Ngonepi
JF-Expert Member
- Jun 2, 2013
- 1,872
- 1,200
Imekuwa ni kawaida sasa viongozi kutoa kauli za kejeli kwa wananchi wanapohoji mambo muhimu yawahusuyo,
Walianza viongozi wengi hapa Tanzania hapo kabla kutoa kauli za kashfa na kejeli kwa wananchi wao wanapoona hawawaungi mkono katika baadhi ya maamuzi yao, lakini wa vile Tanzania haijawahi kupata KIRANJA mwenye kumudu kumwajibisha kiongozi wake anapokosea limekuwa ni tatizo la kudumu sasa sisi wananchi maskini kukashifiwa na kukejeliwa.
Juzi hapa waziri wetu anayehusika na mambo ya UMEME ametuambia kama hatuwezi kununua umeme kwa bei wanayozidisha basi tukae GIZA au tutumie KOROBOI,
Hizi ni kashfa kwetu, ukweli watanzani walio wengi zaidi hatumudu kulipia umeme hata kwa bei iliyopo sasa! Na viongozi si kwamba hawajui!
Wastani wa kima cha mshahara kwa Mtanzania ni ngumu sana kutumia umeme kihalali kama inavyotakiwa. Mara nyingi tumeona operesheni kata umeme mitaani, lakini si kuwa watu tumapenda kudaiwa au tunapenda bure, ukweli ni kuwa umeme ni bei juu mno kwa mwananchi wa kawaida!
Nina ushahidi wa matajiri weengi wanaoiba umeme, na ukiwauliza mbona wanaiba na wanapesa madai ni hayohayo ya bei kubwa ya nishati hii.
Sasa bora viongozi wangekuwa wanakuja na kauli za kistaarabu wanapotaka kutuumiza na si maumivu na kashfa juu yake!!
Nimetaka kuwauliza wenzetu huko KIBAKWE na ninyi mtauziwa bei sawa na sisi jamani!! Taratibu na hizi kauli zenu hata kama mna uhakika hatuna cha kuwafanya wazee!!