Wewe ndio unachagua ufanikiwe au usifanikiwe?

Wewe ndio unachagua ufanikiwe au usifanikiwe?

mchonjoya

Member
Joined
Aug 17, 2016
Posts
81
Reaction score
200
Habari members wote,

Kila mtu anaitaji mafanikio katika maisha yake. Ili kufanikiwa lazima upange na kuchagua, na kuchagua ni maamzi ya kila mmoja wetu. Uchague kufanikiwa au kutofanikiwa, kwa kutozingatia mambo haya muhimu;
1. Mungu
2. Uwaminifu
3. Muda

Mungu - Bila Mungu hakuna chochote, Mungu (imana) ndo kila kitu. Kila mtu anaamini na anachoamini kuwa na imani kwa kile unachokifanya kunakufanya ujenge imani katika kukifanya kwa kuamini kitaleta tija siku za mbeleni.

Kujenga imana huko ndio kunakufanya uongeze bidii kukifanya kitu hiko kwa nguvu zote kwa sababu ndani yake umeweka tumaini la kufanikisha. Kukosa umani ni kukosa tumaini.

Uwaminifu - Ni njia ya kuyaendea mafanikio, kwa sababu hakuna aliyefanikiwa akiwa mwenyewe. Ili ufanikiwe lazima utafanya kazi na wengine, na ili watu wafanye kazi na wewe itakulazimu ujenge uwaminifu. Kukosa uwaminifu jua unayafanya maisha yako kuwa magumu na hautafanikiwa.
Uwaminifu ni utajiri, uaminifu ni mafanikio

Muda - Muda ndio dira ya kila kitu. Hata maagano ya wewe na Mungu wako ni muhimu kuzingatia muda. Kuna muda wa kuabudu, kufanya kazi na kulala, vyote hufanywa kwa kuzingatia muda. Ukikosa kuzingatia muda katika mambo yako utafeli, kwakuwa utafanya vitu nje ya muda. Huwezi kufanya kazi yoyote nje, chochote ukifanya nje ya muda hakiwezi kuwa na fanida.

Muda ni mali, dili, kiongozi sahihi, na pasipo kujali muda huwezi kufanikiwa.

Mafanikio yetu yapo ndani ya muda wetu.

Sent from my F-02H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom