Wenza walio mizigo

hayaa endelea kututumbuaa banaaí ½í¸¢í ½í¸¢í ½í¸¢í ½í¸¢í ½í¸¢í ½í¸¢
 
Ukimpigia simu ameongea jambo la maana saana utaskia nipo jikoni nampikia kaka ndizi.
 
That ought to be a no-brainer especially to someone like you!
My idiocy, foolery, imbecile, and bullshit tolerance threshold is very very low.....

Back to the old self.

Mkuu Nyani heshima kwako. Huwa sina kauli kwenye jukwaa hili zaidi ya kuchungulia kiwiziwizi tu. Ila leo nimekoshwa na shairi mantashau toka kusikotegemewa. Hizo nahau, sarufi, vijembe ... Lakini umetia dosari kurejea ngamani (kwa kina Trump) tena.
 
Ha haaaa uzuzu hadi kwenye umbea....outing na mtu wa aina hiyo lazima uboreke...siasa hayupo...umbea wa bongo movie hayumo.....ujasiriamali hayupo...mzike/movie hayupo khaaaaa!!!! Ila yuuko online kila mara...hivi hata hujui nani na kwa nini flan katumbuliwa???? Inaboa aiseee.....
 
Kuna wenza mizigo, wenza hewa..... Shida tu

Yaani nilipokuwa nausoma huu uzi nilianza kukuwaza, nikiwa na mwenza kama wewe siku hiyo nina issue zangu nimevurugwa unakuja na yale majibu mengine kama haya.
 
Mpenzi au mwenza mzigo huwa ni vigumu sana kumwacha,wanaoachwa ni wale wenye akili timamu pale wanapokosea wakati wanaakili timamu huwa tunahitimisha kwa kusema "nilidhani unaakili kumbe ni puto"
 
Nisahihi kabisa bwana Nyani, unakuta eti kwa mfano ukizungumzia maswala ya maendeleo, yeye ataki anasema achana na kujipa mawazo baby, ehh niambie kesho tutatoka out,? Yaan yeye ana habari hataki kujua hata mshahara wako ni kiasi gani, anachojua yeye ni matumizi tu, fanya ufanyavyo pesa kwake haitoshi, wakati hataki kuuza hata maandazi, hakupi changamoto yoyote ,anafurahia kupanga panga na kuhama hama mtaamzima nyumba zote mmeshakaa,!! kazi sasa anajua upo kazini lakini muda wote anataka kuchart na wewe....nyumbani kwenyewe shida kibao kama ulivyotoka ndivyo utakapopakuta jion, kujiongeza kwake ni kosa la jinai............
 
Ndio maana ya kuchunguzana kabla ya kuona, wanawake wengi mwanzoni huigiza saaaaaana na ndo hapo wanaume wanapohisi wameopoa kumbe wameopolewa
 
Yaani nilipokuwa nausoma huu uzi nilianza kukuwaza, nikiwa na mwenza kama wewe siku hiyo nina issue zangu nimevurugwa unakuja na yale majibu mengine kama haya.
Mie ni precious and sweet mwenza.... Worry not😀
 
NN kwa mimi ni bora huyo kuliko mtu "mjuaji".

Ndio maana dating ni kitu muhimu sana ndipo mahali utapata idea kuhusuu mtu.

Halafu Kuna wengine akili za darasa si kivile lakini yuko "street smart " ni ngumu kusema huyu mtu hana akili kwa maongezi tu.
 
Ndugu Nyani, niliwah kuwa na mtu wa dizaini hiyo yani nishida sana, mkitoka out au ukiwa na rafiki zako unakuwa na hofu sana pindi na yeye akitaka changia mada, mana ataongea pointless mpaka rafiki zako wanabaki kukukodolea macho wew, so kama uko na rafiki yako muelewa anaokoa jahazi kwa kusema "yeah ni kweli shemu usemalo" hahaha pata picha aibu inavyokuvaa na kukunyanyasa, ila dawa ni piga chini aisee
 
Jamani wanaume mmehaswa kuishi na wanawake kwa kutumia akili si vinginevyo.. Chuma unoa chuma.ni hayo tu
 
Alaf bora huyo zuzu awe mwanamke alaf uwe mwanaume kumbadilisha ni rahisi.
Akiwa mwanaume ni kasheshe yaani atajifanya anajua kila kitu.MI naona bora kupiga chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…