Wenye Uzoefu na Watu Wasiojulikana

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,614
Kuna nukuu za kamanda wa polisi mkoa wa Songwe, nimezisoma kwenye habari katika gazeti la mwananchi, kuhusu uchunguzi wa kutekwa kwa Mdude. Binafsi nipo njia panda.

Nazianisha baadhi ya nukuu kutoka kwa kamanda katika hiyo habari;

Nukuu-Kamanda;

“Mdude hayupo wazi kwani lazima wanapokupiga wanasema kwa nini uliniibia au kwa nini ulifanya hivi au kwa nini umefanya hivi.”

Ulakini;

Je, ni kweli watekaji ni lazima watakuwa wanakupiga huku wanakuambia sababu ya kukuteka?

Nukuu-Kamanda;

“Daah! Unauliza maswali magumu... Mdude mwenyewe hasemi waliomteka akina nani na kama yeye mwenyewe anasema hawajui, unafikiri sisi tutajua kweli? Anapaswa kusema gari lilikuwa na namba fulani, walioniteka walikuwa wanasema hiki, hiki na hiki, ili na sisi tuanzie hapo,” alisema kamanda Kyando."

Ulakini;

• Hivi ukitekwa kwa purukushani, ghafla unafunikwa usoni kwa kitambaa, je, unaweza kuzifahamu namba za gari? Je, lazima watekaji waje na gari likiwa na namba za usajili?

• Je, watekaji huwa ni lazima wawe wanazungumza ndani ya gari? mfano, tumpeleke mtaa x kwenye ile nyumba! au pita barabara ya samora!. Kwani watejaji huwa hawajipangaki mapema mpaka waanze kuongea ndani ya gari? Kwani watekaji hawawezi kutekeleza mambo yao kimya kimya?

Nukuu-Kamanda;

“Tukimuuliza walipokuwa wanakupiga walikuwa wanakuambia nini? Hasemi. Sasa hapo tunafanyaje? Kimsingi majibu rahisi ni kwamba bado uchunguzi unaendelea, ukikamilika tutawaambia.”

Ulakini;

Je, ni lazima watekaji wakuambie kitu wakiwa wanakupiga? Je, hawawezi kukupiga kimya kimya?

Chanzo; Gazeti la Mwananchi;
 
Polisi wameweka vyeti pembeni maana anayewapangia cha kufanya pia alipata ZERO

ni aibu kwa wenye elimu zao, mafunzo ya kitaalamu, uzoefu, heshima ya kazi na manishani kibao ya utendaji uliotukuka kutumwa kazi zisizo za ki ueledi na.aliyepata SUFURI

majitu yapo makao makuu polisi pale yanakula chai ya maziwa na mayai, kuku mpaka dawa za ARV yanaletewa mezani mradi yaendelee kusambaza ukimwi kwa askari wa kike wasio na nguvu ya kuwakataa, hayafanyi kazi yaliyotumwa yanaangalia upepo wa wenye ZERO wanakovumisha! AIBU
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom