ABTWAHILAKILIMALI
Member
- Jan 10, 2015
- 78
- 27
WEWE NI NANI?
Najua utakuwa umeshapata jibu na umesema aaah huyu Bassanga maswali yake banah, sasa kuna kuna mtu ambae hajijui yeye ni nani! Lakini kiukweli hujui wewe ni nani. Hebu jiulize hapo ulipo wewe ni nani, ukipata jibu sahihi basi naamini hapo ndipo maisha yako yatakapoanza kubadilika, watu wote waliobadilisha maisha yao walijitambua wao ni kina nani, na watu wote ambao hawakujitambua wao ni kina nani maisha yao yalikuwa magumu na wamekufa masikini hali ya kuwa walitakiwa kufa matajiri. Wamekufa na vipaji hali ya kuwa walitakiwa kuvitumia duniani. Tatizo sio kuishi, tatizo ni kuishi ukijua wewe ni nani.
Sitaki unijibu kwa sababu naamini kama nikikupa nafasi ya kunijibu wewe ni nani, utanipa majibu haya;
★Mimi ni binadam ★Mimi ni mtu ★Mimi ni Juma ★Mimi ni Hadija ★Mimi ni mwanamke ★Mimi ni mwanaume ★Mimi ni Fundi viatu ★Mimi ni mwalimu Mimi ni muhasibu
Lakini tujiulize majibu haya ni sahihi?
Kiuhalisia huu ni uongo tuliokalilishwa huko nyuma. Eti wewe ni mtu mmmhh unadhani ungezaliwa halafu ukaambiwa wewe ni ng'ombe hadi leo si ungekuwa unajua wewe ni ng'ombe? Hapana huu ni uongo, Mimi Juma ni kweli wewe ni Juma lakini unafikiri leo ukibadilisha dini si unaweza kuitwa Joseph? Kwani unakuwa sio wewe tena? Mimi ni Mwanamke hahahaaaa hebu fikiria ungezalliwa halafu ukaambiwa wewe ni mwanaume ungepinga? Ukasema mimi ni mwanamke kiuhalisia ungekubali hivyo, maana huu ni uongo haya ni majina tu tunapewa na tunayakubali hivyo. Ndio maana leo wapo watu waliambiwa wao ni masikini hadi leo wanajua wao ni masikini wakati waliambiwa uongo.
Wewe ni fundi viatu au Mhasibu, hivi kuna ukweli ndani yake, hebu fikiria siku unasema kuwa sitaki tena kushona viatu, sitaki tena kuwa Muhasibu ndio tuseme unakuwa sio wewe tena?
Mfano mtu akifa utasikia watu wanasema tunaushindikiza mwili wa marehem John naamini wakati huo wewe haupo rafiki hebu jiulize wewe ni nani?
Ukiangalia kwa undani kabisa utaona tafsiri zote hizo tunazozijua ni tafsiri tulizoambiwa huko nyuma, na sio uhalisia, ndio maana leo mtu akifukuzwa kazi anataka kufa kwa presha, kwanini hajui yeye ni nani?
Mtu yuko radhi kufanya kazi ambayo haipendi kwa sababu aendeshe maisha yake tu, kwa sababu baba yake alishamwambia urithi wake ni elimu na ajira hivyo ndivyo anavyojua hajui yeye ni nani. Ndio maana anashinda kwa waganga apandishwe vyeo, huu ni ujinga.
Hebu fikiria leo anakuja mtu anakwambia wewe mwanamke nini? Wakati anakuona kabisa una jinsia ya kiume, Hili linakuwa kama tusi kubwa sana kwako na hapa panaweza kutokea ugomvi mkubwa sana lakini kiukweli jiulize ni kweli wewe ni mwanamke? Ukilijua hilo huwezi kugombana. Ukikijua kile utaishi kwa amani sana.
Mtoto anapozaliwa huwa anazaliwa amekunja mikono maana kuna kitu ambacho amekuja nacho duniani kama karama (kipaji) amekabidhiwa na Mungu hiyo ndio humtambulisha yeye ni nani na mtu anapokufa vile vile anakufa akiwa amefungua mikono maana kile alichokuja nacho duniani tayali amekiacha duniani.
Sasa kuna watu wanazaliwa wamekunja mikono na wanakufa wamekunja mikono, maana kwamba alikabidhiwa Karama kuja kuiacha duniani na anarudi nayo kwa Mungu hajaitumia wala hajaiacha duniani, sasa sijui unaipeleka wapi na ukiulizwa kwanini umerudi nayo sijui utajibu nini?
Rafiki kaa chini jiulize wewe ni nani? Ukijua wewe ni nani huwezi kufanya vitu kwa sababu fulani yupo, kwa sababu akuone, huwezi kushindwa kufanya kitu eti kwa sababu fulani hayupo.
Ukipata jibu anza, ukikosa jibu NITAFUTE
Action= SUCCESS

Last edited by a moderator: