kitororondo
JF-Expert Member
- Jan 17, 2018
- 597
- 710
Amani iwe kwenu wapendwa.
Nimeamua kuwashirikisha jambo hili yumkini kama yupo aliyewahi kupitia hali hii basi anisaidie japo ushauri natokaje katika hili.
Japo nitaeleza kwa kifupi ila mengine ntaendelea kutiririka taratibu.
Ni hivi: Nimekuwa kwenye mahusiano mengi, kipindi cha nyuma na kufikia mwaka 2013 nikazama kwenye penzi la jimama, nahisi ndiyo tatizo likaanzia hapo maana tangu hapo sikupenda wala kuwa na hisia za kimapenzi kwa mwanamke yeyote wa rika langu au aliye mdogo kwangu.
Nikajikuta napenda wanawake walionizidi zaidi ya miaka 10 na kuendelea. Na kwakweli shetani akawa upande wangu; yaani nimekuwa na bahati nao, wakati mwingine sielewi inakuwaje ila nikitokea kumpenda tu mmama yeyote kuna mazingira yanajitengeneza mpaka nikitafakari huwa naona kama kuna mtu pembeni anayehakikisha napata kile ninachokitamani.
Shida wengi nawaacha kwakuwa wana wivu halafu wanapenda mpaka unaependwa unaogopa yaani. Sasa tatizo ni kwamba nataka nioe mwaka huu, tena nipate kabinti kabichi ila kila ninayempata yaani siwezi kuwa naye hata week nishamzingua.
Yaani sijui naonaje; kila atakachofanya naona kero tu yaani nakosaga hata cha kujadili nikikaa nao nakuwa nao tofauti kuanzia mawazo, mtazamo, mipango hata mapendeleo ya vitu mfno wa mavazi, mziki, vyakula, n.k
Sasa nafanyaje kutoka katika mkwamo huu mpaka kuna muda nawaza nitakuwa nimerogwa nini?
Msaada wa mawazo yako tafadhali.
Sent using Jamii Forums mobile app

oa hiyo mijimama iliyokubemenda tu.