Kweli Tanzania inajengwa na wenye moyo, lakini wenye meno wamezidi kasi ya wenye moyo...........hivyo ulaji ni mkubwa kuliko uzalishaji........ guess what? ......umasikini ndo unaongezeka maana wanakula mpaka visivyo vyao
.
Ni kweli kabisa lakini siku izi mambo ni tofauti kabisa yani watu wanatumia madaraka kujilimbikizia utajiri wa nchi...kwa hali hii hatutafika kokote zaidi ya kufundisha kizazi kinachokuja nacho kufanya maovu haya...itafika mahali wenye moyo watachoka na ndipo watakapoanza kutafuta njia ya kuikomboa nchi yao kwa nguvu...am out
Anza kujitokeza wewe,kwani wewe ndio kiini cha maovu yote yanayotokea katika jamii aidha kwa kuyashabikia ama kuyafumbia macho ama kumnyooshea tu mtu kidole na kushindwa kureact...........take good example kwa yule mwanafunzi wa tunisia ndo nawe uanzie hapo,usipoweza better uhame jf
..Kweli kabisa mkuu nakumbuka wakati nilipokuwa nakula kiapo cha chipukizi...kuwa mimi ni chipukizi wa Tanzania, nitaitumikia na kuilinda nchi yangu ya Tanzania, muda wowote, mahali popote..ewe mwenyezi mungu nisaidie....ilikuwa inatoka ndani ya moyo kabisa..lakini sasa mambo hovyo hovyo!
Umenikumbusha nyimbo za kipindi kile wakati nikiwa Kinda zilikuwa hivi........Taifa litajengwa na wenye moyo, Iya Iya na wenye moyo.......Taifa litajengwa na kina nani.......... Iya iya na wenye moyo......
Yaani nakwambia tulikuwa tunapewa na kujengewa moyo wa Utaifa na Utanzania zaidi.