Wenzangu mnapata wapi ujasiri wa kuleta mada zinazohusu maisha yenu au ya mtu hapa JF?

T-Bagwell

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
1,190
2,323
Habarini wana JF,

JamiiForums imekuwa ikisaidia watu mbalimbali kwa njia mbalimbali.

Mimi nashindwa kuanzisha mada nyingi sana humu kwenye jukwaa sanasana zinazohusu maisha yangu kwasababu nahisi labda mtu anaweza nitambua kupitia hiyo mada au kama ni mada kuhusu mtu fulani anaweza kuwa na yeye ni mtumiaji wa JamiiForums na akagumiana na hiyo mada na akagundua kuwa ni yeye na mtu aliyeileta hiyo mada ni mtu flani.

Nashindwa kuelewa wenzangu mnapataje ujasiri wa kuanzisha mada humu?

COMMENT YAKO IWE YA MSAADA.
 
Usiogope! Umefichwa nyuma ya keyboard so sio rahisi watu kukushtukia unless utaweka jina lako hadharani...
Mkuu bila jina mtu anaweza kukutambua, kwamfano ukatoa story inayohusu maisha yako, ni rahisi sana mtu wako wa karibu au mtu anayekufahamu kukugundua pasipo hata jina.
 
Tayari nimekwisha kujua, wewe si ndiye yule muoga mtaani kwa akina mwajuma kigodoro?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kuna specific details unaficha na nyingine una twist kidogo, kama unaishi mwanza unasema upo Mbeya, kama nimwalimu unasema wewe nesi, kama una waoto wa 4 unasema 3 au 5, umri waounautwist kiaina pia, lakini kisa kizima kinakuwa generally ni kweli
 
Topic nyingine mkuu zinauwezo wa kumpelekea mtu akakugundua direct, labda kama nyie huwa hamuwazi upande mwingine.
Nyie mnaoweka mipicha yenu DP ndio mnaoharibu... Embu angalia user name yangu, nani atagundua kirahisi kuwa mimi ni fulani? By the way kila baada ya muda huwa nina badili ID name au kufungua akaunti mpya. Hata kama kuna mtu alikuwa ananifuatilia anapotea maboya.
 
Kuna details unaficha na nyingine una twist kidogo, kama unaishi mwanza unasema upo Mbeya, kama nimwalimu unasema wewe nesi, kama una waoto wa 4 unasema 3 au 5, umri waounautwist kiaina pia, lakini kisa kizima kinakuwa generally ni kweli
Tatizo ni kisa mkuu, kwamfano unaelezea kisa kinachohusu mahusiano yako wewe na mwenza wako, unadhani akiikuta hiyo topic atashindwa kuelewa kuwa ni yeye?

Alaf topic nyngne ukizi twist znaweza poteza u reality watu wakahisi umetunga.
 
Nyie mnaoweka mipicha yenu DP ndio mnaoharibu... Embu angalia user name yangu, nani atagundua kirahisi kuwa mimi ni fulani? By the way kila baada ya muda huwa nina badili ID name au kufungua akaunti mpya. Hata kama kuna mtu alikuwa ananifuatilia anapotea maboya.
Kwani nani ameweka yakwake mkuu, sio lazma mtu akufuatilie mkuu only single topic inaweza mfumbua mtu akakutambua au akajua mada inamhusu.
 
Back
Top Bottom