Siku zote huwa tunafundishwa kuwa mke au mume bora(wife material or husband material) hawana bei, hawahongeki, hawaibiwi wala kuporwa.
Kuna wanaume na wanawake wanaolalamika kuwa wanaibiwa wake au waume zao. Pamoja na hayo huishia kuweka uadui na huyo anayemtuhumu kumuibia bila kujua kuwa mwenza wake ndio tatizo.
Matatizo ya kimahusiano kwenye ndoa nyingi leo yanashindikana kutatulika hadi kufikia hatua ya wawili kutengana kwa sababu wanafunika makosa yao ya zamani kwa makosa ya wa.ayoyaona sasa.
Nawaambia bila kujali mahusiano yenu yana muda gani kuwa, mnafanya makosa makubwa wakati wa kuchagua wapenzi kipindi cha mwanzo.
Uchumba hivi sasa umepoteza maana tofauti na kipindi cha nyuma ambapo kilikuwa ni kipindi/muda wa wawili kufahamiana kabla ya kuianza kuishi pamoja.
Leo vijana wanakutana wiki mbili tu bila kuchunguzana wanafunga ndoa bila mmoja kujua tabia ya mwenzake ilivyo. Wanakuja kushtuka kuwa tabia zao haziendani wanaamua kuachana baada ya kuona hakuna muafaka.
Hii ipo sana kwenye familia nyingi tu ndio maana siku hizi kumekuwa na ongezeko kubwa la mabinti kuzaa watoto bila kuolewa.
Niliwahi kumsoma mwanasaikolojia mmoja anasema kuwa tendo la kwa mara kwanza kwa wanandoa lina impact kubwa sana kwenye kulinda ndoa yenyewe kutokana na upekee wake.(hapa kuna wataalam wanaweza kurlezea zaidi)Hivyo mwanasaikolojia huyo anashauri kuwa vijana hawana budi kutunza miili yao hadi pale watakapofunga ndoa.
Kwahiyo wale mnaolalamika kuwa ndoa zenu zina matatizo ni kwa sababu mmeasi kanuni za asili, mmefanya zinaa/uasherati halafu baada ya miaka kadhaa ya kuishi pamoja mnaanza kulalamika huku mkisahau jinsi mlivyoanza. Matatizo yale ya mwanzo yanawarudia kama matatizo mapya.
WHAT GOES AROND COMES AROUND