WHAT is Going on in PINDA'S mind? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WHAT is Going on in PINDA'S mind?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bongolander, Feb 2, 2012.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Wakuu najua kuna thread zinaendelea kuhusu Mgomo wa madaktari, lakini hii habari niliyoiona kwenye IPP media "Pinda aagiza madaktari wakamatwe" imenitia wasiwasi na kuamua kuiweka post hii na kunifanya nijiulize kama kweli Waziri Mkuu Pinda, ndiye yule aliyekuwa Mizengo Kayanza Peter Pinda waziri Tamisemi. Kauli zake za hivi karibuni zinaonesha kuwa yule aliyekuwa Tamisemi was a very smart man. Understanding, able to express himself and being understood, one who used power of logic and a like. Huyu ambaye ni PM yuko tafauti sana. Unless IPPMEDIA wameongopa.

  Najua kuna madaktari wengi hapa tunaomba mtujulishe ni nini kinaendelea na kwanini Serikali inawabeza.

  Awapiga marufuku madaktari kukutana- Kwanini hataki wakutane? isn't it unconstitutional for him to do so? Hivi kwanini madaktari wasiwe na haki ya kukutana, kuna ubaya ganbi wakikutana kujadili maswala yao?

  “Kuanzia sasa serikali inawahimiza madaktari wote walio katika mgomo kuacha mara moja na kuripoti kazini ifikapo kesho (leo) asubuhi, Jumatatu tarehe 30 Januari, 2012. watakaoshindwa kufanya hivyo, watakuwa wamepoteza ajira zao,” alisema Pinda.

  Aliongeza: “Mikutano (ya madaktari walioko kwenye mgomo) inayofanyika ni kinyume cha sheria. Hivyo, naviagiza vyombo vya dola tusiiruhusu. Hakuna (kukutana) Starlight, Don Bosco wala wapi,” alisema Pinda.

  Kweli waziri mkuu wa nchi naye ameingia kwenye siasa za mipasho, kupamba na wataumishi wa umma kwenye vyombo vya habari? Kuna habari kuwa kila mara walipotaka kuonana naye aliwakimbia, aliwapa kazi hiyo wasaidizi wake. So anawakimbia halafu hataki wakutane kujadili issue zao, what is this Mr PM.

  “Hadi sasa hakuna taarifa kama alimaliza internship kwa kuwa hajawasilisha cheti cha kumaliza mazoezi hayo na hakuna taarifa juu ya mahali anapofanyia kazi. Aidha, Dk. Ulimboka siyo mtumishi wa serikali na wala hajasajiliwa kama daktari,” alisema Pinda.

  So is the issue here uhalali wa Ulimboka, au kuna bigger picture ya issue nzima ya uozo kwenye sekta ya afya? How come this Ulimboka guy becomes the topic? Ina maana kukutana kwa watu ni kosa kwa kuwa kiongozi wao si dakatari halali? udaktari halali ni upi, wa vyeti bandia au? na unahusiana vipi na issue nzima ya maslahi ya madaktari Tanzania? Kwanini wale wa Mikoani wamegoma, au maedanganywa na Ulimboka???   
 2. Michael Pima

  Michael Pima Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Madaktari ni sehemu ndogo tu ya wanataaluma wa Kitanzania ambao hupewa stahimili chini ya kiwango. Kuna wana Taaluma wengi sana wa Kitanzania nchi za nje tena wanaofanya kazi kubwa kuzidi wenye nchi hizo. Wanataaluma hawa wa Kitanzania ukiwagusia suala la kuijenga Tanzania kwa kufanya kazi Tanzania wanakuona umerukwa na akili. Nadhani mazingira kama haya yatazidi kuwapukutisha wanaTaaluma wetu kutika Tanzania na kwenda kwingineko wanakodhaminiwa. Hata yule ambae hakuwa na mawazo ya kukimbia nchi sasa atayapata. Kikubwa ni kukaa mezani na kutimiza stahili za kila upande kwani mabavu hayajengi bali hubomoa.
   
Loading...