jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 24,989
- 22,521
Mkuu Sikonge, mimi nilikuwa nasoma na kutizama mkuu.JMushi1,
Sijui ulikuwa ukifuatilia News zipi. Ila huko USA, huwa mnabaniwa sana News. Ndiyo maana mie husoma news za nchi tofauti na hapo unapata ukweli wa upande wa pili.
Izrael walikuwa siku zote wakiogopa HAMASI wataingia madarakani muda wowote. Hamasi walikuwa wakimuheshimu sana Arafat na kwa sababu wote walikuwa wakipata misaada kutoka Lebanon na hata Arafat alishakaa sana Lebanon, alikuwa ni mtu pekee wanayemfahamu kwa ukaribu.
Hamasi walikuwa wakisubiri tu Arafat afe na wao waje wachukue nchi. Hawa jamaa hata uchaguzi walishinda ila UN wakachakachua matokeo. Mtu pekee alifanya Hamasi wasiamke wakati huo alikuwa ni ARAFAT. Kifo cha Arafat kiliwapa Green light Hamasi na washirika wao na moto ukaanza. Hawa jamaa huwa wanasumbua sana na wana kichwa kigumu kama Hesbollah.
Kumdhalilisha kote Arafat ilikuwa ni kumuonyesha Ubabe na kuwa wanaweza. Kifo chake kingelifanya jamaa apande chat ila kuishi kwake huku akiwa HOI, kulimfanya apoteze sana nguvu. Ila jamaa hawakujua kuwa Hamasi ndiyo walianza kujijenga kwa nguvu kipindi cha baadaye,
Nyakati zile, suicide bombings hazikuwa popular sana kwasababu vita ya Iraki wala Afghanistan ilikuwa bado.Fatah nao ya Arafat, ilikuwa na wing ya suicide bombers kama ilivyo Hamas.Ila Arafat alikuwa akidai hawezi kuwa control, na suicide bombing ilikuwa ndo kama trick yao ya kuwalazimisha Israel warudi kwenye meza ya majadiliano.
Hata ile siku ya 911, wapalestina walishangilia sana na kwenye TV ikaonekana, Arafat ndo akatoa kauli kuwa nao wanasikitika na shambulizi lile, lakini damage tayari ikawa kubwa, na Bushi ndo kuanzia hapo akawa na kisasi naye zaidi...
Bush na Sharon, waliitumia sababu hiyo kumkataa Arafat, wakisema amalize kwanza issue za suicide bombers ndo arudi mezani,then baadae wakasema tayari mikono yake ina damu na hafai tena kwenye negotiations.
Kama yule babu wa Hamas,YULE MLEMAVU AMBAYE WALIMPIGA BOMU,akiitwa Hamad kama sikosei, ndo alikuwa akiweka wazi kabisa kuwa suicide bombing ndo solution.Arafat yeye hakuweka wazi hivyo, lakini Fatah nao bado walikuwa waki claim baadhi ya hizo suicide bombings, na wakati mwingine wakisema siyo wao...Hilo la suicide bombings kuendelea na huku mazungumzo kuendelea at the same time ndo walilokataa kina Bush na Sharon.