Wenye "madingi" wakali tukutane hapa

Baba akuwa mkali kwakweli. sijui nilipokuwa Mdogo ilantangu nilipopata Akili sikumbuki Kama alishawahi kunyanyua mkono wake kunipiga, Ila mtiti kwa bi mkubwa ni balaa.

Ilikuwa inafika kipindi ukichezea bakora kwa mama Baba anagombelezea Apumzike kwa amani.
 
Mshua alinichapaga viboko mbele ya demu wangu alikuja kusuka.
Dingi amekuja mchana kula chakula akakuta hakuna maji hata ya kunawa mikono, kubabake alinichapa sticki hizo.
Demu wangu alikua nje anasukwa na dada yangu, dingi ananichapia sebuleni.
Kwa kuwa nilikua sitaki demu wangu ajue kama nachapwa, nikawa najikaza sipigi kelele.
Dingi akajua viboko havini umizi, akaanza kunipiga na mavibao, kubabake nilivimbaga mikononi.
Mara Paaaap nikatoka na mindoo kwenda kuchota maji, mialama ya viboko kwenye matako, mgongoni, mikononi.
2001 hiyo Kiloleni Tabora
 
Mzee alikua anasema kama unajiona upo vizuri njoo tuzipange.

Alikua hapendi mtu anyoe kipara, kaka yangu akawa mbishi siku hiyo karudi home na kipara. Mzee akamwambia kimbia ukiona upo mbali sema tayari.

Jamaa akakimbia mzee anaona mdau anasogea tu hasemi tayari, akamuungia. Dakika kadhaa mbele tunaona kaka anarudishwa kabebwa begani.
Kufika home akaambiwa tuzipange, ghafla jamaa kapiga magoti analia anaomba msamaha.

Mzee akamwambia adhabu yako utakua unapaka kiwi kichwa hadi nywele ziote.
 
Madingi wakali dawa yao wapelekee wajukuu tu sasa hivi wanavyozeeka uone.
true yaan wanavyopelekwesha hadi unajiuliza hivi ndo yule Dingi yangu bandidu ninayemjua mimi au
mana wanakuwa wa pole kupita viwango mbaya zaidi anafanyiwa vitu ambavyo wewe mwenyewe mwenye mtoto kimfanyia usingeweza wanawadekeza zaidi ya maraika
yaan utasikia tu acha nitakuchapa
kama kuna kiti chake cha uzee hakai mtu lkn huyo mjukuu wake anapanda na michanga tena wakati mwingne wanabanana hapo kukaa kiti kimoja
station ya tv anachagua yeye
wkt enzi nzake thubutuuuu uweke station unayotaka wewe wakati yeye yupo kwanza utaanzaje
 
Mshua alinichapaga viboko mbele ya demu wangu alikuja kucheza kwetu.
Dingi amekuja mchana kula chakula akakuta hakuna maji hata ya kunawa mikono, kubabake alichapa sticki hizo.
Demu wangu alikua nje anasukwa na dada yangu, dingi ananichapia sebuleni.
Kwa kuwa nilikua sitaki demu wangu ajue kama nachapwa, nikawa najikaza sipigi kelele.
Dingi akajua viboko havimizi, akaanza kunipiga na mavibao, kubabake nilivimbaga mikononi.
2001 hiyo Kiloleni Tabora
Dah mdau kumbe wewe niwanyumbani kabisa tabora
 
Mimi nakumbuka siku ya mwisho dingi kunichapa.....alinikuta nasoma saa sita usiku yeye yuko nzwiiiii......akaniuliza kwa nini sijalala, nikamjibu huoni nafanya nini.....akajaa povu....akafuata fimbo kwani alikuwa anaziweka sehemu......akaanza kunitandika......nilitulia tuu, ila ikafika wakati nikasema leo lazima nimuonyeshe huyu mzee......niliikamata ile fimbo na nikaivunja vipandevipande.....kulikuwa na music system ya Phillips niliifuata na nikaivunja vipande vipande.......nikaenda kwenye kabati la vyombo....nililiangusha na almost vyombo vyote vya udongo vilivunjika.......ndio ilikuwa mwisho wa mzee kunichapa......
 
true yaan wanavyopelekwesha hadi unajiuliza hivi ndo yule Dingi yangu bandidu ninayemjua mimi au
mana wanakuwa wa pole kupita viwango mbaya zaidi anafanyiwa vitu ambavyo wewe mwenyewe mwenye mtoto kimfanyia usingeweza wanawadekeza zaidi ya maraika
yaan utasikia tu acha nitakuchapa
kama kuna kiti chake cha uzee hakai mtu lkn huyo mjukuu wake anapanda na michanga tena wakati mwingne wanabanana hapo kukaa kiti kimoja
station ya tv anachagua yeye
wkt enzi nzake thubutuuuu uweke station unayotaka wewe wakati yeye yupo kwanza utaanzaje
Madingi wanaokubali kupelekewa wajukuu hao si wakali, wale wababe wa vita mjukuu akija asalimie na kusepa, hawana muda wa kulea mtoto na mjukuu!
 
Mkuu baba yako alipofariki (RIP) Baba angu ndo alishika ukanda wote wa maziwa..Kig, mwnz, Tbr, Sh, Kagr.

Huyu jamaa unaweza sema sio baba yako hana lugha rafiki hata kidogo..

Alijaliwa mimacho makibwa akikuangalia tu unakua mdogo..

Huyu jamaa aliniwekea watu wa kunichunga nisiongee wala kusimama na msichana.

Tushawah changia dem na hili jamaa, Siku nyingine tukakutana gest mm naingia yy anatoka..

Kanishinda 22yrs
hahaha.... kwahyo dingi angu ndio muasisi
 
Mwaka 99, enzi hizo simu ya mezani, alikuja mgeni akaomba simu apige hapo simu inakaa chumbani, nikamwambia dingi mgeni anaomba simu, dingi akaguna tu nikajua kakubali nikatoa simu mgeni kaongea alivoondoka mweh!!!!
Nlichezea kichapo heavy yani mvua ya stiki..... Apumzike kwa amani mdingi
We mhenga 99 nlikuwa nna miaka mitano
 
Mkuu baba yako alipofariki (RIP) Baba angu ndo alishika ukanda wote wa maziwa..Kig, mwnz, Tbr, Sh, Kagr.

Huyu jamaa unaweza sema sio baba yako hana lugha rafiki hata kidogo..

Alijaliwa mimacho makibwa akikuangalia tu unakua mdogo..

Huyu jamaa aliniwekea watu wa kunichunga nisiongee wala kusimama na msichana.

Tushawah changia dem na hili jamaa, Siku nyingine tukakutana gest mm naingia yy anatoka..

Kanishinda 22yrs
Duh noma
 
Mwaka 99, enzi hizo simu ya mezani, alikuja mgeni akaomba simu apige hapo simu inakaa chumbani, nikamwambia dingi mgeni anaomba simu, dingi akaguna tu nikajua kakubali nikatoa simu mgeni kaongea alivoondoka mweh!!!!
Nlichezea kichapo heavy yani mvua ya stiki..... Apumzike kwa amani mdingi
nimechekaaa...kujifanya mkarimu kuliko mwenye simu yake ndio nini sasa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom