Wezi kutoka Kenya na Ujerumani

Wezi kutoka Kenya na Ujerumani

Wacha1

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2009
Posts
16,676
Reaction score
8,246
Daily News

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, itatoa zawadi nono na fedha taslimu Sh milioni 5 kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa kijana James Mabakuri (22), anayetuhumiwa kumuua mke wa Balozi mstaafu Andrew Daraja.

Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa mtoa taarifa huyo atalindwa na kuhakikishiwa usalama wake baada ya kutoa taarifa.

Kijana huyo anatuhumiwa kumuua Anna Mbago (65), mkazi wa Kimara Temboni, kwa kumchoma kisu kifuani na tangu siku ya tukio Polisi inaendelea kumsaka bila mafanikio.

Katika hatua nyingine, Polisi inawashikilia raia wawili wa Kenya na Ujerumani kwa tuhuma za kukutwa na noti bandia zikiwamo dola za Marekani 8,400, euro 9,500 na Sh 680,000.

Tukio hilo lilitokea juzi jioni Msasani Mwisho, Kinondoni na watuhumiwa hao ni Arne Kipper(30) wa Ujerumani na raia wawili wa Kenya waliotambuliwa kwa jina moja moja la Reuben na Yego, wote wakiwa na umri wa miaka 36.


Fedha hizo zilikamatwa baada ya upekuzi uliofanywa katika gari namba T 727 BAK aina ya Toyota Cresta ya raia huyo wa Ujerumani na Polisi inaendelea na uchunguzi zaidi ili kufahamu mtandao wa watuhumiwa hao.

Pia aliwahadharisha wananchi kuwa makini na fedha zinazotolewa kutokana na kuwapo nyingi bandia badala ya kuziamini zaidi za nje kwa madai kwamba haziwezi kuwamo za bandia.

Utajiri wa haraka haraka.
 
Hii mijitu tunayoenda kuungano nayo ni mijizi.
Lakini viongozi wetu ndio wameshupaa kwelikweli tuungane, sasa huku ni nini kama sio kuongeza wimbi la uhalifu na hofu kwa raia wema.
 
Back
Top Bottom