Wewe mzuri? Jifunze kuheshimu wengine

Wewe mzuri? Jifunze kuheshimu wengine

mwanawao

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2010
Posts
3,235
Reaction score
5,919
Binadamu tumekuwa na tabia za kibinafsi sana siku hizi za kudharau wengine. Huwa ninasikitishwa sana na comments za watu pale wanapowadharau wenzao haswa kuhusu suala la maumbile yao.Unakuta mtu anaanza kumkejeli binti ni 'Mbaya' sura kama 'Ndimu'? Hivi unafikiri yeye ndo alijiumba mwenyewe hvyo? Angekuwa na uwezo wa kujiumba unafikiri asingejiumba kama ulimwengu unavyopenda awe? Eti huyu mdada miguu kama fito.

Angejiumba si angejitengenezea liguu kama Tembo kabisa ili mfurahii. Ooh! Huyu mkaka sura mbaya sana tena kafupi hawezi pata mdada, kwani alipenda awe hvyo? Wengine wamefikia hata hatua ya kudharauliana maumbile yao ya ndani, yule mdada rambo, mtaro au maji sana ooh wengine ni maumbile tu hawajapenda kuwa vile. Ooh! Yule mkaka kibamia, hajapenda kuwa vile ni maumbile tu kama Mungu alivyopenda.

Tusimnyanyapae yoyote maana hata wee mzuri, mwenye sura nzuri, mguu wa bia, mrefu, n.k hukujiumba wee hvyo. Ulijikuta tu ukiwa hvyo. Unaweza pata ajali siku yoyote na sura ikageukia kisogoni sijui utamringia nani au miguu yote ikakatika sijui huo mguu wa chupa ya bia na urefu wako utakuwa wapi au ukapatwa kisukari na huo mtarimbo doro utamringishia nani? Kila mtu anasehemu yake kwenye jamii kwa hiyo tusimdharau yoyote.

Wadada jiaminini msijichubue, msitumie madawa ya kuongeza kalio, kila mmoja ana uzuri kwa namna yake. Tembea kifua mbele maana kila mtu Mungu amemuumba kwa namna nzuri na tena ya kupendeza sana.

Kuwa natural ndo habari ya mjini, kuwa artificial itakuharibia uzuri wako wa asili!
 
Nenda Celebrity forum, soma Thread inayomuhusu ROMA MKATOLIKI na Star aliyempachika mimba uone jinsi wana JF tulivyo na roho mbaya!
 
Nenda Celebrity forum, soma Thread inayomuhusu ROMA MKATOLIKI na Star aliyempachika mimba uone jinsi wana JF tulivyo na roho mbaya!

Watu wana roho mbaya sana. Wengi hawajui tofauti zetu za kimaumbile ndo zinafanya ulimwengu huu upendeze. Inasikitisha sana..
 
Mawazo yako ni mazuri, ila akili za watu zimegeukia kiunoni sikuizi
 
Kweli hiyo tabia baadhi ya watu wengi wanayo,au utasikia mtu anasema yule kila kitu chake kizuri ila viji guu tuuu ndio mashaka..
 
Nenda Celebrity forum, soma Thread inayomuhusu ROMA MKATOLIKI na Star aliyempachika mimba uone jinsi wana JF tulivyo na roho mbaya!

Halafu ni wanawake wenye kumponda mwanamke mwenzao...

Kuna wanadamu ni watu wa ajabu mno...

Ajabu ni kwamba hao wanaoponda wenzao hata ukimpa kalamu na karatasi halafu umwambie amchore mtu anayeona ni mzuri hawezi...
 
Na wengi wanaoponda hawana watoto, sasa sijui wanajisahau vipi wakati hawajafahamu watazaa kitu cha aina gani, wakizaa stuli cjui watamlaumu nani.
 
Sielewi kwa nini wanawake hawapendani. Na ukimwangalia anayemponda mwingine unaweza kuta wanafanana tu hamna tofauti yyte
 
Na wengi wanaoponda hawana watoto, sasa sijui wanajisahau vipi wakati hawajafahamu watazaa kitu cha aina gani, wakizaa stuli cjui watamlaumu nani.

Siku akizaa hiyo stuli ndo atafurahi haswa.... na Mungu hachelewi kukupa sawa sawa na kebehi unazotoa kwa wengine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom