Wewe zitto wewe!!!! Ohooooooo!!!

Cathode Rays

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
1,738
Reaction score
1,495
Wewe bwana mudogo najua iko humu JF wewe,

Haya mambo yako ya uchokonozi haya wewe mtoto sio mazuri,

Unajua kabisa kuwa sasa hivi watu tuko kwenye puresha ndani ya kyama yetu ya Mabinuzi lakini bado unaleta masikhara na chokochoko....Eeeehh, kwani ungesubiri tumalize Dodoma ukaja bunge lijalo ungekufa we mutoto au ndiyo sifa za damu changa

Ulituchokoaaaaaaaa wakati ule tukakutoa nje ya bunge tukafikiri umejifunza, masikini we aaah wapi kumbe tulikuwa tunapigia mbuzi gitaa na kumuuliza hii ni ala gani,

Ukaja katikati hapo na chokochoko tena mpaka ukasababisha watu wamekanda unga wao wa ngano tayari kuanza kupiga machapati ukatia shubiri, watu wakashindwa kabisa kula na vikawa haviliki kwa utulivu mtoto wewe ulivyo hasidi

Haya ona sasa tena unakuja na machokochoko mengine ya Uswisi........

Hivi kwanza we mtoto, hivi ni nani anaekupa hilo jiti la kutuchokolea watu....eeeeh, nauliza ni nani huyo we mtoto...jibu sio unanitolea macho hapa

Kwanza umeonaje Uswisi kuwa tumeweka hayo unayoita mabilioni????

Wenzako tumejitutumua tukajidundulizia kidogo kidogo angalau siku tukistaafu tusiwe omba omba we unasema tumeiba

Halafu tumedundulizia nje kwa sababu hapa ndani mwanetu ni vigumu kudunduliza,

Ukipinda huku mama yako akishaona unadunduliza anavililia hivyo vijisenti, ooh, mara kitenge cha bibi, mara babu mgonjwa n.k. ndiyo maana mwanetu tumeona tujidundulizie nje....angalau ukiziweka huko zinatulia tuliiiiiiii mwanangu....Hapa ndani tutapata ushawishi wa kuzitumia na tutashindwa kujitunza tukizeeka mwanetu

Halafu pia si unajua hawa manani hii wale ambao huwa wanatupa kampani wale.....eeeh, najua umeshawafahamu.....hawa huwa hawana adabu hata kidogo hawa kijana wangu.....umekutana nae siku ya kwanza hata hamjafahamiana vizuri kaomba laptop....mara ukijipinda hata kabla hujapinduka sawasawa anaomba ka Honda CRV....Ndo maana tunaona bora hata tudundulizie Uswizi maana akikubishia sana unampa kadi ya ATM na namba ya Siri akaangalie salio mwenyewe.....................Ndiyo sababu tunadundulizia Uswizi we mtoto na inatia huzuni hujatuuliza kwanza wazee wako tukuambie kwa nini tunadundulizia huko umalipuka tu ghafla

Anyway, hili nalo ni upepo tu limekuja na litapita hilooooooooo tukirudi bunge lijalo hakuna mtu anakumbuka tena!!!!! Tutapumua tu na tutaendelea na kudunduliza tena safari hii Visiwa vya Faroe na kule kwingine kule sijui ndo wanaita Bermuda kule...

Na ukiendelea na chokochoko zako tutaenda kwa Mama Zitto kule Chigoma tumweleze kabisaaaaaa kwamba aongee na mwanae...na tutamwambia kwamba unahitaji Jiko we mtoto...heheeeee.....maana nyie vijana damu zenu moto bila majiko ya kuwapooza hamtulii kabisa....Tena itabidi uchaguliwe hilo JIKO ili, heheeeee, tuwe na uhakika ni speed governor kiwango

Sasa tukishindwa hapo, itabidi, eeeeeeehhh, tuone namna ambavyo hizo chokochoko zako tunavyoweza kuzihamishia India.....tutafikiria zaidi hapo baadae hiyo tiketi yako tukupatie wapi kati ya Mabwe Pande au ki "Mwakyembe" style....

Hahahaaa, haya bwana mdogo, chokochoko hizo chunga sana sie wazee wako bana, jua hili tumeliona kabla hata hujafikiriwa we mtoto


(Loooool, weekend stress management)
 
zitto,lissu,mnyika wanawanyima usingizi mafisadi
 
Hizi mambo ziko na huku pia?.
I thought this was a stress free zone!
 
Huuu mtaa gani huuu kwanza na hisi mtoa mada aja kaguliwa
 
Utaniutani kumbe ndo message sent and delivered.
 
Rekebisha lugha afu ipelekejunako stress
 
Rekebisha lugha afu ipeleke kunako stress
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…