Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 93,474
- 119,280
Sabahalkheri waja wenzangu! Natumai nyote mu wazima wa siha tele popote pale mlipo.
Sasa bana kuna hiki kitu kiitwacho akili. Kwangu mimi, kitu hiki huwa nakiona ni changamani sana.
Lakini kwa vile dhumuni la uzi huu siyo kujadili akili Kama akili, basi sitajikita kabisa katika kufasili akili ni nini. Huo ni mjadala wa wakati mwingine na kwa sasa nitasadiki tu kuwa nyote au pengine wengi wenu mnajua akili ni nini.
Nirudi sasa kwenye mada dhamiriwa, hivi mshawahi kutoka na wenzao walio na akili ndogo kulinganisha za zako?
Unakuwa na mwenza lakini unaona kabisa huyu nimemzidi akili tena kwa mbali tu lakini yeye kwa vile hana akili anakuwa hata hajui kama umemzidi.
Asilimia zaidi ya sabini ya kila kitokacho kinywani mwake ni pumba pumba tu....hata kuandika vizuri kwa ufasaha bila makosa ya kitahajia hawezi, kusoma na kuelewa nako hawezi, busara za kawaida nazo hana, lakini hapo hapo haeshi kujiona ana akili na busara sana.
Wenza wa hivyo ni mizigo kwa kweli. Vikubwa waviwezao wao ni umbea umbea tu. Lakini hata kwenye umbea kuna viwango pia. Kuna wengine hata wakiwa wanapiga umbea unaweza kuona dalili za uwezo wao wa kichwani.
Ila kuna wengine hao ndo hamna kabisa. Hata akiwa anapiga umbea unaona kuwa huyu mtu hana akili....ni zuzu flani.
Sasa ndugu zanguni nyie wenza Kama hao huwa mnakabilianaje nao? Piga chini tafuta mwingine au mnavumilia na kuendelea nao hivyo hivyo?