Wezi wananifilisi

Hapo inabidi uingie mwenyewe mzigo na wati wako kadhaa mkikamata mmoja mmtolee mfano na onyo ili wenzie wakisikia na kuona wakae mbali na hiyo bustani
Nimefanya hivyo mara kadhaa ila sikufanikiwa
 
Samahani mkuu,naweza kumpata huyo mzee?
Huyo mzee sio mganga kwahiyo hawezi kukupa dawa, ni mfanyabiashara mwenye hardware, mashamba na mifugo. Wala sikumbuki jina lake na hanijui, na sidhani kama unaweza mpigia akakupa msaada au akakubali kuwa ana jambo hilo.

Mimi nimetoa observation tu, mbinu kama hiyo utapata wapi hilo ni nje ya uwezo wangu.
 
Nitafute pm,nitakupa dawa ambayo mtu akiiba si ataacha nyayo? Unaifunika kisha nakuja mimi naitengenezea dawa,huyo mwizi eidha atawehuka,kama sio kufa kabisa
Eneo la tukio kupata nyayo ni ngumu kwakuwa nimefika na kukuta wamevunja mlango na eneo lina nyasi fupi fupi.
 
Sawa mkuu..shukrani kwa wazo lako pia.
 
Simple tu mbona.

Tafuta kijana ambae hajulikani maeneo hayo, panga nae dili kwa makubaliano maalumu.

Kesho yake saa kumi na moja alfajiri, mnafika, anakaa hapo Garden peke yake mpaka mida kama ya saa 12:30 asubuhi.

Ikifika mida ile watu wanaanza kupita kwenda makazini, anajifanya kama hayuko sawa, anazunguka zunguka tu hapo bustanini, kama kuna ufagio anachukua anaanza kufagia fagia.

Watu wakianza kumtilia maanani na kuanza kuongezeka kuona kulikoni, yeye ndio kwaanza azidi kuongeza mbwembwe, ikibidi hata anaanza kuvua nguo.

Watu wakishajaa na kuwa wengi(hii ni kawaida ya mswahili na kumpiga hawawezi) unajitokeza pale mwenye mali, unamuangalia huyo mwizi wako halafu unapiga simu kwa mganga wako(jamaa mwingine uliempanga na wala hayupo mbali)

Ukishapiga simu unaweka loudspeaker, unamwambia mganga tayari mtu kanasa huku.

Basi chap mganga anakuja hata kwa bajaj na vitambaa vyake vyekundu na vyeusi, anafanya fanya dawa pale mpka mwizi wa mchongo anarudiwa na fahamu mnampakia kwenye bajaj haooooo unaenda kuwalipa hela yao mbele kwa mbele.

Tazama hii video mtangazaji wa itv alivyotuletea tangazo la dawa ya kukamata wezi.

View: https://youtu.be/m1fhoU_pbTg?si=Pc5BywrRA2-d1fFz
 
😁😁shukrani,nitajaribu kufanya hili nalo nione matokeo yake
 
KUNA WAHUNI PALE MWANZA MIAKA HIYO ILEMELA, KUNA MUUZA MKAA ALIIBIWA SIMU NI MUHA AKATANGAZA JAMANI ALIENIIBIA SIMU YANGU ARUDISHE MATEJA WAKACHUNA, ALASEMA HAYA WAKUU, AISEEE ILE SIMU ILIANZA KUITA TUMBONI KWA MDAU MMOJA TEJA, AKACHUKUA KISU ILI ATOBOE TUMBO AITOE, PARAPANDA ITALIA PARAPANDA TUMLAKI BWANA YESU MAWINGUNI,,, KWISHAAAA
 
Hahaha..ningepata mtu kazi mwenye dawa hiyo ingekuwa vyema sana
 
Tafadhali naomba unijulishe wapi- huko dar -nitapata ving'ora vya solar.
Namba yao ya simu-kama unaweza kuipata
 
Ajiri Wamaasai wawili hao hawana bei ,ukiandaa bajeti ya "Shuka 10 za kimaasai" aka KIlo moja aka Jiwe aka Box kwa mwezi kila mmoja anachukua.
 
Sure mkuu Kuna wataalam wanatengeneza mpaka nyoka anakuwa mlinzi wa eneo Hilo akiingia mhalifu anaee! Ila sasa kuwapata wataalam wa namna hiyo ni mbinde kwa sasa wamejaa matapeli mpaka ufanikishe unaweza jikuta umeliwa pesa nyingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…