wenyeji wa Mtwara wasaidie

wenyeji wa Mtwara wasaidie

Kipala

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
3,763
Reaction score
700
Naomba wenyeji wa Mtwara wachangie:
ni kata zipi za Mtwara ambazo ni za Mtwara na zipi za Mikindani?
Kati ya kata zifuatazo:

Majengo
Mitengo
Mtonya
Naliendele
Rahaleo
Railway
Shangani
Ufukoni
Vigaeni
 
mtwra mkndani n hzo zote
ila za town kbisa ni majengo rahaleo railway shangani ufukoni vigaeni hzo zngne n mtwra mkndan ila zipo nje ya mji kdogo
 
Hizo zote mkuu zipo katika Halmashauri ya Manspaa ya Mtwara-Mikindani. Ilivyo ni kuwa kabla ya mji wa Mtwara haujaundwa, Mikindani ulikuwepo tangu enzi za tawala za Kiarab, wakati huo Mtwara mjini yakiwa ni mashamba ya mkonge tu. Miaka ya 1950's Waingereza walipobuni bandari ya Mtwara ndipo watu wakaanza kujenga nyumba za makaz hasa ikizinagatiwa Mikindan iko baharini kabisa na imezungukwa na milima. Hivyo mwitikio ukawa ukuaji wa Mtwara kuliko old area-Mikindani. Na kwa pale Mtwara, eneo la mwanzo kabisa lilikua ni Majengo(siku hizi wanapaita Mji Mkongwe).
Sasa ili kutoa kumbukumbu na heshima kwa Mikindani, ikabidi mji uitwe Mtwara-Mikindani. Kumbuka Umabali kati ya Mtwara na Mikindani ni kilometa kati ya 12-15,umbali kati ya Mtwara na Naliendele ni kilometa 10-12. Kimsingi Mji wa Mtwara unaundwa na Mtwara mjini yenyewe, Mikindani na Naliendele. Mfano wake ni kama Kigoma-Ujiji, Iringa na Ipogolo, Morogoro na Kingolowira/Mikese,Kibaha na Picha ya Ndege na miji mingine yenye sifa hizo.

Sasa inapokuja kata, Mikindani siyo kata bali Mikindani ina kata kama nne hivi(Mtonya, Kisungule et al) wakati Naliendele ni kata inayojitegemea na hivyo kufanya kata zote za Mtwara kuwa 15.
 
CHAZA ahsante kwa darasa murua. Una dada weye, ningependa kuja kuoa kwenu ili tuchangie damu.
 
Last edited by a moderator:
hizo zote mkuu zipo katika halmashauri ya manspaa ya mtwara-mikindani. Ilivyo ni kuwa kabla ya mji wa mtwara haujaundwa, mikindani ulikuwepo tangu enzi za tawala za kiarab, wakati huo mtwara mjini yakiwa ni mashamba ya mkonge tu. Miaka ya 1950's waingereza walipobuni bandari ya mtwara ndipo watu wakaanza kujenga nyumba za makaz hasa ikizinagatiwa mikindan iko baharini kabisa na imezungukwa na milima. Hivyo mwitikio ukawa ukuaji wa mtwara kuliko old area-mikindani. Na kwa pale mtwara, eneo la mwanzo kabisa lilikua ni majengo(siku hizi wanapaita mji mkongwe).
Sasa ili kutoa kumbukumbu na heshima kwa mikindani, ikabidi mji uitwe mtwara-mikindani. Kumbuka umabali kati ya mtwara na mikindani ni kilometa kati ya 12-15,umbali kati ya mtwara na naliendele ni kilometa 10-12. Kimsingi mji wa mtwara unaundwa na mtwara mjini yenyewe, mikindani na naliendele. Mfano wake ni kama kigoma-ujiji, iringa na ipogolo, morogoro na kingolowira/mikese,kibaha na picha ya ndege na miji mingine yenye sifa hizo.

Sasa inapokuja kata, mikindani siyo kata bali mikindani ina kata kama nne hivi(mtonya, kisungule et al) wakati naliendele ni kata inayojitegemea na hivyo kufanya kata zote za mtwara kuwa 15.

uko sahihi mkuu
 
Back
Top Bottom