Wenye tabia hizi wapo wengi tu naomba mbadilike

Wenye tabia hizi wapo wengi tu naomba mbadilike

Pilot_In_Command

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2013
Posts
2,507
Reaction score
3,460
Habari wakuu,
kuna katabia fulani kapo miongoni mwetu.. au baadhi yetu tunakutana na hichi kitabia

mtu hakutafuti.... masiku/wiki/miezi... hakuna salamu hakuna kujuliana hali..

ikikalibia sikukuu ndio wa kwanza kupiga anaomba hela

akikwama kufukuzwa katika chumba chake ndio anakutafuta umsaidie

akikamatwa na polisi ndio wa kwaanza kukukimbilia umtoe jela

wengine mshipa wa aibu hawana wao wanatuma sms ya kukuomba hela utazan ulikuja DUNIANI kwa ajili yake..

Mtu unamsaidia,basi hata shukrani hakuna,unatuma hela asemi kama kaipata... ukimpigia simu ndipo anajichekesha ... alaf ukikata simu.. kimyaaa.... mpaka umtafute wewe.. au apate tena shida ndipo akutafute... mie huwa nawaonaga kama WACHAWI tu.

wenye TABIA hizi wapo wengi tu naomba mbadilike
ingawa tenda wema nenda zako.. usingoje shukrani.. basi tuwe tunawasiliana mara kwa mara na sio hadi wakati wa shida tu

MCHAWI NDUGU,WACHUNGUZE WA KWAKO.
 
Sasa kuna wale hajawahi kukutafuta , ,akitaka kuoa au kuolewa atakutafuta kwa udi na uvumba,,,anataka mchango. harusi ikiisha humuoni tena hata salamu,,siwapendi nyie watu wa hivo mfyuu
 
Sasa kuna wale hajawahi kukutafuta , ,akitaka kuoa au kuolewa atakutafuta kwa udi na uvumba,,,anataka mchango. harusi ikiisha humuoni tena hata salamu,,siwapendi nyie watu wa hivo mfyuu
Wapo wengi tu.. hii michango ya HARUSI ndio pasua kichwa.... ndio hivyo wengine tuna mioyo ya aibu tunajibana tunatoa tu
 
Ukiona hivyo wewe ni muhimu kwao, watekelezee wanachohitaji halafu ondoka kwa furaha.

Hata Mshumaa huwa unakumbukwa wakati wa Giza totolo ili uweze kutoa mwanga pale penye giza.

Huwa nawapenda sana watu wanaonikumbuka wakiwa na shida tu.
 
Leo umeongea point..
 
hiyo tabia sio poa kabisa. lakini kwa nini na wewe usiwatafute kuwajulia hali kabla ya wao kukutafuta wakiwa na shida.
mimi siwezi kulaumu maana moja ya udhaifu wangu ni kupigapiga simu kila mara.
mie huwa nawatafuta.. na naendaga hadi wanapoishi nawajulia hali.. naondoka sas ukifanya kwa muda mrefu alaf unaona wao wame kaa kimya kwa harak haraka unachukulia kama unajipendekeza.. basi mie nakausha na dili na mishe zangu.. utashangaa baada ya muda wanaanza kuomba mia mia
 
Ukiona hivyo wewe ni muhimu kwao, watekelezee wanachohitaji halafu ondoka kwa furaha.

Hata Mshumaa huwa unakumbukwa wakati wa Giza totolo ili uweze kutoa mwanga pale penye giza.

Huwa nawapenda sana watu wanaonikumbuka wakiwa na shida tu.
Kaka upo?

Naomba unikopeshe elfu hamsini narudisha mwisho wa mwezi
 
Hahaha huwa hawaanzagi direct, anakupigisha kwanza stori(anakuweka Sawa) ndio baadaye utasikia "Kaka nilikuwa na shida"
hehehe...
usijikoroge kuuliza "vipi mambo yanasemaje"
hapo jibu ni "daah kaka.. hali ni mbaya"
hapo jiandae kupokea RUNGU..
 
Tafuta hela usitafute marafiki hii ndio kauli mbiu yangu. Rafiki anaweza kuwa mnafiki au akakusaliti.
Hela haiwezi kukusaliti au kuwa mnafiki bila ya wewe kuitumia na kukupa faraja pia hela inaleta heshima. Kama huamini nenda ukweni ukiwa huna mapene halafu baada ya miaka ukishapata mapene nenda tena utaona heshima utakayopewa.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom