What Made You Stay?

Kama una mtoto wa kike mlee kujiamini hamna mwanaume atakaye inua mkono wake kumpiga hata kofi. Nina ndugu wanne watatu ni wakubwa kwangu wote wameolewa wengine wanakaribia 20 years kwenye ndoa; hamna alowahi kupigwa hata kofi kwa kuwa hatukulelewa tuje tunyanyaswe na wanaume! Make your daughter confident. Nilishaeleza jinsi baba alivyotulea.
 
You said it all nyumba kubwa
 

...this is sooo humbling...do i deserve this? ...hahhh?
mwj1....story ya maisha yako waweza tunga kitabu na kuuza copyrights za sinema...
kwangu mimi, wewe ni rafiki mrembo, rafiki mwema, mwenzangu, mshauri wangu, soulmate wangu.
Naendelea kukuombea mw'mungu akuzidishie moyo huo wa upendo na kusamehe,...hayo uliyoyapitia,
mwenyezi mungu tu ndio mfariji wa kweli kwa neema zote anazoendelea kukujaalia na atazozidi kukujaalia...
 
Kuna kitu kwangu imeshakua fumbo la imani,
Iweje watu hao hao walitakana wakakubaliana na wakapendana sana hata kufikia kupata watoto,
Baada ya muda moto wa chuki utakao waka huko ndani, hahuna wa kuuzima, kwakweli shetani ni muongo sana.
Kwa utamaduni wetu wa kiafrika tena sanasana kwetu Tanzania, wanawake niwaoga sana kuanza maisha.
Kwa kuogopa watu watasemaje au watakushangaa umeachana na mwanaume, na una watoto, lakini kuliko uishi maisha,
Ya ndoa kwa miaka mingi ya mateso na machozi mengi, ni bora tu uanze maisha, na kwa hali ya sasa no one atakunyooshea,
Kidole kua una watoto bila kuishi na baba yao. Kwani single parents wanaongezeka kila kukicha, na wanaume wasiku hizi
Wengiwao ni waelewa swala la watoto kwao wala sio shida, akiamua kua na mtu hata kama ana watoto, na cha kushangaza
Atawapenda sana wale watoto kuliko hata baba yao.
 
Reactions: Mbu
Ila huwa nashangaa sana katika hali ya sasa bado kuna watu wananyanyua ngumi kuwapiga wake zao. Ni jambo la ajabu sana

Mara nyingi wanaume wa hivyo hawajiamini kabisa; nasema hivyo kutokana na experience. Chunguza almost wote sababu ni wivu ambao hugeuka kuwa obssession yaani mwanaume anaamini anakumiliki kama vile gari!
Na bahati mbaya wengi hatujui kutofautisha wivu wa kawaida na obssesion; hivyo twatumia msemo wa "wivu ishara ya mapenzi".
Hivi katika jamii atakayekuudhi/kukosea ni mkeo tu? Ukigombana kazini na coleage wako unampiga? Au kwavile ni mwanaume mwenzio so huenda akafight back? Why mke? Hivi wewe hujawahi kumuudhi mkeo, kwanini naye asikupige? Au kwa vile wewe umetoa mahari? Kama ni mahari mbona India wanawake ndio wanatoa na bado wanapigwa?

Anyway real men don't beat their wives only the weak and insecure men!
 
huyo mama mkwe wako i hope alikua anakupa support wakati wa mateso yako,otherwise i am nt on her side! mwj1, im sorry abt what happened to u. with tears in my eyes,i am so poud of u gal! huyo mwenzio wala usimuombee,hatobadilika! omba mungu akupe upendo mpya,wa maana! umesema vyema,familia ama marafiki ina sehemu kubwa sana kwa ajili ya victim wa abuse! nilimsaidia wifi yangu ambae alikua victim,namshukuru mungu sasa amesimama. ilikua baada ya kutoka kwake kumtembelea,na kumuacha na useless (she called him hubby), ile naingia kwangu napigiwa simu jamaa keshamkata mapanga. the scene, the blood, the kids faces! i am proud of me for that,kati ya mafanikio yangu hili ni mojawapo!
ngoja nikasali kwanza,nitakuombea leo!
 
Pole sana kwa Anjela na pole kwa mwjmii one. Hii thread imenitoa machozi .Mimi tuna magomvi na mume wangu lakini sikubaliani na makofi.Aliwahi kuthubutu kunipiga siku moja na siku hiyo nilienda polisi sikuwa na huruma na unyama wake,hii imemfanya mpaka leo asirudie tena kunipiga.nisingeenda polisi inamaana ingekuwa ananipiga kila anapojisikia.
 
Pole sana kwa kweli endelea kumuomba Mungu upate ujasiri zaidi
 
King'asti ubarikiwe sana haya mambo sijui lini watu watayaacha
 
Mbu ulikuwa mitaa gani bana tulikuwa tunakutafuta na soulmate lol
 
Mamushka nafikiri watu wanahitaji kujitambua wao ni nani na hatua anayokuwa amefikia inabidi kuchukua maamuzi bila kujali nani atasema nini na kitu gani
 
Kaunga ulichoongea kina ukweli ndani yake kuna wanaume hawajiamini basi wanatumia weakness hiyo ili wafiche udhaifu wao na kujifanya ni wababe kwa wake zao
 
so bad bora asingemuoa kama ndio anampiga kiasi hicho khaa watu wengine bana sijui wanafikiri kuoa ni sawa na mbio za vijiti mnapokezana..

na yeye angela itabidi apate ushauri wa kufa mtu..
 
so bad bora asingemuoa kama ndio anampiga kiasi hicho khaa watu wengine bana sijui wanafikiri kuoa ni sawa na mbio za vijiti mnapokezana..

na yeye angela itabidi apate ushauri wa kufa mtu..
Ndetichia mimi nafikiri huo ni udhaifu fulani Kaunga kasema mbona rafiki yako akikusoea haufanyi hivyo kwanini ufanye kwa mkeo kama sio udhaifu ni nini
 

...kwa kuungama kiukweli tu [individual cases] ndipo utapoweza tambua mzizi wa fitna wa tatizo hili,...lakini
tatizo juu ya tatizo ni kwamba katika wanaume kumi [10] utaobahatika kuwauliza sababu ya kufikia kutumia
ngumi, mateke na makofi kwa wapenzi/wake zao...huenda ni mmoja au wawili anayeweza kukupa jibu la kueleweka.

...the rest, either kwa aibu atasema si kweli kama anatabia hiyo, hupitikiwa tu na shetani, au atasema bila
"kuonyesha" nani ni mwanaume ndani ya mahusiano mwanamke atampandia kichwani.
Hebu tujiangalie sisi wenyewe
tunachangia vipi kwenye matatizo haya...

tukianzia kwenye malezi;.....

wewe kama mzazi, unamuandaa vipi mtoto wako wa kiume kuja kupambana na maisha ya mapenzi, mahusiano?
kila mtu kwa experience yake, tujadiliane umri muafaka wa kuanzia malezi hayo...

-wazazi wengi mnachangia ku create monsters !!!-


Mbu ulikuwa mitaa gani bana tulikuwa tunakutafuta na soulmate lol

...nipo bro,...udhuru kidogo.
 
I wish kama tungepata wanawake wengine wenye udhubutu kama MwanajamiiOne.

Ni kweli mkuu... Huwezi amini, mimi ni mchanga sana katika ndoa lakini ninavyosoma post za wadada hapa najifunza mambo mengi sana. Niko confident kusema kuwa sijawahi kum-abuse mke wangu kipenzi physically, lakini yapo mapungufu ya kibinadamu ambayo posts za kinadada hapa zinanifanya nijtahidi sana kupambana nayo. Shetani ashindwe...
 
Mbu umeongea jambo la msingi sana ni dhahiri inabidi turudi nyuma tujiangalie na jinsi gani tunaelea watoto kama wewe ni mzazi wa kiume mwenyewe tabia ya kupiga mkeo , Je? Siku binti yako naye akipigwa na mume wake utajisiaje au utachukua hatua gani?
 
Reactions: Mbu
Tuko mkuu we acha tu tunahitaji sana kumuomba Mungu ili tuweze kufikia malengo na kuwa na familia yenye amani, upendo , utulivu na kuthaminiana pia
 
Mkuu, hapo nilipokuza, kukozesha na kupigia mstari, ninakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa, lakini udhalilishaji wa wanawake si tabia ya wabantu tu. Hata sisi wabantu tumeanza kubadilika. Wengine wanaona kama mabadiliko haya ni kuwalea vibaya wasichana, pale mama anapomwambia mwanawe m/mke arejee nyumbani, au anpomkemea mume kwa kumwambia "huyu ana kwao, hukumwokota jaani".

Udhalilishaji wa wanawake upo ulimwenguni pote miongoni mwa races zote - Waafrika weusi na weupe, waarabu, wahindi, wachina, wazungu wa mabara yote, na response ya wanawake wengi inakuwa kama hii ya Angela. Ni juzi tu rafiki yangu mzungu alinisikitikia mateso anayopata toka kwa mume wake - wivu, gubu, kisago - na bado anabakia kwa kisingizio cha watoto lakini ukweli ni kuwa anafikiri iko siku mume atabadilika.

Imefikia wakati, kwa takwimu nilizonazo za nchi moja ya Ulaya, wastani wa wanawake watano kwa mwezi huuliwa na waume au ex-wao, ukiwachia mbali ya maelfu wanaojulikana na wasiojulikana rasmi kesi zao; ukilinganisha na 1/45 ya wanawake wanaoua waume zao pale maji yanapowafika shingoni. Imefika wakati pia wanaume/wanawake wanavishwa vilinzi (GPRS) ili kuwakinga mahasimu zao wasiwasogelee.

Tatizo lipo kwenye mfumo dume, toka majumbani hadi serikalini. Angalau kwa nchi zinazoendelea wanajaribu kulipunguza. Mfano ni EU ambapo wamo wanaandaa sheria ya kuwasakama wanaume watesaji na wauwaji. Hata hivyo mitaani, bado mke akiteswa inaonekana kama ni stahiki yake.

Ninachowashauri wasichana wasimame wenyewao kujilinda na hii hali. Mkisubiri huruma ya mume, serikali na familia zetu, mtaendelea kuteswa. Ikiwa sula ni la watoto, watoto si wako peke yako. Na ikiwa ni tamaa ya kumbadilisha mume siku moja, kumbuka kuwa walishishashindwa wazazi wake kumbadilisha. AMKENI
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…