nakumbuka Siku chache kabla ya Mechi, Uongozi Na Mashabiki wa Simba hawakuwa wakijadili Mikakati ya Ushindi wa Mechi hiyo bali walikuwa wakijadili Kombe litakaa wapi baada ya Mechi hiyo wengine walisema Ikulu, wengine BOT hakuna kujadili Mikakati ya Ushindi
Jumapili ya 19/5/2019 kwenye kipindi cha Sports AM kinacho rushwa na Azam TV kikiongozwa na Mahmud Zuber, Ali ulizwa mgeni mwalikwa aliyekua mchezaji wa Simba na aliyekuwepo kwenye timu iliyo ingia fainali ya 1993 Fikiri Magoso.
Alichosema Aliyekua mfadhili ndugu Azim Dwji japo yeye Fikiri Magoso hakutaka kumtaja jina ila anafahamika nani alikua mfadhili kwa wakati ule.
Dewji aliwapa fedha baadhi ya nyota wa Simba ili wafungwe. Kwamujibu wa Magoso anadai inawezekana labda ahadi aliyoitoa ilikua ni kubwa na hakutegemea timu itafika fainali.
Anadai kule Angola baada ya mechi kwisha kwa suluhu ya bilabila na timu kufuzu baadaya ushindi wa tatu kwa moja, Dwji alizimia na yeye alikua mmoja wa watu waliomsaidia wakati amezimia kwakua alikua kwenye bench.
Baada ya Mechi ya fainali hapa DAR kwisha wao walijua ninikilitokea mbaka wakapoteza ile mechi na baadhi ya wachezaji akiwemo yeye Magoso , Godwin Aswile,Ramadhan Reny, Dua Said na mwingine ambaye alimtaja ila Mimi nimemsahau , waliamua kutaka kuitoa siri ya nini kilitokea kwakua lawama zote zilikua juu yao wachezaji.
Mfadhili aliwaita pembeni wale waliotaka kutoa siri na kuwapa shilingi lakitano kila mmoja.
Shida ilikuja baadae, Baada ya kukosa kombe waliahidiwa watapewa zawadi ya gari ndogo. Baada ya gari ndogo kutolewa kwa wachezaji, shida ikarudi kwake yeye na wale walio pewa zile lakitano kwa kila mmoja.
Mfadhili alitaka kwanza warudishe zile laki tano, ndio wapewe zile gari ndogo, kwaiyo wachezaji karibu wote walipewa zile gari ila wao waliopewa kiziba mdomo walichenjiwa kibao, sasa katiyao kila mmoja alitumia njia yake kuweza kupewa gari. Anadai katiyao (walio kula kiziba mdomo) kunawengine hawakurudisha ila gari walipewa ila yeye alitafuta mbaka akaipata iyo laki tano na kuipeleka na kukabidhiwa gariyake ndogo.
Ni bora Azim angeacha Simba ishinde halafu asiwanunulie hizo Kia.
Kuliko alichokifanya.
Kama ni ukweli basi hao akina Masatu, Mwameja na Masha wanatakiwa wahojiwe na Takukuru kwa kulihujumu Taifa.
Mimi ningekuwa wao ningechukua pesa na ningecheza kwa uwezo wangu wote ili kukinda heshima ya Taifa na Michezo kwa ujumla.
Aiseee,kweli hii kali hata hivyo bila huyo mwandishi wasingejua kwani teknolojia ilikuwa chini sana.Ki ukweli mechi ile simba walizidiwa ki uwezo, ki uchawi kizengwe na ki mkakati. Stella abijan waliigawanya timu ya mara2, kundi la wachezaji wa kwanza kilikuwa ni kikosi b lkilitua dar wiki1 kabla ya mchezo, simba wakawa wanakiloga usiku na mchana, kundi la2 yaani kikosi cha kwanza kiliweka kambi nairobi na kilivuka border na kufika dar j5 na kilifichwa ubalozin adi ijumaa jioni ndiyo wakafanya mazoezi mepesi uwanya wa Tanganyika packers, kwenye hicho kikosi kulikuwa na wachezaji3 wa kukodiwa viungo2 na beki1ambao waliwadhibit wachezaji wa simba vilivyo, siku3 baada ya mechi simba waliwakatia rufaa ambayo caf iliitupa kwa vigezo kadhaa na mtonyo huu simba walipewa na mwandishi wa habari wa stella abijan.......... ni story ndefu kidogo, binafsi nilibahati kutoka