Werema, Maswi, Mboma wapumulia mashine

Werema, Maswi, Mboma wapumulia mashine

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,247
Reaction score
25,191
Zitto-Kabwe-November18-2014.jpg

Kamati ya Zitto yakabidhiwa ripoti, kuwahoji

Naibu Spika wa Bunge,Job Ndungai (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati za Bunge ya Hesabu za Serikalin (PAC),Zitto Kabwe (katikati) na makamu wake,Deo Fllikunjombe Ripoti Uchunguzi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika ofisi za Bunge mjini Dodoma jana.PICHA:OMAR FUNGO

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inatarajia kuwahoji Mwanasheria Mkuu (AG), Jaji Frederick Werema, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Robert Mboma na wengine waliotajwa katika kashfa ya kuchotwa Sh. bilioni 306 ya akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Hatua hiyo imekuja baada ya kamati hiyo kukabidhiwa ripoti ya ukaguzi wa hesabu za akaunti hiyo na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai jana ili kuifanyia uchambuzi na kutoa mapendekezo.

Ukaguzi wa hesabu na uchunguzi huo vilifanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru).

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimkabidhi Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, ripoti hizo, katika Ofisi za Bunge, mjini hapa jana.Waliokuwapo katika makabidhiano hayo ni Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo

Filikunjombe na wajumbe wa kamati hiyo; Ally Keissy (Nkasi Kaskazini-CCM), Kombo Khamis Kombo (Mgogoni-CUF) na Ismail Aden Rage
(Tabora Mjini-CCM).

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah.Akikabidhi ripoti hiyo, Ndugai aliitaka PAC kuifanyia uchambuzi na kutoa mapendekezo.

Hata hivyo, aliitaka ihakikishe inajikita katika kutumia ushauri uliotolewa na CAG na Takukuru katika kutoa mapendekezo kwa sababu waliwahoji wahusika wote.”Baada ya kukamilisha kazi, taarifa irudi kwangu ili kujiridhisha kabla ya kuiwasilisha bungeni,” alisema Ndugai.

Baada ya kupokea ripoti hiyo, Zitto akihojiwa na waandishi wa habari, alisema wa kwanza kuhojiwa na kamati yake atakuwa ni CAG.Zitto alisema kwamba na kwamba kamati itafanya kazi iliyokabidhiwa na Ofisi ya Spika kwa siri.

Alisema watafanya kazi hiyo kwa siri kwa kuwa ndani ya suala hilo kuna mambo ya mahakama, hivyo wanaepuka kuingia katika malalamiko hapo baadaye ya mtu kuonewa na kwamba, watahakikisha wanatenda haki.

Naye Filikunjombe alisema kamati yake ina uwezo mkubwa wa kumaliza kazi hiyo ndani ya siku 10, kuanzia sasa kwa kuwa kazi kubwa
imekwisha kufanywa na CAG.

IPTL WANENA
Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imesema itatoa ushirikiano kwa Bunge pindi watakapohitajika kufanya hivyo.IPTL ilisema hayo kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Meneja Uhusiano wake, Sylvester Joseph, mjini hapa jana.

"Kwa niaba ya mwenyekiti wa Kampuni za IPTL na PAP, tunaahidi kutoa ushirikiano kwa kamati ili ifanye kazi yake vizuri kama tulivyotoa
ushirikiano tangu uchunguzi ulivyoanza,” ilieleza taarifa hiyo ya IPTL.

Iliongeza: “Tunachoomba ni kwamba, kamati ifanye kazi yake kwa uadilifu ili suala hili liishe na tuweze kujikita sasa katika kuzalisha umeme kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania.”

Juzi tulisikia watu wakisema kuwa ripoti imetoka na baadhi ya vyombo vya habari hata kwenye mitandao ya kijamii kuwa ripoti hii imetoka...hatujui wapi ripoti hiyo ilitoka, ila tunataka umma ujue kuwa sasa ndiyo ripoti imekabidhiwa.”

Kashfa ya Tegeta Escrow iliibuliwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.Kuibuliwa kwa kashfa hiyo, kulisababisha Kafulila kuingia kwenye malumbano makali yaliyowafikisha katika kutoleana maneno ya dharau na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, bungeni.

Maneno hayo ya dharau yalihusisha Jaji Werema kumwita Kafulila kuwa ni tumbili na Kafulila kumwita Jaji Werema mwizi.Baadhi ya wabunge wamekuwa wakishinikiza wakitaka ripoti hiyo pamoja na ile ya uchunguzi uliofanywa na Takukuru ziwasilishwe bungeni ili zikajadiliwe na wabunge ili ukweli ujulikane.

Tayari nchi wahisani zimetangaza kuikatia misaada serikali ya zaidi ya Sh. trilioni 1 kutokana na kashfa hiyo.Akaunti ya Tegeta Escrow ilifunguliwa kutokana na kutoelewana kuhusu gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na kampuni ya kufua umeme ya IPTL na kuuzwa Tanesco.

Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID), katika uamuzi wake wa Februari 2014, ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa
kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL.

Kwa uamuzi huo, ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye akaunti ya Escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali, lakini badala yake fedha hizo zilitoweka ghafla kwenye akaunti hiyo.

KILICHOMO KATIKA RIPOTI YA CAG
Matokeo ya ukaguzi uliofanywa na CAG kuhusiana na kuchotwa kwa Sh. bilioni 306 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow yameiweka matatani Ofisi ya Mwananasheria Mkuu wa Serikali (AG), huku yakizitambua fedha hizo kuwa ni za umma.

Vyanzo vyetu mbalimbali vimebainisha kuwa Ofisi ya AG inadaiwa kuingia matatani, baada ya ripoti ya ukaguzi huo iliyovuja, kubaini kwamba, inahusika moja kwa moja katika kuisababishia serikali hasara ya jumla ya Sh. bilioni 321 katika kashfa hiyo.

Pia Wizara ya Nishati na Madini, nayo pia inatajwa na ripoti hiyo kuhusika katika kuisababishia serikali hasara hiyo.

Vilevile, Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) nayo pia imeingia matatani, baada ya kuhusishwa na ripoti hiyo kwa tuhuma za kulikosesha shirika hilo kiasi hicho cha fedha.

Ofisi ya AG inahusishwa na kashfa hiyo, baada ya ripoti hiyo kueleza kuwa ilivunja sheria makusudi kwa kuelekeza kuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye gharama za uendeshaji (capacity charges), ambazo Tanesco walilipishwa na IPTL, isilipwe.

Maelekezo hayo ya ofisi ya AG yanadaiwa kusababisha serikali kupoteza mapato ya Sh. bilioni 21.

Aidha, wizara ya Nishati na Madini inaguswa na taarifa hiyo kwamba ilisaini nyaraka kuidhinisha kutolewa fedha hizo kwenye akaunti hiyo bila kuhakikisha fedha za Tanesco zinarudi.

Hatua hiyo ya wizara hiyo inadaiwa kuipotezea Tanesco kiasi hicho cha fedha.

Nayo Bodi Tanesco inaguswa katika kashfa hiyo kwa madai kwamba, haikutimiza wajibu wake kwa kugeuza maamuzi yake na hivyo kulikosesha shirika kiasi hicho cha fedha.
Ripoti ya CAG inaigusa Bodi hiyo isisema kwamba iligeuza maamuzi yake ama kwa kushinikizwa na wizara au kwa rushwa.

Ripoti hiyo imebainisha pia kuwa Wizara ya Nishati na Madini haikujiridhisha kuhusu uhalali wa umiliki wa IPTL.

Pia imebaini kuwa Kampuni ya PAP haikununua kihalali asilimia 70 ya hisa za kampuni ya Mechmar katika IPTL kwa madai kwamba, zilizuiwa na mahakama.
Vilevile, imebaini kuwa kampuni hiyo (Mechmar) hawana hati halisi za hisa (share certificates).

Ripoti hiyo imebainisha pia kuwa PAP ilifanya udanganyifu mkubwa katika malipo ya kodi kwa kutoa nyaraka za uongo kuwa walionunua hisa kwa Sh. milioni sita, badala ya Dola za Marekani milioni 20 na kuikosesha serikali mapato ya Sh. bilioni 8.7.

Inabainisha kuwa fedha zilizokuwamo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, ambazo ni jumla ya Sh. bilioni 306 ni matokeo ya Tanesco kulipishwa gharama za uendeshaji zaidi ya kiwango kinachotakiwa kulipwa.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa Tanesco walipaswa kurejeshewa Sh. bilioni 321 zilizolipwa ziada kwa IPTL kati ya mwaka 2002-2012.

Hivyo, fedha za akaunti ya Tegeta Escrow ni fedha za umma na kwamba, yote ilipaswa kurudi Tanesco na shirika kuendelea kuwadai IPTL Sh. bilioni 15

CHANZO: NIPASHE
 
Hawa wakurya hawana akili kabisa, wamewashushia heshima watu wa Musoma sana hasa werema na Maswi, Mkoa wa Mara haujawahi kupata viongozi wajinga kama hawa toka nchi ipate uhuru. Nyabafu zao.
 
Ndugai aliitaka PAC kuifanyia uchambuzi na kutoa mapendekezo.

Hata hivyo, aliitaka ihakikishe inajikita katika kutumia ushauri uliotolewa na CAG na Takukuru katika kutoa mapendekezo kwa sababu waliwahoji wahusika wote."Baada ya kukamilisha kazi, taarifa irudi kwangu ili kujiridhisha kabla ya kuiwasilisha bungeni," alisema Ndugai.

Haya ya kuwataja watuhumiwa ni utashi finyu na kupenyeza hoja za kisiasa, kinachofanywa na kamati ya Zitto ni Ndugai alichoagiza.

Pinda must Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imesema itatoa ushirikiano kwa Bunge pindi watakapohitajika kufanya hivyo.IPTL ilisema hayo kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Meneja Uhusiano wake, Sylvester Joseph, mjini hapa jana.

"Kwa niaba ya mwenyekiti wa Kampuni za IPTL na PAP, tunaahidi kutoa ushirikiano kwa kamati ili ifanye kazi yake vizuri kama tulivyotoa
ushirikiano tangu uchunguzi ulivyoanza," ilieleza taarifa hiyo ya IPTL.

Iliongeza: "Tunachoomba ni kwamba, kamati ifanye kazi yake kwa uadilifu ili suala hili liishe na tuweze kujikita sasa katika kuzalisha umeme kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania."

Juzi tulisikia watu wakisema kuwa ripoti imetoka na baadhi ya vyombo vya habari hata kwenye mitandao ya kijamii kuwa ripoti hii imetoka...hatujui wapi ripoti hiyo ilitoka, ila tunataka umma ujue kuwa sasa ndiyo ripoti imekabidhiwa."

Haya mambo ya kuita watu wezi wakati wote tunaona ripoti ndio inakabidhiwa ni ushabiki tu, kushabikia usichokijua.
 
Hawa jamaa waliohusika wataishia kupoteza kazi tu,jela haiwahusu kabisa.
Hii ya kuwaachisha kazi halafu wanaachwa kuendelea kutumbua fedha walizoiba mpaka vitukuu haikubariki. Kila mtu sharti avune alichopanda.
 
Msukule wa fisadi Lowasa
Mkuu salama............Pinda ana siku 10 kama waziri mkuu, mtoto wa mkulima aliingia mjini na issue ya kufuga nyuki baada ya kuona biashara ya asali hailipi akaamua apige dili kupitia IPTL......Pinda must Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
 
Tatizo hii nchi bana hapa utaona hii mijizi inatajwa live bila chenga ila itachoropoka hivi hivi.
 
Zitto-Kabwe-November18-2014.jpg

Kamati ya Zitto yakabidhiwa ripoti, kuwahoji

Naibu Spika wa Bunge,Job Ndungai (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati za Bunge ya Hesabu za Serikalin (PAC),Zitto Kabwe (katikati) na makamu wake,Deo Fllikunjombe Ripoti Uchunguzi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) katika akaunti ya Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) katika ofisi za Bunge mjini Dodoma jana.PICHA:OMAR FUNGO

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) inatarajia kuwahoji Mwanasheria Mkuu (AG), Jaji Frederick Werema, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Robert Mboma na wengine waliotajwa katika kashfa ya kuchotwa Sh. bilioni 306 ya akaunti ya Tegeta Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Hatua hiyo imekuja baada ya kamati hiyo kukabidhiwa ripoti ya ukaguzi wa hesabu za akaunti hiyo na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai jana ili kuifanyia uchambuzi na kutoa mapendekezo.

Ukaguzi wa hesabu na uchunguzi huo vilifanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru).

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimkabidhi Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, ripoti hizo, katika Ofisi za Bunge, mjini hapa jana.Waliokuwapo katika makabidhiano hayo ni Makamu Mwenyekiti wa PAC, Deo

Filikunjombe na wajumbe wa kamati hiyo; Ally Keissy (Nkasi Kaskazini-CCM), Kombo Khamis Kombo (Mgogoni-CUF) na Ismail Aden Rage
(Tabora Mjini-CCM).

Wengine ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, na Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah.Akikabidhi ripoti hiyo, Ndugai aliitaka PAC kuifanyia uchambuzi na kutoa mapendekezo.

Hata hivyo, aliitaka ihakikishe inajikita katika kutumia ushauri uliotolewa na CAG na Takukuru katika kutoa mapendekezo kwa sababu waliwahoji wahusika wote."Baada ya kukamilisha kazi, taarifa irudi kwangu ili kujiridhisha kabla ya kuiwasilisha bungeni," alisema Ndugai.

Baada ya kupokea ripoti hiyo, Zitto akihojiwa na waandishi wa habari, alisema wa kwanza kuhojiwa na kamati yake atakuwa ni CAG.Zitto alisema kwamba na kwamba kamati itafanya kazi iliyokabidhiwa na Ofisi ya Spika kwa siri.

Alisema watafanya kazi hiyo kwa siri kwa kuwa ndani ya suala hilo kuna mambo ya mahakama, hivyo wanaepuka kuingia katika malalamiko hapo baadaye ya mtu kuonewa na kwamba, watahakikisha wanatenda haki.

Naye Filikunjombe alisema kamati yake ina uwezo mkubwa wa kumaliza kazi hiyo ndani ya siku 10, kuanzia sasa kwa kuwa kazi kubwa
imekwisha kufanywa na CAG.

IPTL WANENA
Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) imesema itatoa ushirikiano kwa Bunge pindi watakapohitajika kufanya hivyo.IPTL ilisema hayo kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Meneja Uhusiano wake, Sylvester Joseph, mjini hapa jana.

"Kwa niaba ya mwenyekiti wa Kampuni za IPTL na PAP, tunaahidi kutoa ushirikiano kwa kamati ili ifanye kazi yake vizuri kama tulivyotoa
ushirikiano tangu uchunguzi ulivyoanza," ilieleza taarifa hiyo ya IPTL.

Iliongeza:
"Tunachoomba ni kwamba, kamati ifanye kazi yake kwa uadilifu ili suala hili liishe na tuweze kujikita sasa katika kuzalisha umeme kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania."

Juzi tulisikia watu wakisema kuwa ripoti imetoka na baadhi ya vyombo vya habari hata kwenye mitandao ya kijamii kuwa ripoti hii imetoka...hatujui wapi ripoti hiyo ilitoka, ila tunataka umma ujue kuwa sasa ndiyo ripoti imekabidhiwa."

Kashfa ya Tegeta Escrow iliibuliwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila.Kuibuliwa kwa kashfa hiyo, kulisababisha Kafulila kuingia kwenye malumbano makali yaliyowafikisha katika kutoleana maneno ya dharau na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema, bungeni.

Maneno hayo ya dharau yalihusisha Jaji Werema kumwita Kafulila kuwa ni tumbili na Kafulila kumwita Jaji Werema mwizi.Baadhi ya wabunge wamekuwa wakishinikiza wakitaka ripoti hiyo pamoja na ile ya uchunguzi uliofanywa na Takukuru ziwasilishwe bungeni ili zikajadiliwe na wabunge ili ukweli ujulikane.

Tayari nchi wahisani zimetangaza kuikatia misaada serikali ya zaidi ya Sh. trilioni 1 kutokana na kashfa hiyo.Akaunti ya Tegeta Escrow ilifunguliwa kutokana na kutoelewana kuhusu gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na kampuni ya kufua umeme ya IPTL na kuuzwa Tanesco.

Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID), katika uamuzi wake wa Februari 2014, ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa
kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL.

Kwa uamuzi huo, ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye akaunti ya Escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali, lakini badala yake fedha hizo zilitoweka ghafla kwenye akaunti hiyo.

KILICHOMO KATIKA RIPOTI YA CAG
Matokeo ya ukaguzi uliofanywa na CAG kuhusiana na kuchotwa kwa Sh. bilioni 306 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow yameiweka matatani Ofisi ya Mwananasheria Mkuu wa Serikali (AG), huku yakizitambua fedha hizo kuwa ni za umma.

Vyanzo vyetu mbalimbali vimebainisha kuwa Ofisi ya AG inadaiwa kuingia matatani, baada ya ripoti ya ukaguzi huo iliyovuja, kubaini kwamba, inahusika moja kwa moja katika kuisababishia serikali hasara ya jumla ya Sh. bilioni 321 katika kashfa hiyo.

Pia Wizara ya Nishati na Madini, nayo pia inatajwa na ripoti hiyo kuhusika katika kuisababishia serikali hasara hiyo.

Vilevile, Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) nayo pia imeingia matatani, baada ya kuhusishwa na ripoti hiyo kwa tuhuma za kulikosesha shirika hilo kiasi hicho cha fedha.

Ofisi ya AG inahusishwa na kashfa hiyo, baada ya ripoti hiyo kueleza kuwa ilivunja sheria makusudi kwa kuelekeza kuwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye gharama za uendeshaji (capacity charges), ambazo Tanesco walilipishwa na IPTL, isilipwe.

Maelekezo hayo ya ofisi ya AG yanadaiwa kusababisha serikali kupoteza mapato ya Sh. bilioni 21.

Aidha, wizara ya Nishati na Madini inaguswa na taarifa hiyo kwamba ilisaini nyaraka kuidhinisha kutolewa fedha hizo kwenye akaunti hiyo bila kuhakikisha fedha za Tanesco zinarudi.

Hatua hiyo ya wizara hiyo inadaiwa kuipotezea Tanesco kiasi hicho cha fedha.

Nayo Bodi Tanesco inaguswa katika kashfa hiyo kwa madai kwamba, haikutimiza wajibu wake kwa kugeuza maamuzi yake na hivyo kulikosesha shirika kiasi hicho cha fedha.
Ripoti ya CAG inaigusa Bodi hiyo isisema kwamba iligeuza maamuzi yake ama kwa kushinikizwa na wizara au kwa rushwa.

Ripoti hiyo imebainisha pia kuwa Wizara ya Nishati na Madini haikujiridhisha kuhusu uhalali wa umiliki wa IPTL.

Pia imebaini kuwa Kampuni ya PAP haikununua kihalali asilimia 70 ya hisa za kampuni ya Mechmar katika IPTL kwa madai kwamba, zilizuiwa na mahakama.
Vilevile, imebaini kuwa kampuni hiyo (Mechmar) hawana hati halisi za hisa (share certificates).

Ripoti hiyo imebainisha pia kuwa PAP ilifanya udanganyifu mkubwa katika malipo ya kodi kwa kutoa nyaraka za uongo kuwa walionunua hisa kwa Sh. milioni sita, badala ya Dola za Marekani milioni 20 na kuikosesha serikali mapato ya Sh. bilioni 8.7.

Inabainisha kuwa fedha zilizokuwamo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow, ambazo ni jumla ya Sh. bilioni 306 ni matokeo ya Tanesco kulipishwa gharama za uendeshaji zaidi ya kiwango kinachotakiwa kulipwa.

Ripoti hiyo inabainisha kuwa Tanesco walipaswa kurejeshewa Sh. bilioni 321 zilizolipwa ziada kwa IPTL kati ya mwaka 2002-2012.

Hivyo, fedha za akaunti ya Tegeta Escrow ni fedha za umma na kwamba, yote ilipaswa kurudi Tanesco na shirika kuendelea kuwadai IPTL Sh. bilioni 15

CHANZO: NIPASHE

Uchumi unaohujumiwa unaweza kukua kweli? Hata ukikua utakuwa dwarf na lazima uwe na matege
 
Hii nchi nikipata chance na mimi nitajichotea na kujilimbikizia mimi na ndugu zangu wote.
 
Nimemuona werema bungeni sijaona kama anamashime ya kupumulia.
 
[h=1]Sakata la IPTL[/h]
Umoja wa Ulaya warejea ukoloni mamboleo
¬ Wasimamisha misaada ya maendeleo
¬ Wasaliti washangilia
¬ Serikali yatakiwa kuyashitaki makampuni na mabenki

UMOJA wa Ulaya kwa pamoja na baadhi ya nchi wanachama wake moja moja zimeamua kusitisha au kusimamisha kwa muda utoaji misaada kwa Tanzania kwa madai kwamba haziridhishwi na mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ndani ya serikali ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Nchi zilizotajwa ni Sweden, Finland, Norway, Marekani na Uingereza. Ni katika nchi hizi mabenki na makampuni ambayo kwa namna moja au nyingine yanahusika katika mgogoro wa ufisadi wa IPTL yana makao makuu yake. Na ni katika nchi hizo kwamba makampuni yaliyoko kwenye mgogoro yalifungua kesi mbalimbali na kudai mabilioni ya fedha dhidi ya kampuni ya VIP Engineering and Marketing na serikali ya Tanzania kuhusu mambo mbalimbali yanayohusiana na mradi wa kufua umeme wa IPTL na hasa suala la akaunti ya ESCROW. Kiasi cha dola za kimarekani milioni 125 zilikuwa zimewekwa katika akaunti ya ESCROW iliopo Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Tumemuona Balozi wa Uingereza akiamsha bendera nyekundu kwa madai kwamba anatetea maslahi ya Benki ya Uingereza ambayo eti ilinunua madeni ya IPTL na hivyo inadai fedha zilizokua zimewekwa kwenye Akaunti ya ESCROW.
Kampuni ya IPTL lilikuwepo siku zote na benki ya Standard Chartered inajua matatizo yote ya ufisadi yaliyoibuliwa katika Mahakama mbalimbali pamoja na ripoti za maofisa wafilisi wa muda wa kampuni ya IPTL hapa nchini. Ikitokea kwamba IPTL na washirika wake wakatiwa hatiani, je kwa vipi Standard Chartered itakwepa mashtaka?

Katika nyakati tofauti Mahakama za Kimataifa na mahakama za kawaida katika nchi za Magharibi zimetoa hukumu na maelekezo kwa kampuni zinazoshitakiana. Baadhi ya maelekezo ya mahakama ya New York ni yale yanayosema kwamba kesi nyingine zingelifunguliwa Tanzania kwa sababu mahakama yake ina uwezo wa kusikiliza mashauri hayo.
Mahakama nyingine Uingereza iliagiza fedha hizo zibaki kwenye akaunti ya ESCROW mpaka mfumo mwafaka wa ukokotoaji utakapopatikana. Hakuna mfumo wa ukokotoaji unaoweza kupatikana nje ya wahusika katika IPTL ambao ni wale walionunua hisa za Mechmar ambayo ilikuwa na asilimia 70% na VIP Engineering and Marketing iliyokuwa na asilimia 30%.
Na hicho ndicho kilichofanyika baada ya PAP ambayo ilinunua hisa za Mechmar katika IPTL kununua hisa za VIP Engineering and Marketing na kukubali kubeba madeni halisi ambayo IPTL itakuwa inadaiwa, kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati 100 kufikia megawati 500 na pia kupunguza bei ya umeme ambao kampuni hiyo inaiuzia TANESCO.
Awali Mahakama za usuluhishi za kimataifa kama ICSD ambapo shauri kati ya TANESCO na IPTL lilipelekwa kufafanuliwa ni kiasi gani IPTL iliwekeza ili kiasi cha capacity charge kieleweke. Uamuzi wa Mahakama hiyo ulimaliza ubishi kati ya TANESCO na IPTL na kuweka kiwango cha malipo ya dola za kimarekani milioni 2.6 na hivyo kuweka wazi kuhusu malipo kwenye akaunti ya ESCROW yanatoka wapi. Kufuatana na nyaraka zilizopo, fedha zote zilizoingizwa kwenye Akaunti ya ESCROW zilitokana na IPTL kuuza umeme TANESCO kwa kiasi kilichokubaliwa.
Jambo ambalo limesababisha hatua hizo kuchukuliwa, zinahusu jinsi fedha zilizohifadhiwa katika akaunti maalum ya ESCROW kutokana na malipo ya mauzo ya umeme iliyoyafanya kampuni ya IPTL kwa TANESCO zilivyoidhinishwa kuchukuliwa.
Kuna baadhi ya watu wasaliti na hata ya baadhi ya vyombo vya habari kushangilia jambo hilo la Umoja wa Ulaya kurejea kutoa misaada kwa masharti ya kisiasa. Wakati mageuzi ya kiuchumi yana anza katikati ya miaka ya 1980, sera za kurekebisha uchumi ambapo Tanzania ilianza kupata misaada kutoka mashirika ya fedha duniani yaani IMF na Benki ya Dunia, ilikuwa lazima misaada ya kiuchumi kutolewa kwa masharti ya nchi husika kutekeleza masharti ya kisiasa.
Baadhi ya masharti ya kisiasa yalikuwa kwamba ni kuachana na itikadi na sera za Ujamaa na Kujitegemea, kuwanyang'anya mawaziri madaraka na kuyaweka mikononi mwa watendaji wakuu na warasimu serikalini na pia kukubali mfumo wa vyama vingi vya siasa na tafsiri ya utawala bora ambayo inatolewa na mashirika ya kimataifa kwa muktadha wa siasa na itikadi za kiliberali.

Kutoa misaada kwa masharti ni jambo ambalo nchi nyingi za Afrika na nyinginezo katika maeneo ya nchi changa zilikuwa zinayakataa. Sababu ya kukataa ni kwamba kila nchi ina historia yake, utamaduni wake, na mchakato wake katika kupata, kulinda na kuboresha uhuru wake na kutengeneza mazingira ya kupata maisha bora kwa watu wake.
Kwamba kila nchi na kila taifa hupitia majaribu yake ambayo kwa namna moja au nyingine yanatengeneza makovu na vilevile mafunzo kuhusiana na kwa vipi taifa linajiamirisha na kujitengenezea ustaarabu wake bila kudhibitiwa na nguvu kutoka nje.
Vita ya kupambana dhidi ya kuwekewa masharti katika kupata mikopo na misaada imepiganwa na viongozi wetu akiwemo Mwalimu Julius Nyerere ambapo katika nyakati tofauti aliwahi kuhoji tangu lini Shirika la Fedha la Dunia (IMF) liligeuka kuwa wizara ya fedha ya nchi wanachama?
Katika hali isiyo ya kawaida nchi za Umoja wa Ulaya zimeanza kuinua vichwa na kutaka kurejesha mfumo wa masharti katika kutoa misaada yake. Kama ni kuamua kusitisha kutoa misaada kwa sababu za kiuchumi na kifedha au kutokana na kubadilisha mikakati ya mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi na nchi, hilo linawezekana. Na wakati mwingine inawezekana kabisa kupunguza kutoa misaada kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani kama ilivyotokea kati ya mwaka 2007 mpaka 2011.

Lakini ni jambo la kishenzi kusimamisha kutoa misaada kwa sababu ya tukio moja ambapo nchi husika zina maslahi katika jambo hilo na hasa kwa kuzingatia kwamba mabenki na mashirika ya nchi hizo kwa namna moja au nyingine yanahusika katika kutengeneza mgogoro.
Ni jambo la ajabu kwamba wakati watu wanashikilia suala la akaunti ya ESCROW ya IPTL kuwa na utata, mkataba wenyewe hauna chembe ya utata na unatamka wazi kwamba fedha zilizowekwa kwenye akaunti ya ESCROW ni mali ya IPTL na serikali ya Tanzania wakati Benki Kuu ni wakala anayetunza akaunti hiyo.
Kwa vipi nchi za Magharibi ambazo zinajua ukweli wa kuhusika kwa mabenki na makampuni yao katika mgogoro wa kifisadi wa IPTL zinatoa shutuma kwa Tanzania na kutoa masharti ya kupata misaada badala ya kushirikiana na Tanzania kuziweka kizimbani kampuni na benki zinazohusika katika mgogoro wa kifisadi wa IPTL?
Katika madai na hukumu zilizokwisha kutolewa nje ya nchi, udhalimu wa IPTL ulikuwa unaibuliwa hasa kuhusiana jinsi wakurugenzi wa kampuni hiyo kwa kushirikiana na mabenki ya nje na wakora walivyokuwa wanatumia njia za kihalifu kuparanganya mahesabu na kufanya kama vile IPTL imekopeshwa fedha kumbe hayo ni madeni hewa ambayo inabebeshwa IPTL.

Wanaonufaika ni wakurugenzi binafsi wa Mechmar na wakurugenzi wa mabenki ya kimataifa.
Kwa mfano tangu mitambo ya IPTL ilipoanza kufua umeme, kiasi kikubwa cha fedha zaidi ya dola milioni 200 zilikuwa zimelipwa kwa IPTL kabla ya kufunguliwa akaunti ESCROW Benki Kuu ya Tanzania.

Fedha hizo zilikuwa ni kiasi kinachotosha kulipa madeni ya IPTL. Kwa vipi wakurugenzi wa IPTL na Benki ya Standard Chartered waliamua kutotumia fedha iliyopatikana kulipa madeni kwa wadai ni kitendawili.
Lakini habari za uhakika zinasema kwamba wakurugenzi wa kampuni ya Merchmar ambayo ilikuwa na hisa nyingi katika IPTL kwa kushirikiana na wakurugenzi wa Benki ya Standard Chartered waliamua kuzungusha fedha walizolipwa na TANESCO badala ya kulipa deni. Kwa upande mmoja watakuwa wamepata faida binafsi na kwa upande mwingine watakuwa wameongeza madeni kwa IPTL na kuchelewesha kupanua uwezo wa IPTL kufua umeme zaidi kwa kutumia gesi badala ya mafuta mazito na kupunguza gharama za uzalishaji.

Sakata la IPTL halikuanza leo ambapo Umoja wa Ulaya na baadhi ya wanachama wake wameamua kusitisha misaada. Tangu awali bendera nyekundu ilishaonyeshwa kwamba kampuni ya Mechmar ambayo ilikuwa inamiliki asilimia 70% ya hisa zote katika IPTL kwa kushirikiana na mabenki na makampuni ya uhandisi yaliyoko Umoja wa Ulaya yalikuwa yamesuka njama za kifisadi kwa madhumuni ya kuhamisha mtaji kutoka Tanzania kwa kubuni madeni hewa na kuzidisha viwango vya uwekezaji ili TANESCO ilipe kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya Capacity charge.
Benki zilizohusika ni benki ya Standard Chartered ya Uiengereza yenye matawi yake Hong Kong, Malysia na Tanzania na kampuni ya Uhandisi ya Watsilla ya Uholanzi na Finland ambayo ilikuwa na kazi ya kusanifu, kufunga na kusimamia mitambo hapa nchini. Kwa nyaraka zilizopo mabenki na makampuni hayo yamehusika kwa kiasi kikubwa katika kukuza mgogoro wa IPTL na kusababisha hasara kubwa kwa maslahi ya Tanzania.
Benki na kampuni hizo kwa nyaraka tofauti yalikuwa yanaghushi nyaraka na kushuhudia uongo kuhusiana na gharama halisi za kununua mitambo na kutoa huduma nyingine za kiufundi na pia kuhusiana na uchukuaji na urejeshaji madeni kwa njia za ujanjaujanja.
Habari za kampuni ya IPTL kuwa na mkakati wa kifisadi ndani na nje ya nchi zilianza kujitokeza tangu mwaka 2002 ambapo kampuni ya VIP Engineering and Marketing ya wazawa ikiwa na asilimia 30% katika IPTL iliyoingia ubia na kampuni yaMechmar ya Malysia kupeleka kesi mahakamani ikitaka itolewe amri ya mahakama ya kuifilisi IPTL ili ubia ufikie kikomo na kila mmoja alipwe haki zake kwa kulingana na hisa alizokuwa nazo na pia faida iliyopatikana.
Kwa upande mwingine mkataba huo unaelekeza namna ya kuingiza pesa zitokanazo na mauzo ya umeme kwa TANESCO, kutoa pesa kwa ajili ya kuwekeza pesa hizo katika miradi mbalimbali na kwa vipi faida itakayopatikana inakwenda kwa nani.

Katika gazeti moja la kila juma (siyo Taifa Imara) liliandika makala iliyosomeka kwamba, "BOT iliwekeza dola za Marekani milioni 22 nchini Ufaransa, iliwekeza shilingi bilioni 48, katika Hati Fungani (Treasury Bills) za siku 182 na shilingi bilioni 8, zilikuwa salio katika akaunti zilizowasilishwa baada ya uwekezaji kufanyika"
Waandishi wa makala hiyo inayozungumzia BOT kutumia kiasi cha pesa za akaunti ya ESCROW kuwekeza katika masoko ya mitaji ndani na nje ya nchi ni jambo ambalo limo katika mkataba wa kuanzishwa kwa akaunti ya ESCROW. Vinginevyo fedha hizo zingekuwa na faida gani kama zingebaki kuwa mtaji mfu (dead capital).
 
Tatizo hii nchi bana hapa utaona hii mijizi inatajwa live bila chenga ila itachoropoka hivi hivi.

Mahakama gani imeamua kesi ya hao wezi, hii nchi inaongozwa na sheria. Tuhuma zimetolewa uchunguzi umeanzishwa na umekamilika, ripoti zimekabidhiwa kwa kamati husika, wakimaliza kuifanyia kazi inapelekwa bungeni wabunge wanajadiri, ya PCCB inapelekwa kwa mwendesha mashitaka kama kuna mtuhumiwa atafikishwa mahakamani. Hizi ndio taratibu, taratibu za kisheria hazina ushabiki kama wakwako.
 
Back
Top Bottom