Buguruni kumekuwa na vijiwe vya kufanyia mipango ya uharifu na polisi wanajua na wanalinda vijiwe hivyo.
Kijiwe maarufu kinaitwa kwa Zero. Pale kwa Zero ni barabarani tu, hakuna choo, jiko la kupikia wala sehemu maalum ya kukaa wateja.
Sehemu hiyo hufunguliwa kila siku usiku tu na kukesha mpaka alfajiri kama vile night club.
Pale pamekuwa kijiwe maarufu cha kupanga uhalifu na pahala pekee pa kujipatia huduma muhimu kama bangi, unga, madada poa na mabwabwa.
Polisi kituo kikuu cha Buguruni kipo mita mbili tu kutokea pale lakini wala hawajishugulishi na uhalifu unaopangiwa pale.
Hii mipango yote kama ya hawa mabwana waliokamatwa huwa inapangiwa palepale huku wakijiliwaza kwa kiroba na mrungi na bangi mpaka kunapambazuka wanaanza kuwashambulia wapita njia hasa waki na mama wanaodamkia kwenye mihanjo yao na kuwanyanganya pochi na simu zao.
Polisi hivi intelijensia yenu ni kuzuia maandamano ya wapinzani tu?
Siku zote kumbuka "prevention is much better than cure"