wenye hela mnaitwa huku

mkuzi

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2013
Posts
1,627
Reaction score
1,462
MWIGIZAJI wa kike wa filamu Kibongo Husna Chobis ‘Awena’ amesema kuwa baada ya kurudi katika biashara zake nje ya nchi yupo tayari kuolewa lakini kwa mwanaume mwenye fedha za kutosha na siyo mbabaishaji.

Akifafanua zaidi, msanii huyo amesema hawezi kuolewa na mwanaume ambaye hawezi hata kumiliki Bajaji.

Pia, amedai kwamba mwanaume mwenye fedha za kubadilisha mboga hana mpango nao.

“Kuzaliwa katika familia ya kimaskini ni bahati mbaya, lakini kuchagua mume maskini ni uzembe na hustahili kusamehewa,” alisema.

Aidha aliongeza kuwa kutembea kwake amejifunza mambo mengi na kuona mastaa wa Ulaya huwa wanaolewa kwa maslahi.

Mwigizaji huyo aliyejizolea umaarufu katika Filamu ya Ndase, alisema moja ya matatizo ya ndoa za Kitanzania au Kiafrika ni kukosea katika uchaguzi na kuingia katika uhusiano.

“Wengi huishia kupotezeana muda kisha kutengana kutokana na kuwa uzembe wa kukosea katika uchaguzi wa mume au mke,” alisema.
 
Biashara gani anafanya nje ya nchi?
 
hao ndo wanakaa sana, wanapata yenye hela yanaishia kuwagegeda tu alaf akijastuka hata maskini wa kumuoa anamkosa. Mi namtafta maskin mwenzangu
 
Maana anafanya biashara ambayo hawezi kuiweka wazi....nje ya nchi utasikia ni China tu.

Kama ana hela anataka mtu mwenye hela wa nn?
 

Huko alikotoka hamna wenye hela? Angeolewa huko huko!
 
Tamaa inawaponza wanawake wengi sana...wanaolewa na mababu zao kisa chapaa
 

Staa gani, mavi tu!
 
Ndo nani huyo Chobizi, umesema ni housegirl huko dubai eti? na hiyo filamu iliyomzolea umaarufu inaitwa nini??
 
Mi hata simfahamu! Au coz mi si mpenzi wa maigizo ya kitanzania?
 
Itakuwa ile biashara ya ukahaba kule China,sio nyingine
 
Hawa mademu dizaini ya Aunt Ezekel sio kabisa. Ukimpata atakua anapenda hela zako tu ukifulia wanakutema mazima. Sunday yuko zake jela uarabuni mwenzie Anty Ezekiel anakula bata hapa bongo hakumbuki hata kama alikula bata na hela za mchizi.
 

Nani kaiona kesho ? Kama hivi ndivyo anavyofikiri basi wasanii wetu wana safari ndefu !
 
Demu mbaya kuliko hausgel wangu.

Halafu anataka wanaume wenye hela.

Akaolewe na ATM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…