Wenzetu wanaenda mbele, sisi tunarudi nyuma

Never mkuu
Labda tuache ushirikina na wizi
Nazikumbuka siku zile. Nilikuwa shule ya msingi. Daftari limeisha u aenda nalo, store keeper anatoboa kwa kutumia punching machine, unapewa daftari jipya, kalamu unapewa, kitabu unapewa.

Waliokuwa sekondari, wanakwenda na kurudi makwao kwa gharama ya Serikali.

Nimefika Sekondari, utaratibu ni ule ule, unapewa daftari, tena kubwa zaidi na zuri zaidi kuliko yale ya shule za msingi. Asubuhi chai kwa viazi mviringo, saa 4 asubuhi wakati wa break, mnapata maziwa. Wakati wa likuzo unapewa cash money kwenda na kurudi.

Kufika chuo kikuu unakuwa tajiri mdogo, nauli unapewa ya daraja la pili (zaidi ya nauli ya basi kwa sababu basi ni daraja la 3), mwisho wa mwezi una high learning allowance, una faculty requirements allowance, una book allowance, na una meal allowance. Wakati mwingine unaambiwa kuwa kuna arrears, eti wakati unalipwa travel allowance, nauli ziilikuja kupanda baadaye, wewe mwebyewe mhusika huna hata habaru. Sisi wengine, allowance za UDSM mpaka tuliwasomeshea wadogo zetu private secondary schools.
 
Ila waafrika tunapokuwa tunajaribu kuelezea kwanini tupo nyuma kimaendeleo huwa kila mtu anaongea lake mbali kabisa na mwenzie tunachanganya mambo ambayo hayahusiani na kuwa kwetu nyuma kimaendeleo.
I wish ungeendeleza hii point yako
 

Asilimia kubwa ya hao waliosomeshwa ndo wamekuja kuwa wezi wakubwa....achilia mbali Ile "entitlement behaviour"waliyo kuwa nayo
 
Awamu ya tano ilipoingia viwanda vingi vilikufa
 
Nakumbuka Stephen Kibona rip miaka ile alinunua 504 mpya pale Peugeot House!

Siku hizi mabehewa hadi Kigwangalla machale yanamcheza
 
Haya yanawezekana na yanajadilika. Tupambane tu kuitoa madarakani hili dubwana.
 
Asilimia kubwa ya hao waliosomeshwa ndo wamekuja kuwa wezi wakubwa....achilia mbali Ile "entitlement behaviour"waliyo kuwa nayo
Wizi ni tabia ya mtu. Mbona wengine, kama kungekuwa na jukwaa ambalo nchi nzima wanaweza kukuona, tungepanda juu ya jukwaa hilo na kuuliza kama kuna mtu yeyote ana tuhuma dhidi yetu ya kuiba mali ya mtu binafsi, taasisi au Serikali, na kwa uhakika wa 100% asingepatikana.

Wengi wetu tulikuwa na subira sana. Sip vijana wa siku hizi, wanataka waanze kazi leo, mwezi ujao wawe na magari. Kwa kuwa haiwezekani, anaanza kutafuta rushwa, kuoba na kutengeneza safari zisizo na tija alimradi apate
 
Nakumbuka Stephen Kibona rip miaka ile alinunua 504 mpya pale Peugeot House!

Siku hizi mabehewa hadi Kigwangalla machale yanamcheza
Nyakati zile si wengi walikuwa na magari, lakini wachache waliokuwa na magari walikuwawananunua brand new cars, siyo hii mitumba tunayoinunua leo.

Hata kwenye mavazi, ukivaa mitumba ilikuwa inaonekana wewe ni mtu duni kabisa, ambaye hujiwezi. Na hizo second hand clothes zilikuwa zinapatikana zaidi kwa mapadre_misheni, na mara nyingi zilitolewa bure. Nguo zile tulikuwa tunaziita, "KAFAULAYA"

Namkumbuka Prof. Kweka (RIP) alipokuwa anafundisha Development Studies (DS) pale UDSM, akawa anasema:

"Symptoms of poverty - living on second items. Second hand clothes, second hand cars, some go further, to marry second hand wives because they are not able to pay required dowry for a virgin girl"
 
Mkuu Bams hongera sana. Huwa nasoma mada zako zote hapa jamii forum. Japo hatufahamiani lkn ni wazi kwamba wewe ni mmojawapo wa wenye uelewa mzuri na upo tayari kuisaidia jamii. Mungu akujalie afya njema ya mwili na roho tunaokusoma tuendelee kufurahia na kunufaika na uwepo wako.
 
Asante Bombabomba. Mungu atujalie maisha marefu yenye afya njema ili siku moja tushuhudie nchi yetu ikipiga hatua za maendeleo, maendeleo yanayoonekana.

Na jambo hilo linawezekana sana, kama tukimpata mtu mmoja tu wa kuongoza hayo mabadiliko, na watu wachache wasio na unafiki, watu wa kumsaidia, na kwa hali ilivyo nchini mwetu, mtu huyo ni lazima awe Rais.
 
Mkuu hili la watu kuwa na magari mapya ni kweli kabisa

Tena walikuwa ni kila jamii iwe mswahili au mhindi
Nakumbuka wakati huo hata mkulima wa Tumbaku au Pamba unamkuta ana tractors na Peugeot pembeni au Land Rover halafu wala hatushangai tukijua kilimo kinalipa

Nakumbuka hata father alinunua gari lake la kwanza mwaka 1969 na sikumbuki kama watu walikuwa wanatuona wa kishua bali kawaida tu maana kutwa tunacheza na watoto wa kawaida tu bila kujitenga na shule tunaenda hizo hizo wote

Maisha ya zamani yalikuwa hayana uhasidi na kuoneana wivu kwa sababu kila mwenye nacho, mali zake na anapozipata zinaonekana kwa juhudi zake

Mtu ana Bar kubwa nje Kuna 404 au 504 ni kawaida sana wakati inaweza kuwa 1/10,000

Leo kijana mdogo hata forty hajafika amefanya kazi serikalini kwa mshahara eti ana nyumba 3 na Gari na miradi kibao

Sasa ataacha kufa kwa pressure huyu akijua ni mali ya dhulma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…