anahitajiushauri
"Ni mwanamke mwenye umri wa miaka 32, ninafanya kazi hapa Dar es Salaam. sasa tatizo lililonileta hapa leo ni kwamba ningependa sana kuolewa na ninaomba Mungu anipe Mume mwema. Nimekuwa na mahusiano mazuri tu na wanaume lakini inapofikia wakati ukigusia masuala ya ndoa inakuwa sumu.Yaani tunakorofishana mpaka kufikia hatua ya kutishia kuwachana.
Kwa sasa nina mwanaume na tumekuwa kwenye uhusiano kwa muda wa mwaka mmoja sasa, lakini nikimueleza masuala ya ndoa ndio inakuwa ugomvi na anaona kama vile namghasi nainafikia hatua tunakorofishana kabisa.
Zake ni kunipiga danadana tu nakuniambia nimpe muda, mimi umri unaenda si unajua tena mwanamke? Yaani hanishirikishi kwenye mipango yake hivyo nashindwa kuelewa. Nikiuliza Muda upi unahitaji? na kwanini tusishirikiane kimawazo?
Nafikiria kuachana nae lakini najiuliza nitaachana na wangapi? Yaani ninapata wakati mgumu sana na ninashindwa kuelewa, je inakuaje mwanamke anaweza kukubaliana na mwenzie vizuri hadi kufikia hatua ya kufunga ndoa?
Au labda mimi napata wanaume ambao hawako tayari kuwa ndani ya ndoa? Naomba mnishauri nifanye nini ili niweze kujua kama ana nia ya kweli au ndio nimechemsha tena!"
USHAURI
Upo tayari Kuwa Mke Mwema au wewe unataka tu Mume Mwema?
Labda huyo BF hajaona kama unastahili kuwa mama wa wanae, kwa mda ulokae naye anaona wewe hutakuwa mke Mwema.
Ndoa ni maisha, kufanya maamzi ya kuingia kwenye Ndoa yanahitaji multiple analysis, Best,more likely na Worse Scenarios, na mumeo mtalajiwa anatakiwa kuyaangalia hayo yote kama ataweza kuya accommodate yakitokea, hasa pale matalajiyo yatakuwa si kama yale aliyotarajia. Anakusoma kwanza Usije kuwa umeficha makucha, chapo hata baadaye binadamu anaweza kubadilika tabia.
Anafikilia huko nyuma files zako zikoje maana the past predicts the future (Trend analysis) japo inaweza kuwa na variations. Kama mulishasimuliana files zenu zako zikamshituwa.
Omba sana, maana Mungu anampa mtu kile kinachomstahili, Huwezi kuomba mume mwema wakati wewe si mke mwema.
Endelea kuomba, Nichunguze ni kipi kilikuwa tatizo kwenye relations za mwanzo na ulikirekrbisha vipi, ni muhimu dada.
Mke/Mume Mwema anatoka kwa Bwana, na wale wamchao Bwana ndo anawapa kile kinachowafanana. Endelea kuomba Utapewa dada.
U