Wewe unayeandaa maharusi utaolewa lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wewe unayeandaa maharusi utaolewa lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 23, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wakati akikimbia kutoka Misri Nabii Mussa alikutana na wachunga wanyama mjini Mediani. Hawa jamaa hawakuwa na busara hata kidogo, na walikuwa wakiwanyanyasa mabinti waliowatangulia kwenye malisho na manywesho ya wanyama. Siku hiyo walikutana na binti za Kuhani wa Mediani na kuanza ubabe wao usio na maana.

  Mussa alikuwa mbavu nyingi, kwa maana alikuwa mrefu na mwenye msuli tosha. Akaona msinitanie; ngumi, makofi na mateke hadi wote wakatimka. Mabinti waliporudi mapema nyumbani hata baba yao alishangaa. Wakamweleza jinsi walivyosaidiwa na mtu mmoja aliyeenda juu kinoma kuwatimua wale wahuni. Mzee akaona huyu atanifaa, akawaagiza wakamwombe aje pale nyumbani nao wakafanya hivyo.

  Kwa kuwa Mussa alikuwa keshafanya soo kule nyumbani, tena soo ya kuua, akaona ni vema aende. Huyu mzee ni Kuhani mwenye utajiri mkubwa, hivyo angeweza kumpa kibarua cha kujikimu kwa siku kadhaa akiwa pale uhamishoni. Akaenda na kweli walielewana sana. Mara moja akaanza kumtumikia.


  Baada ya muda mrefu kiasi chake, Mussa akawa akitamani kurudi kwao. Lakini ili kuendeleza mahusiano, mzee Kuhani alionelea ni bora jasiri huyu amuoe binti yake mmoja. Mabinti wakaandaliwa vema na kungwi maarufu sana aliyeitwa Siphora. Mabinti wakatoka na mashauzi ya kila aina, masaa mengi yalipita wakicheza na kujishaua mbele za Mussa. Baadaye walipiga pozi, Mussa akaulizwa: Umemuona yupi?
  Mussa alijiinua taratibu na kupita kati ya wale mabinti, hadi mwisho alipomkuta Siphora akamshika mkono. “Huyu hapa!”

  Kila mmoja alishtuka pale ukumbini. Hata Siphora mwenyewe hakuamini kilichoelekea kutokea. “Ebo!” Kuhani aling’aka, “huyo siye bi harusi mtarajiwa.”

  Mussa hakubisha: Sawa, ni mwandaaji tu wa maharusi. Lakini ni mwanamama ambaye bila ya shaka ana uzoefu mkubwa kuliko wale anaowaandaa. Hakukuwa na jinsi, akachukua jiko lake na huyoooo… akatokomea nalo.

  Utamaduni huu hauko Mediani pekee, wala hauko katika mtindo huo wa Mediani tu. Tanzania tumekuwa mbele sana kutoa vipaumbele kwa wawekezaji hasa kutoka nje na kuwadharau wawekezaji wa ndani. Pengine mkate kutoka nje hunoga zaidi ya unaopikwa ndani, na Kuhani alimwona Siphora tangu alipokuwa binti mdogo akiomba kazi pale kwake. Hivyo anaona kuwa binti huyu ana haki ya kufanya kazi ileile na palepale maisha yake yote.

  Huku kwetu tunajuana vizuri sana. Tunafikia mahala pa kuambiana “wewe Mbonde unataka kuwekeza nini? Unaujua uwekezaji wewe?” lakini ikija ngozi nyeupe hata aliyo duni kuliko Mbonde itapewa nafasi na maelekezo sahihi. Kisha itaambiwa “waangalie sana mashababi kama huyu Mbonde, watakuharibia.”

  Hivi karibuni nilikwenda kwenye Kampuni inayozalisha vileo. Nilikuwa na makabrasha yote waliyoniagiza ili kufikiria kunidhamini kwenye kipindi cha Televisheni. Dada aliyenipokea alikuwa na ulimi wa kasuku: “Karibu sana. Umekuja na dokumenti yoyote? Iache pale… tutaishughulikia.” Alinionesha trei iliyokosa matunzo kando ya meza yake. Nikamweleza kuwa hiyo haikuwa mara yangu ya kwanza, nilishaelekezwa kuonana na Meneja Uhusiano.

  Kabla sijamaliza kusema alitokea njemba mmoja aliyekwenda kwenye trei ile, akachomoa karatasi moja na bila kuisoma akaiviringishia betri yake ya simu na kuitia mfukoni. Sasa kweli niache dokumenti zangu orijino pale?
  Wakati nikimshangaa huyu njemba (na hasa huyu dada) aliingia mtu aliyeonekana kama Mjapani hivi.

  Dada aliachana na mimi, zikapanda “Good morning” na Mjapani akaomba kuonana na Meneja Uhusiano. Haraka dada yetu alifungua mlango mmoja na kutoa “Welcome” ya motomoto kabisa wakati Mjapani akijitoma ndani.


  Tunawaandaa watu wavune vyetu wakati sisi hatuna haja ya mavuno bali mshahara au posho kutoka kwao. Inawezekana posho hiyo ni kidogo sana kiasi cha kutomtosha huyo muandaaji, hivyo anafanya hadi juhudi binafsi ili waje wengi. Hajui kuwa hapa nchini tupo wengi zaidi.Katika hili sioni tofauti yetu na mwandazi wa harusi za watu asiyetaka kuolewa.


  0713-248943, 0682-078000
   
Loading...