Wasalaam Jf.
Wewe ni nani?
Nafsi ni nini?
Tunazielewa vyema dhana hizo, jambo la msingi ninalopenda kushare na ninyi ni kuishi kwa uhalisia, kuishi wewe kama wewe, kuna maumbo mawili hapo, umbo la kwanza ni wewe nafsi, na umbo la pili ni wewe mwili na namna unavyojiwasilisha katika dunia ya kawaida. Umbo nafsi linaposhaabiana na umbo mwili hapo tutasema unaishi uhalisia lakini yanapotofautiana kwa lugha nyepesi tutasema unaigiza na panaweza kuibuka na unafiki mfano unapoonyesha una furaha ambayo kinafsia unajua humaanishi, kuonyesha kuwa una pesa na tajiri ki uhalisia sivyo hayo ni maigizo na unafiki.
Hivyo kuna hasara nyingi ambazo unaweza kuzipata kwa kutoishi katika uhalisia wako kama vile maumivu ya mda mrefu kimwili na kiakiri kutokana na kuishi maisha ambayo sio yako, kutojiamini kwa kuwa hujikubali n.k.
Kwa upande mwingine kuna faida nyingi za kuishi katika uhalisia wako kama vile maendeleo binafsi kwa kujikubali na kufanyia kazi mapungufu yako n.k.
Nawasilisha.