Wenye miaka 40 hatuajiriki?

Wenye miaka 40 hatuajiriki?

Wanaogopa mtaenda kulala tu huko maofisini

kabla hujapost mchango wako, jaribu kuutathmini kama unamantiki! Kwa taarifa yako wengi wa wafanyakazi wa vyeo vya juu wana umri zaidi ya miaka 40. Na ni watendaji wazuri tu!
 
Miaka 40 unaeweza kiingia ktk siasa na kugombea Urais..
 
Kaka...at 40 bado unafikiria kuwa mtumwa???? mimi hapa nina hit 40yrs this yr na nilishajipanga kustaafu toka utumwani but pia naona nimechelewa sana kufanya hivyo ingawa nilishajiandaa more than 5yrs ago..!
 
Miaka 40 ushazeeka

usimkatishe tamaa. 40 bado ni kijana mdogo.. katika mazingira ya kawaida na hizi technologia na kwa mujibu wa ILO productive age ni 70 years. kwa hiyo bado ana miaka 30 of active production.
 
Kwanini kila tangazo la kazi hata za serikali inakuwa na kipengele cha umri kuwa "kuwa asiwe zaidi ya miaka 35" wakati serikali inajua kuwa sisi amboao tuko katika rika hilo walitukosesha elimu na wengine tumekuja kujisomesha wenyewe kwa mategemeo kuwa siku moja nitapata kazi lakini hali sivyo;

Utashangaa taasisi za umma,viongozi wakitoa masharti haya ya kipumbavu na kibaguzi.lakini cha kushangaza wao wanahama kazi kila siku!.

Hii nchi vipi?,

hakuna haki kabisa,watu hatuna lili wala lile,basi tupeni hata mkopo kama basi!,jamani hii nchi gani ambayo oppotunities zipo kwa kundi fulani tu.....heri uwe panya road,tumechoka!,unaomba kazi mpaka unashikwa na uchizi!

Nina amini baba au ndugu yangu angekuwa na nafasi huko nisingeteseka hivi ktk ardhi hii
.

Sasa Wataajiri Vipi Mwenye Miaka 40 Wakati Ndiyo Anaelekea Kufa? Waajiri MFU Mtarajiwa? Hatutaki Hasara!
 
Back
Top Bottom