.........Yassin Arrafat............
Tutadai na sisi ufukuriwe wa hayati Mwalimu Nyerere
Wanasayansi nchini Uswiss wamebaini uwezekano wa aliekuwa kiongozi wa Palestina marehemu Yassin Arrafat kuwa aliuwawa kwa makusudi kwa kuwekea madini hatari ya Plutonium.Wanasayansi hao wamethibitisha uwepo wa madini hayo baada ya kuyakuta ktk nguo za marehemu na hali kadhalika ktk vitu vyake kama mswaki n.k.
Mke wa marehemu kwa sasa anataka mwili wake ufukuliwe kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Source:Aljazeera TV.
Halafu mwili wake ukifukuliwa ndo atafufuka? Huko ni kumtesa marehemu. Anayejua kulipiza kisasi ni Yule Muumba.
Mkuu ni Yasser Arafat AKA Abu Ammar, huyu jamaa waisraeli walimdhibiti kwenye kona pale Ramalah, wakamkatia hadi umeme na maji, halafu wakamkatia na suplly za chakula, maji ya chupa ambayo alikuwa akipelekewa na watu wake, na medicine, baadaye wakamfungulia maji ya bomba, maji yenyewe ya bomba yanatoka ama kupita eneo la Israel wanapoishi, nadhani alilazimika kuyanywa, ama hata kunawia, waliichoronga compund yake na mavifaru, wakambakizia chumba kimoja tu, hata choo na bafu vilivunjika, aliishi pale kwa shida sana, ila alibakia na bastola yake pembeni akasema atapambana hadi tone la mwisho la damu, siwezi sahau hii kitu, ni Ariel Sharon mnyama sana.Baada ya kuanza kudhoofu kwa kasi akiwa pale, ghafla waisraeli wakamkubalia mke wake aliyekuwa ufaransa waje wamchukue wakmampatie matibabu, ndo ilikuwa safari yake ya mwisho.
I know that mkuu, ndio maana nilikuwa najiuliza kwa sauti, kwa sababu hata wakijua will it change the direction? Ilishajulikana madini hayo yanaua, na wala hawatamjua aliyetumia silaha hiyo kwa kwenda mbali zaidi, kwa kuwa Yassir alikuwa mpambanaji mashuhuri aliyejulikana kimataifa, hivyo ni kuelewa tu kwamba aliuawa kwa silaha hii. Mbona Patric Lumumba mpaka leo hajulikani kaikwa wapi pamoja na vimanenoneno kwamba alitumbukizwa kwenye acids akayeyuka kabisa na wengine kila wanachopenda kusema. Kujua huko kunawaumiza zaidi ndugu zake na kuvuta nguvu ya visasi. Hukumbuki yanayodaiwa kwamba hata Mzee Karume muuwaji wake alikuwa analipiza kisasi kwa kuuliwa kwa babake? Au kule Iringa yule Kleruu kuuwawa na mnyalukolo kwa sababu ya visasi hivyohivyo? Tuna kheri waafrika wa vijijini tunaomalizia kwa kusema, "Swela bwana" ikaishia hivyohivyo.Mkuu, kwa wenzetu kupata ukweli wa jambo ni value inayojitosheleza; siyo lazima afufuke au kuwepo nia ya kulipiza kisasi. Lengo ni kujua kitu gani kwa hakika kilimuua. Hilo tu ni value.
Kwajinsi walivyomtreat, waliogopa tu lawama wakimwua waziwazi, kwasababu walimdhoofisha wakijuwa wanachofanya, na haya mambo ya sumu tena ndo basi.Mkuu nilikuwa naifuatilia hii issue sana kipindi kile.Baada ya Ariel Sharon kwenda Washington kuonana na Bush, walikubaliana kwamba Yasser Arafat si wa kukaa naye meza moja tena.Bush alijaribu kufanya kinyume na Clinton ambaye aliamini Abu Ammar ni muhimu sana kwenye mazungumzo ya amani.(kama unakumbuka tukio la Camp David ambapo aliwashikanisha mikono na yule Yitzak Rabin kama sikosei)Ambaye waisraeli wenye msimamo mkali walimwua.Kuna Video nilishaona ya mwaka 60 mwishoni na walionyesha kabisa Yassir Arafat akiwa anatembea nje huko Lebanon baada ya mashambulizi makali ya Izrael. Walianza kupigiana simu/Radio call wamuuwe au lah. Mwisho wakaamua kumuacha hai.
Tatizo kubwa walilokuwa nao Izrael ni kuwa waliona heri wawe na Arafat kama Rais maana alikuwa akiwazuia hawa Radicals wasifanye mashambulizi Izrael. Better the Devil you know.... ndiyo ulikuwa msemo wao.
Sidhani kama walitaka kumuua huyu jamaa na hasa ukichukulia alishazeeka na kuwa mtu wa GOOD TIME sana na hasa huyo Mke wake. Kwao ilikuwa heri ya kuwa na ARAFAT hai kuliko Merehemu. Ndiyo maana walikuwa wakipiga ila wanamuacha hai.