Nachangia mada hii kama mtaalamu/expert.
Kwa muda mrefu sasa (zaidi ya miaka 5) antivirus bora kuliko zote ni Bitdefender. Huwa inafuatiwa kwa ukaribu kabisa na Kaspersky. Zingine zote hubadilishana nafasi kuanzia ya tatu na kuendelea.
Bitdefender ilikuwa na tatizo moja tu nalo ni kuizidi nguvu kompyuta kama processor na ram ni ndogo. ila kwa sasa hilo si tatizo tena kwakuwa sikuhizi mashine nyingi zinauwezo mkubwa.
Nashauri utumiaji wa Internet security badala ya antivirus kama unaitumia sana online. Hata mambo ya e-banking huwa salamazaidi. Binafsi natumia Kaspersky internet security na sijawahi pata tatizo kubwa sana kwakuwa hata kama nitapata atack haitachukua hata wiki nitapata update yenye uwezo wa kuondoa tatizo hilo.
Avast ina uzuri wake. Wakati wa kuondoa virusi baada ya kushambuliwa. On boot scan ni utility inayotumika kuiruhusu avast ianze ku operate kabla ya operating system yako na kwa hiyo virus hata vikiwa na uwezo wa kupambana na antivirus hapo vitafeli. Hii ni kwa kuwa virusi na minyoo (worms) wengi hufanya kazi juu ya operating system.
Onbooy scan hutumika sana kuondoa virus kwenye mashine . Hata trial version tu hutosha kuondoa virusi kwa njia hii. Lakini siku hizi Bitdefender, kaspersky na baathi ya anntivius AV na Internet Security IS zina option ya kuboot from cd na ikaanza kuondoa infections pia.
Nawashauri mtumia MALWAREBYTE pamoja na AV au IS zenu ili muwe salama zaidi. Pia baada ya installation ni vizuri ukafanya settings kidogo kwenye SCHEDULES hasa ya kuscan ili ifanye hivyo walau mara moja kwa wiki Kulingana na mazingira hatarishi ya komputa yako ulipo.